MZUNGU ana access ya siri za serikali

LIYUNGU,
Code:
Nabii unayajua haya maana uko Holland sasa unamalizia masomo yako na wewe kila mara uko na Damian.
Wewe hujawahi kusimama na kufanya kwa kujituma kama anavyo fanya jamaa mbali ya kuwa DJ kila mara.

LIYUNGU, SAMAHANI JARIBU TENA KUFANYA UTAFITI WAKO VIZURI ILI TUFAHAMIANE ZAIDI NA NI KITU GANI NINACHOANDIKA HAPA. UDJ TENA? MBONA SIKUELEWI UNACHOSEMA?
MAELEZO NILIYOTOA MIMI NI MAJIBU YA MAELEZO YAKO AMBAYO HUZAA MASWALI MENGI SANA NA PIA UNAKUWA NA LUGHA YA KUJIGHAMBA KITU AMBACHO SIKIFAGILII HASILANI. MFANO ANGALIA MANENO UNAYOANDIKA MWENYEWE:-



Code:
[COLOR="red"]Mimi nina data nzito na bado nadhani he is right kufanya hayo maana mimi na wewe hatuwezi kumpunguzia lolote kwa serikali[/COLOR]

SASA HAPO NDIPO UNAPOULIZWA DATA NZITO ZIPI? NA KWA NINI SASA ZIWE SIRI WAKATI WEWE UNASEMA U MUWAZI AU HUMWOGOPI MTU? NDG. YANGU HAKUNA CHUKI NA MTU HUENDA NI JINSI UNAVYOJIELEZA NDIO UNAZUSHA MASWALI MWENYEWE. TENA ULISEMA,

Code:
[/B]Kelele zako juu ya huyu jamaa na mambo yake unazianza leo lakini sisi tumeanza zamani na sasa tumeamua kukaa kimya si kwamba tunakubal ila hatuna namna.
Bado tueleze uoga wako na grudges zako against huu mtandao na kwa nini unadhani unahitaji Katiba kwa malengo yapi.Otherwise kwa huyu Consular nasema wewe si wa Kwanza kulalamika watu wamesha mweleza hata Mkapa uso kwa uso akauchuna .
Hakkenburg alivyo pata nafasi ya kuwa Konsgula sijui lakini mimi Lunyungu nimefanya naye kazi kwa karibu sana na ananijua nilivyo mchungu kwa Nchi yangu na hataki kunisikia mimi. Na hivi siko Holland tena nadhani anapeta.

SAWA KAMA UMESHACHOKA UNATULIA TU WENGINE NAO WAENDELEE, INAWEZEKANA, NJIA ULIZOKUWA UNATUMIA KUTAFUTA UFUMBUZI ZILIKUWA SI NZURI AU KELELE ZAKO ULIZIPIGIA KULIKO SIKO,HATUJUI. WENGINE NAO SASA WATAENDELEA KWA STAILI ZAO, WAKICHOKA NAO WAKAE KIMYA, WENGINE WAENDELEE MPAKA SIKU YA KIAMA, AMBAPO ALLAH ATAKAPOKATA SHAURI. ZAIDI YA YOTE UNATUTUSI WATANZANIA WOTE UNAPOSEMA HIVI,

Code:
[I]Watanzania wenyewe wakiambiwa wajipange wafanye mambo yao hawawezi wanaona 10 euro ni kubwa na jamaa kwa kuwa anataka ujiko anachofanya ni kusema na viongozi wale na kutoa pesa ili wakutane .

Watanzania wana maneno tu kutenda hapana. Huyu mzungu ana matatizo sana lakini sasa tufanyeje ? Mwaka 2005 August Mkapa aliulizwa mbele yake kwamba kwa nini asiondolewe tukawa na mzawa na balozi majibu ni ya Mkapa jamaa anajitolea sana so mwacheni aendelee ila ataweka note kwenye hand over notice kwa rais ajaye

Kwa tabia za watanzania ni waongeaji kama hivi lakini you got no idea ugumu wa kuendesha mambo haya[/I]



