Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 876
- 4,101
Nimeona wabunge na mawaziri wamemaliza kujadili ripoti ya CAG. Kwa namna mambo yalivyokwenda ni kama spika amesimama na mawaziri kufunika kombe. Lakini wakati huo wabunge wakiamua kuungana na mawaziri dakika ya mwisho kwa kupiga makofi kama walivyopigiana wakati wakichangia.
Cha msingi zaidi ni wale wote waliowataja mawaziri kuonekana kama waasi na watashughulikiwa kisiasa hasa wale waliosema nchi inakufa. Kwa ujumla yeyote aliyejitutumua kuungana na CAG amekatwa jina kuelekea 2025. Sawa ndio vizuri wakalime na kufuga
Mwisho, baada ya spika kufunika kombe CAG huko alipo na watendaji wake wapo mikoani wanatafuna posho kwa ajili ya kuandika ripoti mpya. Tusubiri tena waje na utepe wa vitabu vipya 2024 kukabidhi vielekee bungeni. Watu wale posho za vikao maisha yaendelee hadi pawepo na political will. Tumeambiwa leo na waziri wa fedha kazi anayofanya CAG ni hisani ya mtawala na kwamba nchi nyingine hakuna huu unaoitwa ripoti za ukaguzi. Twendeni twendeni twendeni