kajojo
JF-Expert Member
- Jun 9, 2012
- 2,947
- 5,495
Dah jamani inaumiza, me ningezirai kabisaYaani kwa kujua hilo niliwaambia hata kwa namna yoyote ile asije mtu akakwambia sijui bonyeza namba flani kwenye simu usikubali.Nikawaambia na namba ni 100 tu zingine ni utapeli.
Tena niliwaasa kama kunatakiwa marekebisho yoyote msifanye chochote mpaka mnitaarifu.
Ila ajabu hata moja hakukumbuka. Kapigiwa simu kwenye namba za miamala baadae wakamwambia kuna marekebisho ya mtandao tunafanya kwa mawakala,wakaomba na namba yake kawapa.
Wakampigia kwa namba yake huku wanamwamuru abonyeze anachoelekezwa kwenye namba ya wakala.Yaan watu ni wa tigo wakampitisha tigopesa kawatumia wakaja voda napo kawatumia halotel katuma mpaka kumaliza hela damn!