Nafikiria kuhama Catholic

Nafikiria kuhama Catholic

Mawazo chanya tayari unayo. Sadaka zako elekeza kwa wahitaji, mfano wafungwa, wagonjwa, yatima, wajane na wazee maana hii ndiyo ibada inayomfurahisha Mungu wa Mbinguni. Na ukiishi hivi Mungu mwenyewe atakuinulia watu na marafiki wapya wengi sana. Lkn ukitaka kuzikwa vizuri kwa mapambio na jeneza kupelekwa kanisani na misa ndeefu... basi wekeza sadaka zako kwa ma padre na viongozi wa kanisa. Amua tu unataka lipi ?
Hapo juu umeandika vizuri sana but usiupotoshe umma hapo nilipo-bold,Imani Katoliki inamjali yeyote ikiwa tu alijijali yeye mwenyewe alipokuwa hai kwa kufanya yale yanayompasa.

Kuwa muumini hai kwa kuhudhuria jumuiya ndogo ndogo,(hata kama hatoi hata cent moja) na kutoa zaka hata mara moja kwa mwaka,zaka ni msingi wa imani kwa sababu unaonyesha shukrani kwa Mungu unayeamini ndiye amekupa mafanikio so acha kudanganya watu kuna kuwekeza hela Kanisani ili upewe heshima hata uwe nani hutekelezi imani utazikwa kama walevi wengine tu
 
Yeye anataka akitoa sadaka aitwe madhabahuni ili waamini wote wamjue yeye ndiye ametoa nyingi zaidi!

Shida kubwa sana hii Kanisa linaonekana limejaa lakini wengi hatujui tumeenda kusali au kujionyesha uwezo wetu.
Hasomagi biblia huyu, hajui kilichomo kwenye Mathayo 6:3-4!
Asituchoshe
 
Leo ndio unafahamu kuwa Catholic ni na hawapo kiroho hata siki moja

Proud to be Muslim
Funny,very funny!!!

Ndiyo maana kumbe upo bega kwa bega na sa100 japo katuulia ndugu zetu Watanganyika 10K+tena baadhi waliokuwa majumbani mwao wala hujisikii aibu kwa sababu mna-share dini?“proud to be” ni kichekesho cha karne,niamini mimi mdau.
 
Mada iliyopo mezani haihusu hayo uliyoandika
 
Hi,
Happy New Year.

Binafsi nimekua mzito kushiriki ibada ya jumuiya, Misa za kanisani au mambo yoyote yahusuyo kanisa katoliki. Sijawahi kuwaza hivi toka nikiwa najielewa but now things are dreadful to me, nilikua naioenda sana hii imani and proud ila kwa sasa naona napoteza muda wangu.

Mkesha xmass nilienda kanisani ila ikabidi nikae nje tu mpaka ibada ilipoisha...never happened before. But niliona naenda poteza muda tu.

Why???
👉 Katoliki halimthamini mtu mwenye roho wa Mungu na mwenye Upako ndani yake, Ila yule anayetoa michango

👉Halithamini sadaka zako unazoto kwa yatima,wagonjwa,wazee, na wenye njaa..ila tu ILE MICHANGO UNAYOCHANGIA KANISANI
👉 Halithamini kujitoa kwako juu ya kanisa ila tu kwa PESA UNAZOTOA KANISANI.

👉Pesa tunazochanga zinaenda kuhusumia wanawake zao na watoto wao waliowapata nje ya utaratibu wao.

HIVYO.....
Yule anayetoa pesa kanisani na kua na ukaribu na viongoz wa kanisa, Mapadri nk ndio mwenye thamani zaidi.

Naomba mnipe mawazo chanya niweze kurudi relini aisee.... Mawazo ya kuhama yamenijaa ila sijui niende wapi ambapo THEY DON'T CARE ABOUT MATERIAL BUT SPIRITUAL AWAKENING

NB. Catholic sio mbaya ila wanao liongoza ndio shida.

Kweli there's a price to pay when you know a lot of things you weren't supposed to know
✖️
Utaenda wapi ambako hakuna michango?
 
Mi wanapo nikwaza Wakatoriki ni Ibada ya
Kuisujudia Sanamu ya Kike tu:
Kwakweli wananikwaza sana hata Sina hamu:
Hii na Karne ya Kizazi kipya:
Siwezi kuisujudia Sanamu ya Kike ya SIMENTI kamwe
Mimi mkatoliki lakini sijawahi kuabudu sanamu
 
The right choice , watu tulihama huko miaka Mingi sana. baada ya kulijua hilo .

no spiritual awekening anymore
 
Akitaka sifa aende Jumuiya 🤣
Ila Kanisani Padri akishasema salini ndugu ili sadaka yenu na yangu ikubaliwe na Mungu Baba Mwenyezi imeisha hiyo
😂😂😂😂😂😂😂
Au anataka pia akifanya usafi Kanisani atangazwe pale mbele na Padre kwamba Vinci ndiye alipamba Kanisa.

