Nani aliyemshauri Rais Magufuli amjibu Lowassa?

Nani aliyemshauri Rais Magufuli amjibu Lowassa?

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,401
Wakati mwingine ni vizuri mkuu wa nchi akawa mwenye busara siyo kila kitu akisikiacho anatakiwa kujibu
Amekosea sana rais wetu kumjibu mtu kama Lowassa
Labda tujiulize wale mashehe kutoka zanzibar waliofungwa bila kuhukumiwa ni magaidi? Na kwanini Rais awahusishe na mauaji yanayotokea Kibiti.

Je haoni hii ni kuendelea kuwaamsha wauwaji hao wa kibiti na kwingineko kuendelea kuua

Wakati mwingine rais wetu magufuli anawapa kiburi wauaji na sababu ya kuendelea kuua

Hatutaki kuona nchi yetu ikiingia katika vita isyoisha
Magufuli amekosea sana jana kuwahusisha mashehe walio ndani na mauaji yanayoendelea huko kibiti na kwingine

Hii vita yake na lowasa haitaiacha nchi yetu salama
Mtu mkimya lakini yuko na watu nyuma yake wanaomsapoti

Bado najiuliza nani aliemshauri kumjibu lowasa au ni yeye kama yeye

Mashehe walio gerezani bila kuhukumiwa amewahusishaje na mauwaji yanayoendelea huko kibiti na kwingineko

Tujifunze kuchagua nini cha kujibu
 
Hapo hata mimi Rais wangu mpendwa sijamuelewa.
Kuhusisha wale jamaa wa Zanzibar na kinachoendelea Kibiti ni makosa makubwa au hakupaswa kuyasema hadharani.

Hii maana yake Rais anatangaza kua kinachofanyika Kibiti ni ugaidi, maana yake ni kua sasa magaidi wote wataanza kumiminika Kibiti maana serikali ishasema kuna ugaidi.

Haikua sawa kabisa kusema yale hadharani kwa mtazamo wangu.
 
Wakati mwingine ni vizuri mkuu wa nchi akawa mwenye busara siyo kila kitu akisikiacho anatakiwa kujibu
Amekosea sana rais wetu kumjibu mtu kama lowasa
Labda tujiulize wale mashehe kutoka zanzibar waliofungwa bila kuhukumiwa ni magaidi? Na kwa nini raisi awahusishe na mauaji yanayotokea kibiti
Je haoni hii ni kuendelea kuwaamsha wauwaji hao wa kibiti na kwingineko kuendelea kuua

Wakati mwingine rais wetu magufuli anawapa kiburi wauaji na sababu ya kuendelea kuua

Hatutaki kuona nchi yetu ikiingia katika vita isyoisha
Magufuli amekosea sana jana kuwahusisha mashehe walio ndani na mauaji yanayoendelea huko kibiti na kwingine

Hii vita yake na lowasa haitaiacha nchi yetu salama
Mtu mkimya lakini yuko na watu nyuma yake wanaomsapoti

Bado najiuliza nani aliemshauri kumjibu lowasa au ni yeye kama yeye

Mashehe walio gerezani bila kuhukumiwa amewahusishaje na mauwaji yanayoendelea huko kibiti na kwingineko

Tujifunze kuchagua nini cha kujibu
Hivi kwa nini kila anachofanya rais watu mnakimbilia kuwalaumu washauri? Una maana rais yeye ni mtu ambaye hana utashi wake na kila anachoshauriwa anakimeza tu bila kuongeza na za kwake? Ukweli ni kwamba washauri wanamsaidia tu kuboresha maamuzi au hotuba yake lakini kila anachofanya ni uamuzi wake binafsi na sifa au lawama ni za kwake.
 
Lowassa angekuwa kipindi cha nyerere angekuwa ndani saa hizi, kuna statement kwa level ya lowasa hakutakiwa kuongea yale

wanaokufa ni ccm tu??

lowassa hana sapoti yeyote, unless unasema hao wauaji ndio wako nyuma ya lowassa??!!!

nyuma ya lowassa?? unamtisha nani??
 
