Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

BM X6

JF-Expert Member
Nov 24, 2020
1,360
4,149
EPISODE 01, SEASON 01

Wakuu nahitaji ushauri wenu ili niweze kufaulu katika huu mtihani, nimepewa kazi kubwa ambayo nikifaulu basi milango mingi itafunguka huko mbeleni.

Kuna Mzee flani huwa tunashirikiana kikazi na mara nyingi mizigo yake huwa anaiagiza kupitia Kampuni yetu, ni Mfanyabiashara na ameanza Biashara miaka ya 90s alivyomaliza tu O level, Sasa huyu Mzee kijana (1971) huwa tunaongeaga mambo mengi kuhusu Biashara huku nikitaka anipe miongozo ili na mimi nielekeze nguvu na akili huko

Huyu Mzee akijaga Ofisini ni lazima nionane nae japokuwa muda mwingi Mimi huwa nakuwa nje ya ofisi kutokana na majukumu yangu mengi si ya kufanyia Ofisini nimesema ni lazima nionane nae ni kwasababu zangu Binafsi na si za kiofisi, Huyu Mzee ndio ameni inspire mm kutaka kufanya Biashara si kimafanikio tu bali hata lifestyle yake, Yani kifupi ana enjoy mafanikio yake anafanya kazi huku amerelax nyakati za kujituma usiku na mchana kwake zilishapita, sio kama wazee wengine wenye Utajiri lakini Bado anajitesa siku nzima kama yeye ndio kaajiriwa jambo ambalo ni tofauti kwa huyu mzee, huwezi kujua ratiba yake muda wowote yupo Ofisini na muda wowote pia anaweza akawa nyumbani, Ni siku ya Ijumaa tu ndio Najua kwamba haendagi ofisini kwake labda kuwe na jambo muhimu sana ambalo linahitaji uwepo wake.

Sio mtu wa mitandao sana hasa kama hii Jf pengine hata haijui, Kuna siku nilimuuliza kuhusu mitandao akanambia anatumia Twitter na Whatsapp tu, so hii story Najua itakua ngumu kwake kuiona, maana hata kwa codes nitakazoweka kama akiiona atajua tu ni Mimi na ndio mchongo mzima utaishia hapo

Sasa nikibahatikaga kukaa na huyu Mzee mtu mbili huwa namuonesha shauku ya mimi kutaka kufanya biashara lakini kila nikimgusia swala hilo ni kama anaona sipo serious, anahisi nataka kufanya biashara kwa kufuata mkumbo tu, Kwasababu nakumbuka aliniuliza nataka kufanya Biashara gani mimi nikamwambia nataka kufanya Biashara kama ya kwake, aliishia kucheka tu

Nakumbuka siku moja nimetoka Zanzibar kupokea mizigo ya ofisi ya wateja, nimefika Dar Huyu Mzee akanipigia simu kuniomba kwamba mzigo wake nisiupeleke store Bali niende nao Ofisini kwetu ili nikitoka kazi nimpitishie kwake, na ndio ilikuwa mara ya kwanza kufika kwa huyu Mzee, Asee vile nilivyokuwa namdhania ni robo yake, Kuna watu wanaishi acheni nyie

Basi Mzee alinikaribisha vizuri sana mjengoni mjengo mjengo kweli! Wakati naingia kwenye Parking sijaona Gari yake niliozoea kumuona nayo siku zote (Land Cruiser ZX V8) nilimkabidhi vitu vyake Mzee akapanda juu Nadhani ni Bedroom kwake alivyorudi akanipeleka Backyard tukakaa, Sasa tulivyokuwa mule ndani sikuona mtu mwingine yeyote ikabidi nimuulize Mzee nyumba yote hii unaishi peke yako? akanambia "hapana mabinti zangu na Mama yao wameenda Kibaha watarudi Jumapili" (Siku hiyo ilikuwa Ijumaa)

