Nahisi nimetapeliwa sijui nifanye nini?

Nahisi nimetapeliwa sijui nifanye nini?

Yes,Cha msingi usiwe mtu wa tamaa, Kuna jamaa yangu mtoto wa mjini aswaaa, anajenga nyumba na kuuza ndio issue zake uko mbweni ,now yupo Dom, basi ye pamoja na ujanja wake alipigwa mil.20 cash ,kiwanja Cha magumashi alipigwa.

Ivi naandika haya kashavuka maji yuko pemba kaenda kuua
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah, Pole sana ndugu! Ila huyo mkeo huyo....! Nsdhani wiki nzima hukuzungumza naye...! Una haki. [emoji34]
Niko mbali na nyumbani mkuu.Inanibidi tu kupiga simu maana yuko hospitali presha ilimshuka na hajatengemaa. Kiukweli natamani nipate mda hata wa wiki hivi bila kuongea nae ila ndio hivyo amenikaba na kuugua
 
Alikuwa na tamaa... ! Tamaa ni mbaya

Itakuwa walimuhaidi bonus!

Poleni sana , hopefully ata recover fasta, ili aweze kuendelea na mihamala kama kawaida
Asante mkuu.Nahisi kuna kitu walisema kuhusu ku boost commission akalamba ndoano😭😭
 
Wanawake huwa rahisi sana kutapeliwa!
Mie kuna demu wangu ni msomi ana degree na pia ana kazi nzuri tu halafu ni mtoto wa mjini na nilikuwaga nilishampa full story jinsi wanavyotapeliwa lakini cha ajabu siku moja anatoka bank kuchukua hela akalipe mafundi site kwake wajanja wakamuwahi wakamuuzia kipande cha mkaa "dhahabu" akaja kijiweni kwangu fasta eti ana habari njema alipoanza tu kusimulia kwamba amepata bahati ya kuwa tajiri ghafla nikamkatisha nikamwomba nione hiyo dhahabu alipofungua kile kimfuko anakuta kipande cha mkaa na alikuwa amekinunua milion moja laki nane.!
Bahati nzuri mazingira ya hapa Dom vibaka wengi nawajua maana nilishawahi kuwa mwizi zamani kwa hiyo nikaanza msako fasta mpaka nakuja kukamata waliomuuzia nikakuta pesa walishagawana wametumia wamebaki na laki nne na sabini tu wakanipa.
Lakini haikupita muda demu huyohuyo akatapeliwa pesa kupitia fb account fake ya mtu aliyejiita Jokate Mwegelo (Mkuu wa wilaya Kisarawe enzi hizo)
Yaani story ni ndefu ila niliamini wanawake akili zao za ajabu sana
Yaani wanawake sijui ubongo wao ukoje(kumradhi hapa).
Same na wangu tu nilishampa abc zote ajabu bado kafanya yale yale niliyomkataza
 
Halafu akanipa mm jukumu la kufuatilia kesi,siku ya kwanza tu kdg nimzibue vibao nkamchana braza...,hz mambo zipo kifamilia fuatilia mwnyw maana kwangu suspect namba moja hyu hyu shemeji nisije kuharibu mambo bure,for sure mi nltaka akabananishwe na wapelelezi kwanza maana mambo zingine haziingii akilini.
Si mchezo.ukiwa na roho ngumu kweli unaweza chukua maamuzi magumu
 
Haha unaweza ukakuta kanajifanyisha kanaumwa sijui presha..

we future hunyer ukiona kapost na status WhatsApp I'm sick mtoe Hospital kabisa anaweka bills ya bure .. tu

maana wanawake wengine kwa drama na maigizo wapo vizuri!!
Hahaha i am sick
 
Ukipenda sana miteremko ujue utakuja uingie mikononi mwa matapeli
 
Sema ni vile wengine hantakuja kununua kitu chochote kwenye dunia hii unaweza ukanunua vitu vya ghari na ukatapeliwa ila unatakiwa uangalifu mno kwa kila transaction ya fedha utakayofanya ila kupigwa tunapigwa tuu Mkuu..
Utapeli unaousema hapo labda iwe sijui bei ya kitu halafu nikapigwa bei kubwa.
Kifupi ningekuwepo wakati unapigwa ningeweza kukuokoa usipigwe. Nimeshaokoa wengi kutoingia kwenye madhira kama hayo. Mbinu za utapeli zinabadirika mara kwa mara. Ukiona ni dili la hela/mafanikio ya haraka au vitu cheap sana- kuwa mwangalifu.
 
Back
Top Bottom