bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 883
- 2,137
Katika matukio mengi yanayotendeka hapa duniani mtu anaweza kuficha siri lakini ukimtazama machoni kuna kitu utatambua!
Moja ya Silaha kubwa sana kwa Mawakili na Wadau wengine wa haki ni MACHO......(Kuna aina 16 za mpepeso wa macho na kila mpepeso ni KIASHIRIA) kwani wanaweza kukutambua kwa URAHISI sana kile unachomaanisha machoni, aidha unadanganya, muoga, umefundishwa, huna uhakika ama unakomaa tu na utetezi wako nk
Nimeshuhudia visa kadhaa mfano CIA/wapelelezi wanapo kutana kazini huwa kila mtu anafanya yake, huwa wanatambuana kwa kuangaliana machoni! Why? isiwe sehemu nyingine ya mwili kama body structure n.k ilihali macho yana yanaakisi? Majambazi, Machangudoa, wagoni (mchepuko), wezi, wahalifu, wababe nk wakikutanisha macho tuu huwa ni jibu tosha !
Yatosha kusema kutazamana machoni silaha ambayo kila mtu anayo kwa asili yake (jaribu leo kumuuliza mtu kwa kumtazama machoni), bahati mbaya ni kwamba silaha hii imekua butu kwa wengi.......
Tabia kutazama macho pia ni suala ambalo mtambuka katika mila na tamaduni mbalimbali mfano huko kwenye nchi za Mashariki ya Kati na na Asia kuongea na mtu huku umemkazia macho ni utovu wa nidhamu lazima utazame chini ndio heshima.........pia yapo makundi ya wanadamu hasa wenye personality ya ukimya na aibu (Introvert ) wanahusika hapa (tafiti pia zinaonesha hivyo)
Bint anayepevuka au hata Bint wa kawaida tu akikuangalia machoni kisha akatazama chini au kwengineko ikisindikizwa na tabasamu huwa sjui wanamaanisha nini. Huwa naona wengi wanafanya hivyo.
Kwa wachina na watu wa tabaka lao na tamaduni zao, mtu ambaye anakwepesha macho, huyo ni muhalifu wa jambo Fulani . ila kwa mazingira hayo hayo, hasa kwa watawala , wafalme, nchi kama china, japan kukwepesha ni ishara ya heshima.
Wachawi na washirikina wengi wanaamini ukimtazama mtu kwa muda mrefu unaweza kumdhibiti na hata watafiti wengi wamezidi kukubaliana na hili la mtaguswa wa macho.
Upo msemo, Ukitaka kumuua Nyani usimuangalie usoni!.
Ukiweza wewe ni Jiwe!
Wenzetu wazungu kutazama pembeni ni dalili ya kuwa kuna kitu unaficha lakini kwa jamii zetu za kiafrika kumtazama mtu machoni (kumkazia macho) hasa aliyekuzidi umri au jinsi tofauti haina tafsiri nzuri (ima dharau ama kiburi)
Macho yanatambulikana kama ni mlango wa nafsi . katika imani nyingine za kienyeji za mwanadamu yanatambulikana kama ukweli , hekima , heshima na nguvu hasa unapomkodolea mtu macho .
Wapo wazazi ambao akiongea na mwanae usipomuangalia usoni na kujibu maswali yake anaweza hata kukupiga kwa nini humuangalii usoni
Kwa mujibu wa tafiti nyingi, hasa za kimahusiano katika eye contact . inaaminika watu ambao wanaangaliana machoni , wanaaminiana . kwa maana nyingine mtu asiyekuangalia usoni hakuamini na hawezi kukubaliana na wewe inaweza hata akakubali kwa maneno lakini si kweli moyoni.
Lakini anayeanzisha mgusano huo wa macho, ana mchango mkubwa sana katika mahusiano ,,, inaaminika anatawala mazungumzo au jambo husika ,,asiyeweza ametekwa ….
Mgusano wa macho usiopepesa , ni ishara ya kwamba upo makini , ni ishara ya kwamba wanaokutazama kama wameelewa , au hawajaelewa , aidha wana hasira na wewe , wanakuogopa unachosema au wanavutiwa na wewe . wale waongeaji wa TEDx wanafahamu ( Technology entertainment and design). Hapa ndipo elimu ya hadhira unapoanzia , nini cha kuongea na watu gani wa kuongea nao .
Mtu yeyote anayeogopa eye contact kuna uwezekano mkubwa sana akawa ni msahaulifu , kwa sababu mgusano wa macho unafanya ukupe kupokea moja kwa moja .
Ndugu Ignaz Paul vital troxler na ndiye mvumbuzi wa TROXLER EFFECT mwaka 1804 aligundua kuwa kwa kukodolea kitu kwa macho kwa muda mrefu kunafanya mazingira ya kitu husika kutoweka taratibu (fade) na kurithiwa na uzoefu ambacho kitu hicho kinacho , mfano unaweza ukaona rangi ya kijivu tupu lakini ndani yake kukawa na pink faded uhalisia hapo ni kijivu . ingawa troxler effect ina maelezo mengi sana katika visual perception. Na hata mwanadamu kweli na uongo vinamtindo wa kupishana , ukiendekeza uongo kuna siku utaumbuka kwa sababu ni lazima utasahau.
macho ya kibinadamu makengeza, mekundu makubwa etc
Macho ya mtu hufikisha la moyoni mwake haraka sana kuliko mdomo, muangalie ndugu, rafiki au jamaa yako pale unapomweleza kwamba nimefanya hiki cha mafanikio utaona mapokezi yake katika macho na si katika mdomo, mdomoni atakudanganya tu macho hayadanganyi hata siku moja, mwenye huzuni mwangalie machoni, mgonjwa na mwenye furaha mwangalie machoni, macho yanakupa ukweli wa tabia ya mtu hivyo usipomuangalia usoni utaishia kubahatisha na kuweka labda labda nyingi tofauti na uhalisia wenyewe. Tuwe na tabia ya kumwangalia mtu usoni katika mazungumzo.