Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

Dally kimono na Diblo dibala, wote ni wapiga solo guiter. Lakini wanatofautiana kwa jinsi ya upigaji wao. Upigaji wa Kimoko ni kama ule wa Nene Tchacou, Saladine, na hata Nguza Viking. Hawa niliowataja hapa, upigaji wako unalingana ila wanatofautiana katika spead ya kubadili chords,(major, minor). Katika hawa niliowataja, Kimoko ni zaidi yao... Kundi jingine ni la Diblo, Jacob Desvarioux wa Kassav, Abel Balthazar wa Msondo, Said Mabera, wa msondo. Group hili, ni tofauti na like la amina Kimoko. Hawa upigaji wao hutumia major, minor, diminish, na minor7 chords. Upigaji wa kutumia chords hizi, humfanya mpigaji kuhama Mara kwa Mara kutoka chord kwenda chord. Hivyo, sauti ya guitar inakuwa rhythmic zaidi. Kwa kutumia hizi chords, mpigaji anaweza mziki wa kasi au slow. Kati ya hawa, Diblo anaongoza akifuatiwa na Jacob wa Kassav lakini kwa tofauti ndogo sana. Said Mabera utauona ufundi wake has a anapopiga nyimbo za mitindo ya Latino, na cha cha cha...Kwa hivyo, upigaji kati ya Diblo na Kimoko ni tofauti kabisa japokuwa wote hupiga mziki wa kasi. Mwangalie Diblo kwenye wimbo "mbuta Nzau" hapo ndio utona tofauti take na kimoko japokuwa wote wanapiga solo guiter.. Dally Kimoko anapiga sharp solo guiter, na Diblo Dibala, anapiga rhythmic solo guiter..
 
Jina analotumia Mourinho hivi sasa "special one" lilishatumika enz hizo,
Hongera kwake majinaa wang, njoo niko nampendaka sana anayuaka kupiga gita muzuri, vile ukisikiaka Moko maana yake "pekee" "Special one" au "moya"
Sikilisaka "maya maya" ya Nyboma utamyuaka huyu mutu kwa nini ni Moko
 
Dally kimono na Diblo dibala, wote ni wapiga solo guiter. Lakini wanatofautiana kwa jinsi ya upigaji wao. Upigaji wa Kimoko ni kama ule wa Nene Tchacou, Saladine, na hata Nguza Viking. Hawa niliowataja hapa, upigaji wako unalingana ila wanatofautiana katika spead ya kubadili chords,(major, minor). Katika hawa niliowataja, Kimoko ni zaidi yao... Kundi jingine ni la Diblo, Jacob Desvarioux wa Kassav, Abel Balthazar wa Msondo, Said Mabera, wa msondo. Group hili, ni tofauti na like la amina Kimoko. Hawa upigaji wao hutumia major, minor, diminish, na minor7 chords. Upigaji wa kutumia chords hizi, humfanya mpigaji kuhama Mara kwa Mara kutoka chord kwenda chord. Hivyo, sauti ya guitar inakuwa rhythmic zaidi. Kwa kutumia hizi chords, mpigaji anaweza mziki wa kasi au slow. Kati ya hawa, Diblo anaongoza akifuatiwa na Jacob wa Kassav lakini kwa tofauti ndogo sana. Said Mabera utauona ufundi wake has a anapopiga nyimbo za mitindo ya Latino, na cha cha cha...Kwa hivyo, upigaji kati ya Diblo na Kimoko ni tofauti kabisa japokuwa wote hupiga mziki wa kasi. Mwangalie Diblo kwenye wimbo "mbuta Nzau" hapo ndio utona tofauti take na kimoko japokuwa wote wanapiga solo guiter.. Dally Kimoko anapiga sharp solo guiter, na Diblo Dibala, anapiga rhythmic solo guiter..
Wewe unajua muziki sasa,dally kimoko mwanzo mwisho anakuwa na key moja,ila diblo alikuwa anabadilisha key sana,na guitar inaongea unaisikia kabisa
 
Fredito Ndalla Kasheba, huyu bwana simlinganishi na hao kina Diblo na Dally Kimoko, lakini huyu bwana alikuwa akipiga solo guitar lenye nyuzi 12. Masololist wapo wengi tu wazuri, hata marehemu Dr Remmy Ongalla naye alikuwa mkali kwa solo guitar. Yule aliyewahi kuwa mwenyekiti wa simba sports club Mzee Hassan Dalali naye pia ni mkali wa solo. Msikilize kwenye wimbo wa vijana jazz uitwao Ngoma umekuwa mwamba ngoma.
 
Dally Kimoko, ana speed Kali katika kutembeza vidole wakati anahama kutoka chord kwenda chord. Lakini chords anazotumia ni za kawaida,(major,minor chords)ambazo mafungu mwili tu. Diblo yeye anatumia chords nyingi zaidi ya Kimoko.(major, minor, minor 7, diminish chords). Ukichanganya diminish, pamoja na minor7 chords, gita litatoa sauti Kali na laini (rythymic sound). Diblo Dibala yuko daraja la waliosomea muziki kama vile marehemu Michael Ennoch aliyekuwa Dar Jazzo.
 
Sikumbuki kama kuna wimbo wa Pepe Kalle ambao solo ilipigwa na Diblo Dibala lakini nakumbuka wimbo kama Hidaya wa huyo huyo Kabasele Yampanya a.k.a Pepe Kalle solo ilipigwa na Dally Kimoko....

Dally Kimkoko amepigia wengi sana kwasababu hakuwa na maringo wala bei kubwa na hili lilimuinua sana na kumfanya kuonesha kipaji chake cha hatari kabisa kwa watu wengi.....
Pon Mon Paka Bouge amekung'uta solo mtu mzima Diblo Dibala!
 
Diblo guitar mpaka liwe computerized ukumbini hora! Nenda you tube uangalie pepe kalle abdjan 1991 ya ukumbini Dally na Caen Madoka wanavyochangamsha ukumbi anaitwa Dally kwanza!
Caen Madoka alimbeba sana Aurus Mabele!
 
Back
Top Bottom