Story zikaendelea pale Mzee akanambia "Kijana wangu nilikuambia uniletee mzigo kwa makusudi, mm kila Ijumaa huwa na utaratibu wa kupata chakula Cha jioni na familia yangu ya ndani na ya nje hivyo nilitaka na wewe uwepo" alivyosema familia ya nje niliwaza mbali, nikamuuliza kwani Mzee wewe una wake wa ngapi? kabla hajajibu alitabasamu "mmoja tu na Najua umeuliza hivyo kwasababu gani, nilivyosema familia ya nje nilimaanisha watoto wa mitaani ambao hawana makazi maalum, kwahiyo badae tutatoka kwenda kuwachukua" nikasema sawa ni jambo zuri Mzee

Wakati tumekaa na kuendelea na story Mzee akanambia kama nitataka kunywa chochote niende kwenye fridge nijihudumie, Nikamwambia haina shida, Mara ghafla Mzee akapokea simu Wakati anazidi kuongea akachange ni kama kapokea Taarifa mbaya, yule Mzee aliinuka pale alipokuwa amekaa akiwa bado anaongea na simu huku akiingia ndani, alivyotoka alikuwa kashika funguo mkononi akanambia "Kijana wangu nimepata dharula itabidi nikuache kidogo ila nitajitahidi niwahi kurudi ili tufanye lile jambo nililokuambia, in case of anything utanipigia simu" Nikamwambia sawa Mzee

Tukatoka kule backyard hadi Parking pale kulikuwa na Magari mawili ambayo sikuwahi kumuona nayo akaingia kwenye Jeep, Yale majeep yenye muundo kama wa Benz G Wagon, Mzee alifungua geti na Remote control akasepa, Mtu mzima nikachoma ndani, nikajiachia kwenye Sofa huku nikiperuzi, Giza likaanza kuingia na saa Ile Mzee anaondoka ilikuwa ni around saa kumi jioni.

Simu ikaita, kucheki ni Mzee, akanambia "Kijana wangu ni kama nitachelewa kurudi Sasa wewe Fanya hivi, umeiona hiyo gari hapo parking?" nikamjibu ndio "Sasa panda juu mkono wa kulia chumba Cha mwisho fungua mlango ingia ndani nenda hadi kwenye dressing table utakuta funguo ya Gari ichukue, si unajua kuendesha gari?" nikamwambia ndio lakini Sina leseni Mzee "Wachana na mambo ya leseni, kwani Driving licence ndio inaendesha gari? Sasa si umesema unajua ku drive, nenda jikoni kachukue hicho chakula pakia kwenye gari wapelekee wenye uhitaji sababu ninaweza nisirudi halafu hicho chakula kikaharibika" nikamjibu sawa Mzee akakata simu

Nikawa najiuliza pa kwenda kuwapata hao watoto, Basi bhana Mimi nikapanda juu kuchukua funguo ya Gari, nikazama hadi chumbani asee ni noma, Chumba kama sebule nikawa sielewi dressing table Iko wapi, kilichonisaidia ni kioo, nilivyoona kioo nikajua tu hii ndio yenyewe hadi kesho sijaelewa Ile dressing table imetengenezwaje, kweli nikakuta funguo pale juu Ile kupiga jicho pembeni nikakuta maburungutu ya pesa elfu tano tano, hata sijayagusa maana nilijua nyumba kama Ile haiwezi kukosa CCTV camera, me nikabeba funguo kikashuka chini hadi jikoni nikakuta mahotpot yana msosi wa kutosha (Wali njegere maini) nikayabeba hadi kwenye Gari (Alphard) nikarudi jikoni kucheck sahani zote za dongo nikaachana nazo nikarudi kwenye Gari nikafungua Geti nikasepa ila sasa nimetoka na sijui naelekea wapi nikicheki saa ni saa moja kasoro, nikaenda hadi Mwenge, nikapark kando ya Barabara nikawa nawaza hao watoto nitawapata wapi, mawazo yakaja niende kwa sister angu flani anakaa uswahilini huko ndiko nikagawe hiki chakula, nikapiga mahesabu ya masaa nitakayo tumia hadi kufika huko muda utakuwa umeenda hata hivyo nitakuta watoto wengi wapo majumbani mwao na watakuwa washakula nikaona nikifosi kufanya hivyo nitaendelea kuipa nguvu ile kauli ya "mwenye nacho huongezewa"

