Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,153
25,376
Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

Kimsingi, Wabunge wengi wameuona, wameusemea na kuukaripia ufisadi na ubadhirifu mkubwa ulioainishwa kwenye Ripoti ya CAG. Wabunge wamesikika hata wakishauri adhabu kali wapewe wahusika.

Bunge limehitimisha mjadala wa Ripoti husika. Nini kitafuata? Wahusika wa ufisadi na ubadhirifu huo mkubwa watafanywa nini na ni nani hasa mchukua hatua hizo?

Kiukweli, sisi walipa kodi wa nchi hii tungependa kuona hatua kali zinachukuliwa dhidi ya mafisadi na wabadhirifu waliotajwa au kuhusishwa na mambo hayo ndani ya Ripoti ya CAG.

Tunalipa kodi kwa maendeleo yetu. Kutumiwa isivyo kwa kodi na wale tuliowapa dhamana ya matumizi ya kimaendeleo ya kodi zetu kunaumiza sana. Tunatamani na kutaka hatua zichukuliwe. Wabunge wameona na kusema; wachukua hatua wafanye hivyo.
 
Ngoja tuone,kama kuna usikivu upande wa Serikali,kwasababu sauti ya bunge ni sauti ya wananchi,kudharau maoni ya bunge ni kutudharau sisi wananchi
Hilo bunge haliko kwa ajili ya wananchi....
Hilo bunge watu washazoea kuwaona wanapiga kelele tu,hakuna hatua yoyote wakatayo chukua
Kumbuka pia uchaguZi unakaribia lazima wawastue wananchi

Ova
 
Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG).
Chini ya serikali sikivu na imara ya Dr.SSH.ni imani ya waTanzania walio wengi kwamba,
hakuna muhuusika hata moja alie tajwa kwenye report ya CAG na kulalamikiwa na waheshimiwa wabunge atasalimika na mkono wa Sheria, wote watawajibika na kuwajibishwa kulingana na makosa yao...
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom