Nafsi imesahaulika. (a rant).

Kwani energy ⚡ unajua ilivyo to it's core?

Au unatafuta logic utembee nayo tu?

Maana ni jinsi unavyo kuwa na attachments za objection hata unaona rahisi ku conclude mambo.

Tuachanene na labels maana unashikiria sana labels.

Energy umesema iko wazi.. Unaijua?

Achana na forms of energy nataka energy kama energy

Je, unaweza kuiterm energy katika muktadha upi?
 
Kama huwezi kui describe, ulijuaje ipo?
Kwa sababu ni kila kitu katika ulimwengu..

Matter yote iliyo visible na invisible is made up of energy..

Nikola tesla alisha sema

If you wanna understand the universe think of it in terms of energy, frequency and vibrations..
 
Hapa kwenye huu uzi bwana mdogo kuna kurukaruka sana kutoka kwenye hoja moja kwenda nyingine bila ushahidi wa kutosha. Kusema celebrities “huzaliwa wakiwa celebrities” au kwamba wanafanya kila kitu kwa maelekezo ni generalization kubwa sana. Umaarufu unaweza kuhusisha kipaji, mazingira, mitandao, fursa, marketing, connections, timing na juhudi binafsi—si lazima kuwe na mpango wa siri.

Vivyo hivyo, kuhusisha Bible, nyota, AI, DNA/epigenetics, GMO na additives za chakula kama sehemu ya mfumo mmoja unaopanga akili za vizazi vijavyo ni kuchanganya concepts tofauti kabisa.. AI inaweza kubadilisha namna tunavyofikiri na kujifunza, lakini hiyo si sawa na kusema itaprogram DNA ya binadamu au kwamba vizazi viwili vijavyo vitakuwa mashine. Hapo tunahitaji ushahidi wa kisayansi, si inference.

Na kuhusu GMO: GMO si sawa na sumu, wala kuwepo kwa GMO kwenye chakula hakumaanishi moja kwa moja kwamba chakula hicho kinaharibu uwezo wa mtu kufikiri. Vivyo hivyo, “additives” si kundi moja la vitu vyenye athari moja; usalama wake hutegemea aina, kiwango na matumizi.

Tatizo kubwa la hoja kama hii ni kuunganisha vitu vingi vinavyotia hofu, kisha kwa sababu vinaonekana vina uhusiano, kuhitimisha kwamba lazima kuna mfumo mmoja unaoviendesha vyote. Huo si uchambuzi wa kina; ni confirmation bias.
 
Kwani energy ⚡ unajua ilivyo to it's core?
Kutojua energy to its core ndio kuna igeuza iitwe Mungu?

Kutojua energy to its core hakufanyi iitwe Mungu.

Tunayo yajua kwenye huu ulimwengu ni yale tu ambayo yapo kwenye observable universe, Kuna vitu vingi hatuvijui vipo kwenye unobservable universe.

Lakini haviitwi Mungu.

Mungu ni dhana ya kidini na kiimani tu. Kwenye uhalisia haipo.
Muktadha wa Sayansi inayoenda kwa uthibitisho sio imani ambayo inafosi tu mambo bila uthibitisho.

Kwenye Sayansi Energy sio Mungu.

Sayansi haitambui Energy kama Mungu.

Science does not term "God" as energy. Science is empirical and studies the physical universe, while God falls outside the realm of scientific measurement and definition.

Kwa hiyo kwa muktadha huu hapa, huwezi kusema Mungu ni Energy. Kwenye Sayansi hii haipo.
 
Binafsi haya madai niliyaweka bayana kwa uzi ya kuwa nimegusia mambo mengi na mtu atachagua aspect ya ku discuss.

Na madai ya AI kuharibu DNA Sikusema physical destruction mkuu, ukielewa vibaya.

Pia kwenye GMO naelewa sio akili tu inayokuwa destroyed but for a large percent nerva za mwili ikiwa tinkered central nervous system nayo inakuwa prone to destruction..