Nikatoka pale Mwenge nikaenda Buguruni, nimepitia Ile footbridge na Mataa nikaingia Barabara ya kama naelekea Ilala, sijafika hata mbali nikapark pembeni kusikilizia, sijakaa sana nikaona madogo wawili nikawasimamisha Nikawauliza wanapoishi hawakunijibu, nilivyoona hivyo sikutaka story nyingi tena niwaambia ninachakula nataka niwapatie lakini nyie wawili hamtakimaliza mnaweza kuwaita na wenzenu? mmoja akaniuliza "kiko wapi hiko chakula chenyewe?" nyie kawaiteni wenzenu mkija mtakiona chakula, nitawaambia hivyo wakaondoka nikakaa kama Dakika 8 nikaona wale madogo wanakuja na rundo la madogo wenzao nikajisemea Leo kazi ipo maana kwa Ile idadi niliyoiona ya wale watoto na nikipiga mahesabu ya kile chakula nilichobeba ni kama hakitatosha kabisa halafu saa hiyo hiyo nikakumbuka nilibeba tu chakula na sikubeba sahani nilipanga nipitie supermarket ninunue zile sahani za karatasi nikasahau

Madogo wakafika hadi kwenye gari, nikawauliza mgahawa wa karibu uko wapi?wakanionesha lengo nikwenda kununua chakula ili niongezee na hapo hapo nitapata sahani za kutumia kwasababu kwa kile chakula kilichopo kinatoshea kwa watu kama 9 ivi na kile kikosi Cha madogo 15 wamefika, nikalock gari nikawaacha madogo pale kwenye gari nikavuka Barabara hadi upande wa pili nikaulizia chakula nikaambiwa kipo, saa hyo ni saa 2 usiku na madakika yake, Nikwambia Mama ntilie nataka chakula Cha watu kama kumi, Yani sahani kumi za wali, akanipakulia akaniwekea kwenye ndoo, nikatumia ujanja wa kumwambia kila sahani ifunike ili chakula kisipoe ili nipate sahani excess, alivyomaliza nikampatia 20k Nikamwambia siendi mbali sana sahani nitakuletea mwenyewe, akakubali bila wasi na sijui kwanini aliniamini kiwepesi vile

Nikafika kwa madogo nikafungua gari nikatoa Yale mahotpot ujinga mwingine ambao niliufanya sikubeba vijiko vya kupakulia na kule kwa Mama ntilie sikuchukua Maji ya kunawa, Sasa ule msosi wa Kwenye hotspots nikaupakua kwa kutumia sahani nikakigawa kile chakula wengine ilibidi wale wali wa mama ntilie na baadhi yao wakala ule niliokuja nao ila ngegere na maini nilizigawanya katika Kila sahani, sasa nikawa nawauliza madogo mtanawa wapi mikono?, dogo mmoja akasema blaza haina haja mikono yetu misafi basi nikawaruhusu wafinye msosi na mm nikichukia sahani moja, walivyomaliza Nikaingiza mahotpot kwenye gari nikalock nikamchukua dogo mmoja Nikamwambia abebe ndoo yenye sahani anifuate wale wengine niliwaambia watusubiri, tukaenda hadi kwa mama ntilie nikampatia sahani zake akanirudishia balance yangu elfu 5, nikamuomba chenchi ya elfu 10 buku buku, akanipatia, tukarudi hadi kwenye gari na yule dogo, Nikawaambia Sasa Mimi na nyie tushamaliza nikampatia Kila mmoja buku buku angalau kesho Asubuhi wawe na uhakika nikaagana nao pale nikasepa, Wakati nipo Njiani nikampigia Mzee kumjulisha kwamba nishafanya kile alichoniagiza akanambia "sawa Sasa wewe unaweza kwenda na hilo gari kesho utalileta nyumbani, si ulifunga vizuri nyumba?" aliniuliza Nikamwambia ndio na funguo Niko nazo, "Haina shida ww unaweza kwenda kupumzika Sasa" okay Mzee, Sasa wakati huo naongea nae kwenye simu Mimi nilikuwa nishapita Ubungo Interchange naitafuta Mwenge, nikielenda nyumbani kwake, ilibidi nigeuze gari nilirudi nilikotoka sababu mm naishi Tabata, Yani kama ningewahi kumpigia simu basi nisingejisumbua kufika mbali kote huko