Uwe unawaza nje ya box itakusaidia kuelewa kwa rais ni binadamu anaweza kukosea na yeye kama kiongozi anatakiwa kuonyesha kuwa ni kiongozi mwenye busara na busara huonekana zaidi unapokuwa umechukizwa

Amekosea sana afaham kuwa nchi hii si familia yake
 
Kitu ambacho Huwa sikubaliani na raisi wangu kipenzi Ni kujibu Kila kitu anachosikia anapaswa ajue vitu vingine hushughulikiwa kimya kimya
Na hili linafanya rais atofautiane sana na watendaji wake katika matamko, mfano Ni juzi tu pm majaliwa amesema waislamu hawausiki na mauaji ya kibiti wiki haijaisha rais anatwambia uamsho na kibiti ni kitu kimoja hatuelewi kwa kweli
 
Hivi kwa nini kila anachofanya rais watu mnakimbilia kuwalaumu washauri? Una maana rais yeye ni mtu ambaye hana utashi wake na kila anachoshauriwa anakimeza tu bila kuongeza na za kwake? Ukweli ni kwamba washauri wanamsaidia tu kuboresha maamuzi au hotuba yake lakini kila anachofanya ni uamuzi wake binafsi na sifa au lawama ni za kwake.
Urais ni taasisi, rais ni kinara. Kama ipo institution kubwa hapa duniani, basi ni Catholic Church na Pope ndio kiongozi wake. Pamoja na ukiongozi wake huo, maamuzi makubwa yenye kuathiri mustakabali wa maisha wa Wakatoliki hupitia hatua mbali mbali na MTAGUSO hufanywa na baraza la Makadinali baada ya maombi na kufunga kwa muda mrefu. Nchi huongozwa na katiba na sio utashi wa mtu. Ndio maana Trump anabananishwa kila leo asiigeuze America kuwa WWE Afterburn
 
Lowassa angekuwa kipindi cha nyerere angekuwa ndani saa hizi, kuna statement kwa level ya lowasa hakutakiwa kuongea yale

wanaokufa ni ccm tu??

lowassa hana sapoti yeyote, unless unasema hao wauaji ndio wako nyuma ya lowassa??!!!

nyuma ya lowassa?? unamtisha nani??

Mkuu;
Mbona mapema sana? Au ulikesha nalo? Hii inaonesha wazi kuwa unatakiwa kwenda kutoa lock. Unataka kutuaminisha kuwa huyo Nyerere alikuwa dicteta sana au? Angalia, ati wanaokufa ni ccm tu. Yaani unataka kutuaminisha kuwa wale Polisi walikuwa ccm?? Yaani jeshi la polisi ni ccm? Weye ndiye ulitakiwa uwe lock up saa hii. Lakini bado unajinafasi huku uraiani tu hadi JF.
Kuambiwa wapo watu nyuma ya Lowasa maana yake ni kwamba, hiyo level uliyoisema amefikia huyo Lowasa hakufika hapo kwa miguu yake mwenyewe bali ana watu wengi tu waliomwinua na kumfikisha hapo.
Mada ni Je, mh rais alistahili amjibu Lowasa?? Usimwinue Lowasa kihivyo. Rais alitakiwa amtume waziri kama Ummy Mwalim amjibu Lowasa wakati huyo waziri alipokuwa anatoa ufafanuzi wa majibu ya yule mama aliyepotelewa na mtoto.
Rais anapowajibu watu ka hao, anawakuza saana.
 
Lowassa angekuwa kipindi cha nyerere angekuwa ndani saa hizi, kuna statement kwa level ya lowasa hakutakiwa kuongea yale

wanaokufa ni ccm tu??

lowassa hana sapoti yeyote, unless unasema hao wauaji ndio wako nyuma ya lowassa??!!!

nyuma ya lowassa?? unamtisha nani??
Utafiti umefanyika kuonyesha kuwa mauaji yametokana na usumbufu unaofanywa na watumishi wa idara ya polisi, maliasili na Serikali za vijiji na mitaa huku wewe unakuja kuropoka humu JF kuwa wanaouwawa ni wanachama wa ccm!
 
Raisi kasema amechomekea ujumbe huo kwa mtu japo hakufafanua.
Ametoa onyo kwa mtu au watu wanaotumia siasa za kuunga mkono mauwaji yanayoendelea Kibiti.
Kwa usalama wa hao wanasiasa waachane kabisa au wataisaidia police,alimaalizia.
 
Back
Top Bottom