Sawa, nakubaliana na wewe maboda wengi wanapiga hela, hasa maeneo ya town na masoko makubwa. Hilo halina ubishi.
Lakini hoja yangu haikuwa kama wanaingiza au hawaingizi.
Hoja yangu ni hii
Je hiyo hela ni endelevu?
Akiumwa wiki moja tu, kipato kinakata
Ajali ikitokea, maisha yanabadilika ghafla
Pikipiki ikiharibika, income inasimama
Hakuna mfumo wa akiba au uwekezaji kwa wengi
Na ukweli mwingine, hata kama wanapata 40k–60k kwa siku, wengi wanatumia bila plan ndio maana wengine wanakaa miaka lakini bado hawana stability.
Kwa hiyo point sio “wana hela au hawana”.
Point ni wana mfumo wa hiyo hela kuwasaidia kesho?