Kwa mara ya kwanza nafika mtaani kwangu na Gari, siku zote Mimi niwakufungua kale kageti kadogo Leo nafungua Geti lote kubwa ili kuingiza ndinga, maana nilipopanga tunakaa watu 3 nyumba zinajitegemea ila tunashea Compaund, nikapark gari nikaingia ndani kulala, kukakucha, Jumamosi mara nyingi huwa siendagi ofisini labda itokee naenda Zanzibar, so nikawa Sina ratiba ndefu nikafua nguo kadhaa nikaingia mtaani kupiga chai, nilivyomaliza nikarudi home direct nikakuta missed call ya Mzee maana nilivyotoka simu niliiacha, nikampigia akanipa maelekezo fulani pale ya kwamba atarudi Jumapili Pamoja na familia yake hivyo kama Nina muda nilipeleke Gari kule nyumbani au nibaki nalo hadi Jumatatu aje alichukulie Ofisini, nikamjibu sawa yote yanawezekana ila acha niangalie lipi litakuwa rahisi zaidi

Baada ya kukata simu nikapiga hesabu kurudisha hili Gari hadi kule mwisho wa mji, nikaona uvivu isitoshe gari lenyewe lilikuwa rafu mavombo machafu humo ndani, Yani ukifungua mlango wa gari Gari lote linanuka wali, nikatoa vyombo vyote, nikajikaza kuviosha hakuna Kitu kinanikera kama kuosha vyombo ndio maana huwa sipikagi mara kwa mara. nilivyomalizana na hiyo Kero nikalipeleka Gari Car Wash nikalirudisha kulipark home, hamuwezi amini nilishinda ndani hiyo weekend yote hadi inaisha na Gari limepark tu uwani

Jumatatu hii hapa, Asubuhi na mapema nikawa najianda kwenda kazini, Nikaingiza vile vyombo kwenye gari ila Sasa nikawa nawaza hao police huko Barabara kwasababu Sina Driving licence, nikasema potelea mbali nikatekenya mchuma hadi kazini nikalipark kimya kimya kama sio Mimi nikaingia Ofisini kwaajili ya kuchapa kazi

Imefika Lunch time najiandaa kwenda kupiga Menu yule Mzee nikamuona anaingia Ofisini halafu ana hasira amekunja sura, nikajisemea hapa kimeshanuka nikaanza ku recall matukio ili nijue ni wapi nimekosea hasa kule nyumbani kwake, kote nilicheza safe na mara ya mwisho kuongea na huyu Mzee ilikuwa ni Ile Jumamosi akinipa mabadiliko ya ratiba yake huku akinipatia option mbili za yeye kupata gari yake, na Mimi nilivyochagua kubaki na Gari hadi Jumatatu sikumpigia tena simu kumjulisha uamuzi niliouchukua....nikapata majibu kwamba inawezekana hapo ndipo nilipo haribu, alikuja kwenye desk langu na kuniambia "nipatie funguo ya Gari na ukimaliza kazi nitafute" hata hakunisalimia akatoka nje ya ofisi akaondoka....

Inaendelea badae acha nipate msosi.....story yangu ina episode 6 tu, episode ya kwanza na ya mwisho (1 & 6) ndio muhimu zaidi Sababu ushauri wako ndio unahitajika hapo

1. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

2. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

3. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

4. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

5. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

6. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
 
Back
Top Bottom