Spika Dkt. Tulia usijisahaulishe; Novemba ilee, tunasubiri mjadala wa wazi na huru Ripoti ya CAG

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,892
3,196
Asalam Aleykum wapenzi wana JF.

Ama baada ya salamu hizo, nitumie nafasi hii kumkumbusha Spika wa Bunge la JMT mh. Dk. Tulia Acson kuhusu ahadi yake aliyoitoa mnamo mwezi Aprili kuhusiana na mjadala wa Ripoti ya CAG iliyotolewa mwaka huu 2023.

Dk. Tulia Acson katika kuwanyamazisha badhi ya wabunge wazalendo ambao waliguswa kwa namna moja ama nyingine na Ripoti ile ya CAG, aliahidi kuwepo na mjadala kuihusu mnamo mwezi ujao kwa maana ya mwezi Novemba katika Mkutano wa Bunge.

Ripoti ya CAG, 2023, ni moja kati ya Ripoti mbaya kabisa kuwahi kutokea nchi hii tangu tupate uhuru! Hivyo, kama Mtanzania na mlipa kodi, nitabaki mdomo wazi endapo Mkutano wa Bunge wa Mwezi Novemba utaisha pasipo bunge kuwa na mjadala kuhusiana na Ripoti hiyo. Na, naomba Bunge lisiishie tu kuwa na mjadala huru na wa wazi, bali lihakikishe watumishi wote walioguswa na Ripoti ile wanawajibishwa kwa mujibu wa Sheria na Taratibu. Hii ni kwa sababu wameshindwa kufanyia kazi maelekezo ya Mh. Rais, Samia Suluhu Hassani, aliyewataka kujitathmini lakini hadi sasa hakuna hata mmoja ambaye amejiudhuru au kujiwajibisha kwa namna moja ama nyingine!

Nina imani, hii Ripoti ya CAG ya 2023, haitapita tu hivi hivi pasipo hatua zozote kuchukuliwa, kama kweli tuko serious kama Taifa katika kudhibiti uadilifu katika matumizi ya fedha na rasilimali za Umma. Vinginevyo, tutashauri hii Taasisi ya CAG, ifutwe kabisa kwa sababu hakutakuwa na maana yoyote ya kuwepo kwake.

Kazi kwako Dk. Tulia Acson.
 
Mwemweeeeee kwani I posho Jimalike bha Aikael po Kanunu bhajhobe tusyaghe isya kusijhobha.
Kwani tulimtuma aende kula posho tu?
😁😁😁😁😁😁
Sisi tulimtuma atuwakilishe kwa maslahi mapana ya Taifa
 
Tatizo wote ni kundi moja mkuu..
Panya kuwajibisha panya mwenzie siyo rahisi
Tuna mpango wa kununua "paka", atusaidie kuwakamata hao "panya" maana wamezidi sana ulafi na uharibifu kwa mali za Umma.
 
Yule hajielewi na wala hatambui madaraka yake,yeye anajiona na yeye ni mtumishi wa umma chini ya Samia!!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo hajioni kama Mkuu wa Mhimili ambao unajitegemea na ambao jukumu lake ni kuishauri na kuisimamia serikali?
Kama ni hivyo kweli, basi tumepigwa na kitu kizito walahi!
 
Asalam Aleykum wapenzi wana JF.

Ama baada ya salamu hizo, nitumie nafasi hii kumkumbusha Spika wa Bunge la JMT mh. Dk. Tulia Acson kuhusu ahadi yake aliyoitoa mnamo mwezi Aprili kuhusiana na mjadala wa Ripoti ya CAG iliyotolewa mwaka huu 2023.

Dk. Tulia Acson katika kuwanyamazisha badhi ya wabunge wazalendo ambao waliguswa kwa namna moja ama nyingine na Ripoti ile ya CAG, aliahidi kuwepo na mjadala kuihusu mnamo mwezi ujao kwa maana ya mwezi Novemba katika Mkutano wa Bunge.

Ripoti ya CAG, 2023, ni moja kati ya Ripoti mbaya kabisa kuwahi kutokea nchi hii tangu tupate uhuru! Hivyo, kama Mtanzania na mlipa kodi, nitabaki mdomo wazi endapo Mkutano wa Bunge wa Mwezi Novemba utaisha pasipo bunge kuwa na mjadala kuhusiana na Ripoti hiyo. Na, naomba Bunge lisiishie tu kuwa na mjadala huru na wa wazi, bali lihakikishe watumishi wote walioguswa na Ripoti ile wanawajibishwa kwa mujibu wa Sheria na Taratibu. Hii ni kwa sababu wameshindwa kufanyia kazi maelekezo ya Mh. Rais, Samia Suluhu Hassani, aliyewataka kujitathmini lakini hadi sasa hakuna hata mmoja ambaye amejiudhuru au kujiwajibisha kwa namna moja ama nyingine!

Nina imani, hii Ripoti ya CAG ya 2023, haitapita tu hivi hivi pasipo hatua zozote kuchukuliwa, kama kweli tuko serious kama Taifa katika kudhibiti uadilifu katika matumizi ya fedha na rasilimali za Umma. Vinginevyo, tutashauri hii Taasisi ya CAG, ifutwe kabisa kwa sababu hakutakuwa na maana yoyote ya kuwepo kwake.

Kazi kwako Dk. Tulia Acson.
November si ndiyo imeanza leo?

Ina siku 30. Kumbuka hilo.
 
Huyu Tulia aruhusu mjadala huru kuhusu CAG, Bandari HGA kwanza ili kuaminika.
 
Back
Top Bottom