Nani aliyemshauri Rais Magufuli amjibu Lowassa?

Nani aliyemshauri Rais Magufuli amjibu Lowassa?

Ni kweli mkuu, utafikiri ni binti wa uswazi, kila kitu lazima ajibu, hata kama si lazima.
 
Lowassa angekuwa kipindi cha nyerere angekuwa ndani saa hizi, kuna statement kwa level ya lowasa hakutakiwa kuongea yale

wanaokufa ni ccm tu??

lowassa hana sapoti yeyote, unless unasema hao wauaji ndio wako nyuma ya lowassa??!!!

nyuma ya lowassa?? unamtisha nani??
Hujaeleweka, nani aliyetoa statement inayolingana na level yake?
 
Unawaambiaje wenzako waache kuropoka wakati wewe kila maji kujaa unaropoka,maji kupwa unaropoka? Wiki iliyopita ulituambia wauwaji kibiti hawpo tena. PM majaliwa akasema waisilamu wasihusishwe na mauaji hayo. Leo unatuambia mashehe na Lowasa wanahusika. Sijapata kuona rais wa aina hii duniani note!
 
Get Real bro!

Lowassa is not a threat in this country. Yes. He once was. But not now or in the future. Him or his supporters, the earlier they realize that the better.

I am sure JPM hakupenda kauli yake ya juzi kuhusu Uamsho. Hata kama naheshimu haki ya EL kutoa mawazo. wale jamaa wa Uamasho wako gerezani kwa order ya Mahakama. Awaachie Mahakama waamue. Kauli kwamba yeye angewaachia mara moja kama angeingia madarakani..maana yake ni kwamba Mahakama haijui kazi yake-au angeitumia Mahakama kufanya analolitaka. It is a long debate on the independence of our judiciary and thats not my concern here.

Lakini I guess hata EL angetakiwa kuwa careful na kauli yake especially kwa kesi iliyoko Mahakamani.

Mzee EL akapumzike Ngarashi anywe maziwa na whisky. Huku akisoma magazeti ya Economist na kuangalia News CNN.

The man is past his sell by dates on the shelf! Amekula vya kutosha! Awe na shukrani kwa waTanzania.

Masanja.
Mahakama za jiccm, mahakama haziko huru Tanzania na kama zingekuwa huru hao viongozi wa Uwamsho wangekuwa huru vile vile kwa utashi wa kisiasa.

Jaji mkuu kateuliwa na rais vipi tutakuwa na mahakama huru? Rais jaji mkuu lazima atekeleze amri ya Boss.
 
Rais Magufuli ndiye alishinda uchaguzi, hilo la kwanza - la pili yeye kama Kiongozi anapewa briefing kila siku kuhusu kinacho endelea Nchini wewe mtu baki uwezi kuja hapa na kutaka kumpangia aseme nini ahache nini, nakukumbusha asemi kitu kwa kubuni anajua alisemalo. Lowassa alishindwa uchaguzi kwa nini baadhi yenu hamtaki kukubali ukweli huo, yaani mnaonekana hamjaziduka kutoka kwenye kimbunga cha shockwave ya kushindwa uchaguzi.

FYI kipenzi chenu kukimbilia kwake Chadema it was a Political hara-kiri/kamikaze ya kujimaliza mwenyewe kisiasa wala nyinyi hilo hamlioni, mpo mpo tu kazi kumunanga JPJM siku nenda rudi hata hamuoni aibu.

Nawakumbusheni tena kwamba Watanzania wanao jitambua hawawezi kuchagua a flipflopper person ambaye anaonekana wazi wazi anajali zaidi kuupata Urais come rain or shine kuliko kuipeleka nchi mbele kimaendeleo. Come 2020 I am sure Urais atakuwa anausikia kwenye radio na luninga tu.
Naomba nipingane na wewe kwenye sentensi ya kwanza kabisa hapo!!
 
Utafiti umefanyika kuonyesha kuwa mauaji yametokana na usumbufu unaofanywa na watumishi wa idara ya polisi, maliasili na Serikali za vijiji na mitaa huku wewe unakuja kuropoka humu JF kuwa wanaouwawa ni wanachama wa ccm!

Msitake ku-derail operation na upelelezi unaoa endelea huko Kanda ya Pwani, mnajitahidi kutumbukiza madai ambayo hayana kichwa wala miguu kama mbinu za kuwasaidia waarifu/magaidi katika propaganda zao za kutafuta public sympathy sioni kama hilo mnalitambua.

Hivi kwa akili za kawaida mnataka kusema Idara ya Polisi, Maliasili, Serikali za vijiji na mitaa vipo Kanda ya Pwani tu Mikoa mingine ina RCs tu ndiyo maana amani inatawala katika Mikoa hiyo!! - What a lame excuse?
 