Sasa ukiendelea kutokea inakwenda kuharibu vizazi via epigenetics.
 
Kwa sababu ni kila kitu katika ulimwengu..

Matter yote iliyo visible na invisible is made up of energy..

Nikola tesla alisha sema

If you wanna understand the universe think of it in terms of energy, frequency and vibrations..
Mimi nakubali kila kitu ni Energy.

Lakini kwenye Sayansi hakuna mahali inakubali kwamba Energy is equal to God.

Kwa hiyo ukisema Mungu=Energy. Hii inakuwa Sikweli na wala Sayansi haitambui hivi.

Labda kama ni imani yako binafsi, hapo sawa.
 
Nani aliye kudanganya?

Sayansi imetokea wapi? Kama sio dini na ancient mysteries?

Kwanza dini yenyewe umekuja baada ya watu kuona kumbe kuwa limited inaweza kuchukuliwa kama opportunity ya control ndo zikazaliwa worshipping agencies

Sasa na wewe usinibishie kuwa Mungu sio energy. Kama unalijua fika kuwa kila kitu ni energy. Na Mungu ni kila kitu including energy.

Achana na indoctrination ya kuwa Dini ni dhehebu la kiimani bali ni njia ya binadamu kujua ukweli ya kuwa yeye ni nani.

Ya kuwa yeye ni Mungu
 
mzee baba kuhusu issue ya AI, kuna hoja nzito sana ya kujadili kuhusu dependency ya binadamu kwenye AI, kupungua kwa critical thinking, attention span, creativity na uwezo wa kufanya maamuzi bila msaada wa teknolojia. Hizo ni hoja zinazoweza kuchunguzwa empirically. Lakini ukiziunganisha moja kwa moja na DNA, GMO, central nervous system na epigenetic inheritance, mzigo wa ushahidi unakuwa mkubwa zaidi.

Kwa kifupi, sina tatizo na hypothesis yako. Tatizo langu ni pale hypothesis unapoiwasilisha kama conclusion kabla ya mechanism yake na evidence kuthibitishwa. nafikiri tuweke kila claim kwenye kipimo chake cha ushahidi, ndipo mjadala unakuwa wa kisayansi badala ya kuwa wa inference.
 
Mimi nakubali kila kitu ni Energy.

Lakini kwenye Sayansi hakuna mahali inakubali kwamba Energy is equal to God.

Kwa hiyo ukisema Mungu=Energy. Hii inakuwa Sikweli na wala Sayansi haitambui hivi.

Labda kama ni imani yako binafsi, hapo sawa.
Ni kwa sababu science is just catching up to something kilicho sababisha yenyewe ianze millions of years ago.

Nayo ni ancient mysteries iliyo kuwa ruled by spiritual codes.

Ndo maana Nilikwambia uwe unaenda kupractice hizi vitu kama, angalau soma kuhusu Buddhism utapata glimpse ya nini namaanisha.

Hata hermerticism imetokea ancient teachings ambazo hazina relationship yoyote na hii limited science inayo leta mkanganyiko
 
Mbona ushahidi uko wazi via technological progress na madhaifu iliyo leta kwa society..

Tumeona increase in depression and mental illness, Tumeona magonjwa mabaya kama cancer, diabetes na hormonal imbalances.

Vijana wanazaliwa legelege, critical thinking nayo inazidi kupunguza, Inshort kuna thesis kibao mtandaoni zina Elezea haya..

Lakini pia before haya kuna movies, kuna projections kibao zineshafanyika kuonesha haya lazima yatokee
 
Mtumishi wa watu, unachokisema ni kweli kabisa technological progress imeleta madhara fulani kwa jamii, na kuna tafiti nyingi zinazochunguza uhusiano wa teknolojia na mental health, social isolation, attention, sedentary lifestyle na namna tunavyofikiri. Lakini depression, cancer, diabetes na hormonal imbalances havingekuwa ushahidi wa kutosha peke yake kuthibitisha kwamba technology ndiyo chanzo chake. Magonjwa hayo yana sababu nyingi zinazoshirikiana.

