Nani huwa inamkuta hii?

Nani huwa inamkuta hii?

Pombe zilivyo nyingi mpka hali hiyo ikutokee utakuta wewe ni mbwiga sana
Waliokunywa pombe kwa sababu ya Hali kama hio wengi wamekufa ama wamejiongezea matatizo zaidi ikiwemo matatizo ya Figo, kisukari n.k ila wenye makampuni ya pombe tena hizo Kali wanazidi kua matajiri.
 
😂 😂 😂 😂 asee usiombe hiyo hali ikukute, hata simu yako ikiita hutamani hata kuangalia anaepiga ni nani.
Hiyo hali nimeipitia kuanzia mwezi wa tatu Hadi wa nne kila kitu hakiendi hata buku haupati unajiona ni mtu ambaye hakuna zuri unaloliona!

Nilimshirikisha rafiki yangu mmoja akanielekeza sehemu niende, nikaenda nikapata tiba kwakweli mambo Yalienda vizuri Hadi Sasa na Mshukuru Mungu.
 
Waliokunywa pombe kwa sababu ya Hali kama hio wengi wamekufa ama wamejiongezea matatizo zaidi ikiwemo matatizo ya Figo, kisukari n.k ila wenye makampuni ya pombe tena hizo Kali wanazidi kua matajiri.
Kufa ni kawaida tu kitu gani ukinywa haufanyi matajiri wazidi kuwa matajiri, hizi ndizo akili za hovyo nani kakumbia mimi nipo kuishi ili nifanye watu wa makampuni ya pombe kuwa mskini?
 
Hiyo hali nimeipitia kuanzia mwezi wa tatu Hadi wa nne kila kitu hakiendi hata buku haupati unajiona ni mtu ambaye hakuna zuri unaloliona!

Nilimshirikisha rafiki yangu mmoja akanielekeza sehemu niende, nikaenda nikapata tiba kwakweli mambo Yalienda vizuri Hadi Sasa na Mshukuru Mungu.
Tangazo liko very strategic.😃😀
I hope Wateja wameshaanza kumiminika DM
 
Mademu sitaki, mziki sitaki kusikiliza, kuangalia muvi sitaki, kamari sitaki, kushusha bendera kwa mkono mmoja nayo sitaki, kupendeza sitaki, kwa kifupi sijipendi, tofauti na zamani, napenda ku stay alone muda mwingi, sijielewi nimepagawa , marafiki wachache sana nimebaki nao,
Sema we jamaa unajikataa vibaya mpk kushusha bendela kwa mkono mmoja hutaki?
 
Haya mambo yaliwah nitokea zaman nikaamua nijitoe uhai ila sikufa mpaka leo huwa nashangaa ilikuwaje nikapona

Baadae nikapata mambo yakaenda vzur sana lakin sahv hali imerudi tena

Hilo pozi la huyo alieketi ni mimi kabisa nikiwa nimemaliza kula na hapo ukute mke yupo pemben ananipa malalamish mara sjanunua hiki mara kile

Ila kwasasa nilishaapa staweza tena kurudia kujitoa uhai,ni bora nikimbie familia
Kwanini uikimbie familia? Komaa hapo hapo. Badilisha tu mindset, kuwa happy all the time, train ubongo wako kuwa happy katika mazingira yeyote.
 
Ndo ujinga gani huo! kila gumu lina mlango wake acha kulia papasa mlango! always nyakati ngumu hazdumu na nyakati njema sio daima! ukiona mlima ujue mbele kuna mteremko....pambanaaaa! usilegee tena ntakuchapa viboko💪💪💪
 
Ndiyo maana mimi huwa nasema "Kifo ni neema."

Maisha ni kama kubeba fuko la misumari kichwani, huna namna zaidi ya kuvumilia hivyohivyo ukiwa unaendelea kutembea.

Watu wanaotamani kuishi milele huwa nawashangaa, ukomo wa maisha unatia matumaini kwamba ipo siku hutasikia maumivu tena, hutasononeka tena.

Maisha hata uwe na kila kitu bado kuna siku tu utakosa furaha: utaumwa, utakosa pesa, ndugu/rafiki watakufa.

Huwa napenda quote ya Andrew Tate "A bad day is coming—for all of us. For all of us in our future, there's a 100% probability that either we're going to die or someone we love is going to die. So, a bad day is coming. You will have a reason to be upset soon enough. That's a fact. Why are you doing it in advance? Nothing's wrong today. Oh, you have flat tire. Boo hoo."

Binadamu tunakuwa upset kutokana na vitu vidogo ila tunasahau kuwa as long as bado tupo hai basi siku mbaya zaidi hazipo mbali.
Fact sana 🥹
 
Ndo ujinga gani huo! kila gumu lina mlango wake acha kulia papasa mlango! always nyakati ngumu hazdumu na nyakati njema sio daima! ukiona mlima ujue mbele kuna mteremko....pambanaaaa! usilegee tena ntakuchapa viboko💪💪💪
🫂❤️
 
Back
Top Bottom