Raisi kasema amechomekea ujumbe huo kwa mtu japo hakufafanua.
Ametoa onyo kwa mtu au watu wanaotumia siasa za kuunga mkono mauwaji yanayoendelea Kibiti.
Kwa usalama wa hao wanasiasa waachane kabisa au wataisaidia police,alimaalizia.


Na wewe ukaamini kabisa kuna wanasiasa wanaunga mkono mauaji? Seriously?
 
Inabidi mzee mmoja akubali lawama amkumbushe jamaa kua kampeni zimeisha sasa ivi yeye ni Rais maana naona jamaa kila siku anatafuta jukwaa la kupiga vijembe na kuimba taarabu.
Na nyie mwambieni mzee wenu mamvi kampeni zimeishaa. Uongo usipojibiwa hubaki ukweli. Kauli anazotoa mzee wenu za kuweweseka kwamba alishinda uchaguzi akafanyuiwa figisu zinadhihirisha kwamba bado yupo kwenye campaign mode kwa hiyo atajibiwa accordingly.
 
Hatutaki kuona nchi yetu ikiingia katika vita isyoisha
Magufuli amekosea sana jana kuwahusisha mashehe walio ndani na mauaji yanayoendelea huko kibiti na kwingine

Hii vita yake na lowasa haitaiacha nchi yetu salama
Mtu mkimya lakini yuko na watu nyuma yake wanaomsapoti

Kwenye red: Jitahidi siku nyingine usiandike jambo usilolifahamu kwa undani wake. Nani amekuwambia mashehe walio ndani hawana uhusiano na mauaji yanayoendelea? Furahia amani uliyonayo nyumbani kwake lakini kaa ukijua Rais anafanya kazi ambayo huna taarifa nazo ili uendelee kuishi kwa amani na kuandika hapa JF. Panua mawazo yako na fikiri kwa utashi zaidi. Rais hakukurupuka kusema aliyosema jana, na kinachoshangaza na pengine kusumbua akili ni wanasiasa kutetea upande unaoleta shida. Na wewe unaweza kuchagua upande.
 
Mbns wewe unavutia sana kwenye udini? Sidhani kuna sehemu ametaja dini ktka maelezo yke, hapo unataka kuleta udini wewe, wale walioko ndani wanachukuliwa kma wahalifu, hvyo usiingize dini nzma ya kiislamu huko, cha kujadili hapa ni kuwa haki itendeke kma hawana makosa waachiwe huru, hiyo miaka kukaa ndani bila kuhukumiwa si sawa.

Mkuu kwani hawajui kwamba walio wekwa ndani ni kwa sababu ya uhalifu tu wa kuua Mapadri na Polisi huo ulikuwa utashi wao wenyewe, Dini ya Kislaam hahusiki chochote na wala awahubiri binadamu kuuana - wenye akili fyatu ndiyo ulazimsha mambo yao ya kisiasa kwa kutaka kupitia mgongo wa dini - hawa jamaa ni hatari sana, wanataka ku-incite wahumini ili wafanye mambo ya ndiyo sivyo kumbe lengo lao ni la kisiasa zaidi.
 
MCHAWI MPE MTOTO AKULELEE.
UKITOA TAARIFA POLISI AU UKISHATANGAZA KUWA FULANI ANAPANGA KUKUUA NA UKAONYESHA USHAHIDI HATA KAMA NI WA KIMAZINGIRA BASI HUYO FULANI BAADA YA HAPO ATAACHA MIPANGO YAKE YA KUKUUA NA NDIYE ATAKUWA MLINZI WAKO.
UKICHOSHWA NA TABIA ZA MTU MZOMEE HADHARANI.
SHERIA HAIRUHUSU MTU KUWATETEA WATUHUMIWA WA UGAIDI WAKATI KESI YAO BADO INAENDELEA.
KUNA VIONGOZI AMBAO LEO WAKIPEWA HATA UWAZIRI MKUU TU MAFISADI WOTE WATATOLEWA MAGEREZANI.
RAIS MAKUFULI ANAUELEWA MKUBWA WA MAMBO YA INCHI KULIKO SISI.
TANZANIA YETU ITAKUWA NZURI SANA KIUCHUMI NA KIUSALAMA JINSI MUDA UNAVYOENDA.
Mwambie aache chuki zake na uislam
 
Mkuu kwani hawajui kwamba walio wekwa ndani ni kwa sababu ya uhalifu tu wa kuua Mapadri na Polisi huo ulikuwa utashi wao wenyewe, Dini ya Kislaam hahusiki chochote na wala awahubiri binadamu kuuana - wenye akili fyatu ndiyo ulazimsha mambo yao ya kisiasa kwa kutaka kupitia mgongo wa dini - hawa jamaa ni hatari sana, wanataka ku-incite wahumini ili wafanye mambo ya ndiyo sivyo kumbe lengo lao ni la kisiasa zaidi.
Kweli kabisa mkuu, hili ni swala la usalama, wengine sasa wameshaanza kusema kwa kuws ni waislam...kma ni swala la dini kwan Magufuli ndo aliwaweka ndani?
 
