Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

Dally Kimoko amepiga gita kwenye ngomà nyingi ninazozipenda kulinganisha na Diblo. Kimoko ni zaidi.
Nilitaka kusema hilo.
Diblo ni maarufu sana kwenye nyimbo za Jean Baron na zake kama Matchatchaa.
Lakini Daly Kimoko amepiga nyimbo nyingi na nzuri kuliko Diblo. Angalia album zote za Loketo ndio utajua Kimoko ni nani.
 
Diblo ndiye mfalme na kama angezaliwa ulaya au marekani angekua idolized kama jimy hendrix.
Achana na Daliki Moko. Yeye gitaa lake uimba na mrindimo utausikia ndani ya damu yake. Diblo ni mkali lakini vibration zake ni haraka haraka haziingii kwenye damu bali utacheza kwa sababu umesikia ila Daliki Moko utacheza kwa sababu umeguswa
 
diblo-jpg.98062
 
...accoplished? Huna haja ya kuandika Kiingereza kwa papara. Unafikiri google ndio kila kitu? Hapa tunafananisha wapiga solo. Tosh alikuwa mpiga solo?


Hapo Tosh anapiga nini mkuu!?!?
 


Hapo Tosh anapiga nini mkuu!?!?
Kwa hiyo ndio unataka kumfananisha na Dally au Diblo? Narudia tena: Tosh hakuwa mpiga solo. Alikuwa anapiga gitaa ndio; lakini huwezi kwa aina yeyote ile kusema Tosh alikuwa mpiga solo kama Dally Kimoko au Diblo Dibala.
 
Mkuu umesema Tosh hapigi Solo ndio maana nimekuuliza hapo ndani kapiga aina gani ya gitaa.!?!?
Sijamfananisha na hao wakongo.
Nataka unisaidie tu hilo ni aina gani basi!
Kwa hiyo ndio unataka kumfananisha na Dally au Diblo? Narudia tena: Tosh hakuwa mpiga solo. Alikuwa anapiga gitaa ndio; lakini huwezi kwa aina yeyote ile kusema Tosh alikuwa mpiga solo kama Dally Kimoko au Diblo Dibala.
 
...
Nataka unisaidie tu hilo ni aina gani basi!
Kudonyoa gitaa hakukufanyi uwe mpiga solo. Narudia tena; Peter Tosh hakuwa mpiga solo. Alikuwa anapiga gitaa? Jibu ni ndiyo. Alikuwa mpiga solo? Jibu ni hapana. Hiyo clip ya Stir it Up inamuonyesha Bunny Wailer kwenye percussion. Je Bunny Wailer ni percussionist au mwimbaji? Kama Tosh alikuwa ni mpiga solo kulikuwa na umuhimu gani kwa yeye kuwaajiri Al Anderson, Mikey Chung au Earl "Chinna" Smith (kwa nyakati tofauti) kwenye bendi yake baada ya kufarakana na meneja Chris Blackwell na kuamua kujitoa kwenye The Wailers? Wapiga solo wa Jamaica enzi hizo naweza kuwataja watu kama Ernest Ranglin, Al Anderson, Don Kinsey, Earl "Chinna" Smith au Junior Marvin.

Hebu sikiliza hawa wapiga solo wa Bob.


Hapa jaribu kumsikiliza Ernest Ranglin


Na hapa sikiliza solo la Earl "Chinna" Smith


Au unaweza kusikia solo guitar la Stephen Marley (mpiga solo wa I Jahman Levi) kwenye Jah Heavy Load


Diblo Dibala "Kelele"


Halafu endelea kuniaminisha kuwa Peter Tosh alikuwa mpiga solo.
 
Kimoko Anaonekana Mkali Kwasababu Kapga Wanamziki Wengi Mf Pepe Kale, Bongoman, Yondo Sister, Nk Na Inasemakana Anatumia kipaji, Hajasomea Hvo Hupga Vpande Vipande. Dibala Yeye Gitaa Lake Ni La Kitabuni Hvo Analijua Gitaa Lote A To Z, Ss Wengine Wanadai Ni Mpigaji Ghali Wengine Wanadai Hayuko Flexible Km Kimoko. Yaan Hupga Vle Anavojua Yeye Au Alivosomea Tu, Ukimtoa Nje Ya Kitabu Hana Ujanja. Lkn Kimoko Alikua Anaweza Kutimiza Kile Anachotaka Mwanamuzi, Alikua Anaweza Kupga Vyovyote Unatotaka Ww. Wanasema Alikua Genius Wa Gita
 
Soukouss Stars, ukiondoa Wenge Musica, hawa jamaa miaka ya 90 ilikua ni shidaa
Balu Canta, Shimita Ngouma Lokhito, Kusala Yondo Sister,Dally Kimoko, Sahladin ilikua ni hatari
Mmemsahau kijana mdogo Bokilo
 
Back
Top Bottom