Vivyo hivyo, ukisema vijana wanazidi kuwa legelege au critical thinking inapungua, hiyo ni hypothesis inayoweza kuchunguzwa. Lakini tunahitaji longitudinal data inayoweza kuonyesha trend hiyo na sababu zake, si kuanzia kwenye observation halafu kurudi kutafuta explanation inayoi-support. Na kuhusu movies na projections—hizo zinaweza kuwa warning au speculative scenarios, lakini si ushahidi wa kisayansi kwamba tukio hilo lazima litokee. Movie inaweza kutabiri technology fulani kwa usahihi kwa sababu waandishi waliona mwelekeo uliokuwepo; lakini hilo halifanyi kila projection ya movie kuwa prophecy.
 
Nani aliye kudanganya?

Sayansi imetokea wapi? Kama sio dini na ancient mysteries?
Sayansi imetokea kwenye utafiti, udadisi na uchunguzi ambao umeleta facts na uthibitisho wa vitu.

Dini ni imani ya vitu tu, ambavyo wala havijafanyiwa utafiti na uchunguzi kupata uthibitisho wa vitu hivyo.
Huwezi kusema Mungu ni kila kitu, kabla hujathibitisha uwepo wake.

Unless otherwise, Utakuwa unafosi tu kwamba Mungu ni kila kitu bila kuthibitisha kwanza uwepo wa Mungu huyo.
Achana na indoctrination ya kuwa Dini ni dhehebu la kiimani bali ni njia ya binadamu kujua ukweli ya kuwa yeye ni nani.

Ya kuwa yeye ni Mungu
Wewe labda una sayansi yako binafsi inayosema kwamba Mungu ni Energy.

Lakini sayansi ambayo ni universal worldwide inayoenda kwa facts na uthibitisho haitambui Mungu ni Energy.

Wapo wanasayansi ambao walikuwa na imani zao kwa huyo Mungu. Lakini sio conclusion kwamba sayansi inatambua uwepo wa Mungu. Hizi zinabaki ni personal beliefs za hao wanasayansi tu.

Sayansi inayoenda kwa facts na uthibitisho haitambui Mungu ni Energy.
 
Toka kwenye AI mpumbavu wewe.
Use use your fucking brain...

Ndo maana nilikua sioni hata hoja yako iliko kumbe unatumia AI kuni jibu?
. Hizo vitu hazina msaada kama una akili
 
Sayansi imetokea kwenye utafiti, udadisi na uchunguzi ambao umeleta facts na uthibitisho wa vitu.
Basi jua tu ya kuwa God is all
Is everything na Energy is just an expresso..

Kama unabisha still wewe uko so ingrained na labels. Unataka kuweka label kwenye kila jambo, na huo ndo mtego hata kwenye science unawaramba.
 
Sayansi haija toka kwenye utafiti, sayansi ni matokeo ya utilization of ancient mysteries.

Hata Albert Einstein alitumia numbering and physics aliyoikuta na ilichimbuka kutoka ancient teachings ambazo hazikuitwa science kwa muda ule
 
Toka kwenye AI mume wangu.
Use use your loving brain...
tunatakiwa kutumia akili ili tuweze kutenganisha tunachokiona na kukipa tafsiri zetu vs tunachoweza kuthibitisha kuhusu chanzo chake kwa njia za kitaalamu zisizo na maswali.
 
tunatakiwa kutumia akili ili tuweze kutenganisha tunachokiona na kukipa tafsiri zenu vs tunachoweza kuthibitisha kuhusu chanzo chake kwa njia za kitaalamu zisizo na maswali.
Foolish. Achana na AI
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…