One would think common sense is common, but very unfortunately it isn't! Huyu jamaa yetu angekuwa anajua kutumia twitter, yule wa Marekani hangeona ndani.
Ha...ha..haaa kweli mkuu
Lakini maropoko yake yasipodhibitiwa yataleta matatizo mengi kuliko anavyodhani.Miropoko ya namna hii ndiyo inayowakaribisha wapiganaji wa kimataifa
30% ya wapuganaji wa IS Syria na Iraq wanatoka nchi mbalimbali nje
Mdomo huponza kichwa
 
Eeeeeeeh

Na bado

Hapa kazi tu

Hakuna kuwea vipole, acha wananchi tuyajue eeeeh


Magufuli oyeeeeee
 
BAKWATA wapongeza kauli ya MH.Rais, ,wasema kweli alichosema Rais kina mantiki kuwa mashehe waliopo gerezani wanahusika na kibiti,,, wanasema acha wakae kama wanavyokaa wale wa GUANTANAMO BAY kwa kauli ya mh Rais ,,,,
Bakwata ni jumuiya ya CCM kama ilivyo UVCCM hivyo haitutishi.
 
Wakati mwingine ni vizuri mkuu wa nchi akawa mwenye busara siyo kila kitu akisikiacho anatakiwa kujibu
Amekosea sana rais wetu kumjibu mtu kama lowasa
Labda tujiulize wale mashehe kutoka zanzibar waliofungwa bila kuhukumiwa ni magaidi? Na kwa nini raisi awahusishe na mauaji yanayotokea kibiti
Je haoni hii ni kuendelea kuwaamsha wauwaji hao wa kibiti na kwingineko kuendelea kuua

Wakati mwingine rais wetu magufuli anawapa kiburi wauaji na sababu ya kuendelea kuua

Hatutaki kuona nchi yetu ikiingia katika vita isyoisha
Magufuli amekosea sana jana kuwahusisha mashehe walio ndani na mauaji yanayoendelea huko kibiti na kwingine

Hii vita yake na lowasa haitaiacha nchi yetu salama
Mtu mkimya lakini yuko na watu nyuma yake wanaomsapoti

Bado najiuliza nani aliemshauri kumjibu lowasa au ni yeye kama yeye

Mashehe walio gerezani bila kuhukumiwa amewahusishaje na mauwaji yanayoendelea huko kibiti na kwingineko

Tujifunze kuchagua nini cha kujibu
Siku zoote hizo alikuwa hafahamu kuhusu kuwekwa ndani hao anowatetea, juzi alipotamka ndo alifahamu au..kwa nini aseme wakati huu??? halafu yeye akisema sawa mnaziba midomo yenu, akisema Rais mnafunua mabakuli yenu..kwa hiyo hata ukisemwa uongo na Lowasa Rais anyamaze tu ndio hivyo..hata mtoto wa darasa la saba hahitaji kufundishwa kwamba Rais anapata taarifa za kina juu ya matukio yote yanayotokea nchini kwake kuliko wewe unayetegemea media! bara kukaa kimya kuliko kuleta ujinga huu ulioandika..
 
Mbns wewe unavutia sana kwenye udini? Sidhani kuna sehemu ametaja dini ktka maelezo yke, hapo unataka kuleta udini wewe, wale walioko ndani wanachukuliwa kma wahalifu, hvyo usiingize dini nzma ya kiislamu huko, cha kujadili hapa ni kuwa haki itendeke kma hawana makosa waachiwe huru, hiyo miaka kukaa ndani bila kuhukumiwa si sawa.
Hivi ukisema wale masheikh hapo hujataja udini???Au ukisema viongoz wa waislamu hujataja dini??Kingine kataja na uchama au hilo nalo hajalisema??Bado unasafari ndefu sana kumuelewa huyo mtu narudia tena alochokiongea kama ni kiongoz wa nchi sio sahihi
 
Hivi ukisema wale masheikh hapo hujataja udini???Au ukisema viongoz wa waislamu hujataja dini??Kingine kataja na uchama au hilo nalo hajalisema??Bado unasafari ndefu sana kumuelewa huyo mtu narudia tena alochokiongea kama ni kiongoz wa nchi sio sahihi
Wewe ndo una safari ndefu ya kuendekeza udini hadi sasa, waliwekwa ndani na kikwetu kwa mambo ya kichochezi, leo unamtolea povu magufuli, hlf wewe na mimi hatuna intelijensia yyte zaidi ya rais anayejua kinachoendelea, bora tupige kimya.
 
Back
Top Bottom