Ila akienda Pentecoste huko
Hasa kwenye huduma changachanga atapata hiki anachokitaka...japo baada ya muda pia atachoka tu maana michango haiishagi.
 
Katoliki ni kama Bunge.. Wabunge wako pale kuwakilisha majimbo yao na wananchi wake, same to Katoliki muwakilishi wako ni Jumuiya.
Kanisa likianza kum appreciate mtu mmoja mmoja na utoaji wake sadaka, Misa itaisha saa ngapi?
Padri anaposema salini ili sadaka yenu na yangu ikubaliwe na Mungu Baba Mwenyezi uwa umesinzia? Zile baraka hapo hazikutoshi mkuu?
Anataka hadi itajwe kabisa ya kwake specifically 😂😂😂💔🙌
 
Yeye anataka akitoa sadaka aitwe madhabahuni ili waamini wote wamjue yeye ndiye ametoa nyingi zaidi!

Shida kubwa sana hii Kanisa linaonekana limejaa lakini wengi hatujui tumeenda kusali au kujionyesha uwezo wetu.
Na hiyo siyo Kanuni ya sadaka
Akishajua namna ya utoaji wa sadaka kibiblia, hataangaika na haya mambo ya kutaka kutangazwa na kusifiwa sana.

MUNGU mwenyewe Mbinguni ndiye anayepokea sadaka zetu zote,,zilizoonwa na watu..hata zile zisizoonwa na watu.
 
Hama tu mkuu 😂 sema na moyo wako tu , Me nilishaacha hata kusali kitambo tu.

Sema lile chuma limepitia mapito mengi sana mpaka leo wataendelea tu kuwepo walishajiengua watu huko ukiachana na Martin Luther , Henry VII mfalme wa uingereza alijitoa sababu kubwa ikiwa kukataliwa ruhusa ya talaka na Papa, ndo ikaanzishwa Church of England na akawa kiongozi wake mkuu na bado hao Anglican bado sana kuwafikia wakatoliki yaan bado.

Kuna kina Charles Chiniquy jamaa alikosoa sana mamlaka ya papa, Menno Simons huyu alipinga ubatizo wa watoto na Muungano wa kanisa na serikali ,
William Tyndale huyu alitafsiri biblia kwa lugha ya kiingereza bila idhini ya kanisa tena walimchoma moto kabisa 😂
Jan Hus huyu nae alichomwa moto tena ni padre kabisa huyu alikosoa ufisadi kanisani tena huyu ni kabla ya Luther.

Wengi wao hawakuanza kwa chuki, bali kwa kukosoa mafundisho, mamlaka ya Papa, au mienendo ya Kanisa.
Wengine walitaka marekebisho ndani ya Kanisa, lakini walikataliwa au kuadhibiwa.

Kwa hiyo mkuu hautakua wa kwanza, Dubwasha litaendelea tu kuwepo mpaka kristo arudi.
 
Ellen G white mwenyewe alishakiri Hilo dude haliwezi kutetereka,miaka ya mbele sabato itasambaratika lakini Hilo dude ni mpaka ukamilifu Wa dahari!
 
Eti Katoliki halimthamini mtu mwenye roho wa Mungu na mwenye Upako ndani 😀😀😀 Nenda kwa Mzee wa Upako! Kwani umelazimishwa kusali Katoliki 😀 Kwamba ukihama kanisa litatetereka? 😀 Nenda tu kwa Mwamposa, Sisi tupo sana tunasali rozary, na kukamilisha sehemu muhimu ya Liturjia ya misa Takatifu kwa kutoa sadaka na majitoleo! Tunaungama ubatizo mmoja, Maondoleo ya dhambi na Sakramenti muhimu. Tunakutakia kila lenye heri huko uendapo!
 
Yaani mtu ana PhD. Heri yetu sisi tunao tunaosuijudu na kutukuza laana, tukitoka hapo tunapiga shetani mawe ya kutosha. Hebu hamieni kalamu dini ya kweli kabisa huhitaji Phd, elimu ya madarasa ni ulimi ya mtume wetu SAW ambayo kwayo tumeangalia mabikra kama yote, na nguvu za ziada juu yake, natamani kujilipua hata muda huu wabillah tawfiq
Halafu anaisujudia Sanamu ya KiKE ya SIMENTI kweli ndio hivyo...!😭😭😭😭
Mnamsingizia sana Mama wa Yesu na yeye hataki mufanye hivyo:
Huu ndio UKWELI
 
Attachments

  • Screenshot_2026-01-03-11-06-14-77_1c337646f29875672b5a61192b9010f9.jpg
    Screenshot_2026-01-03-11-06-14-77_1c337646f29875672b5a61192b9010f9.jpg
    68.3 KB · Views: 13
Anataka hadi itajwe kabisa ya kwake specifically 😂😂😂💔🙌
Mwanzo wa mwezi uwa wanataja baada ya sadaka ya kwanza. Muda wa vipaji, mf. Leo jumuiya flani italeta vipaji au familia fulani ina sadaka ya shukrani.. asubiri hizo, mbona zinakuwepo. Ni kwamba hajui au kusudi 🥹
 
Back
Top Bottom