LIYUNGU, BINAFSI NATOFAUTIANA KWA NGUVU ZOTE NA WEWE KATIKA MANENO KAMA HAYO HAPO JUU YA MAJUMLISHO YASIYOLETA MANTIKI WALA KUKUBALIKA.YAANI WEWE UNAONA WATANZANIA WOTE (INCLUDING YOU?) ZAIDI YA MILLION 40.5 KUWA NI WAZUNGUMZAJI TU NA KWAMBA HIYO NI TABIA YETU?? UKIAMBIWA UTUHAKIKISHIE HILO UTAWEZA? EBU JIFUNZE KUELEZA VITU ULIVYO NA UHAKIKA NAVYO NA BILA HAJA YA KUJISIFU KUWA WEWE NDIWE PEKEE MTENDAJI MWENYE UFANISI.
MAANA HATA SEHEMU NYINGINE ULISEMA KUWA BAADA YA KUONDOKA SASA KONSUL ATATESA AS IF WEWE PEKEE NDITE ULIBARIKIWA UTENDAJI BORA. KAZI YAKO INAWEZA KUWA NZURI, TUTAKUPONGEZA LAKINI HUNA HAJA YA KUWAONA WATANZANIA WENGINE WOTE KUWA NI VIBONDE.



Code:
[COLOR="red"]Tumia lugha kidogo ya ustaraabu wacha kuonyesha chuki[/COLOR]

SAMAHANI SI KAWAIDA YANGU WALA SIJAONYESHA CHUKI BALI NILIKUWA NAJIBU MASWALI YAKO MENGI BWANA LIYUNGU. WALA SINA TABIA YA KUBISHANA NA WEWE NA WALA SIJAWAHI KUBISHANA NA MTU KWA AJILI YA MABISHANO TU.
***********************************


NAKANDAMIZA KIBARA
Code:
[COLOR="red"][I]Nabii najua huyu jamaa unatoka naye mkoa mmoja huku Tanzania beef yenu inaanzia wapi [/I][/COLOR]
.

SAMAHANI KAMA WEWE UNATOKA NAYE MKOA MMOJA, SI KILA MTU, ENDELEA KUBASHIRI TU PENGINE TUTAFAHAMIANA VIZURI ZAIDI. MIMI SINA BEEF NA UNAYEMZUNGUMZIA, BALI HUWA NINA BIFU NA MATENDO YA MTU YEYOTE YULE YASIYO FUATA UWAJIBIKAJI UNAOPASWA.

Code:
Matatizo ya Consul si ya Damian tunayajua sote na tumesha sema hata mbele ya Rais pale The Hague majibu yake kila mmoja aliyasikia
.

NI MATATIZO GANI AMBAYO WEWE UNAYAFAHAMU AMBAYO YALISHINDIKANA KUONGEA NAYE (KONSULI MWENYEWE) NA AU BALOZI WETU MPAKA IKABIDI MMWAMBIE RAIS? NA JE SASA TUISHIE HAPO, KWA VILE MLISHA YAWASILISHA HUKO THE HAGUE?

Code:
Yeye anauza visa na mambo mengine kama ya utalii anatumia pesa za visa kutengeneza makaratasi na dvd na CD rom nk za utalii Tanzania.

INAONEKANA UNAJUA SANA TAARIFA YAKE YA FEDHA YA MAPATO NA MATUMIZI. HEBU TUMEGEE KWA UFAFANUZI ZAIDI MATUMIZI YA VIZA KUTENGENEZA MAKARATASI NA CD ROM N.B (zipi) KILA WAKATI

Code:
Sasa tafadhali sema shida yako na Damian ni ipi na network ya watanzania si umoja ule maana walio wengi ni wanafunzi ambao hawana muda wa kuunda umoja
.

NILISHASEMA SINA SHIDA NAYE; MAELEZO YA NETWORK YALITOLEWA KAMA MASAHIHISHO, PALE AMBAPO LIYUNGU ALIPOELEZA KUWA HUO NI MTANDAO AMBAO HAUMILIKIWI NA YEYOTE WALA HAKUNA ANAYE UCONTROL KITU AMBACHO SI KWELI. GET IT RIGHT, RUHUSA YA MTU YEYOTE KUJIUNGA NA MTANDAO HAINA MAANA KUWA MTANDAO HUO HAUNA MWENYEWE AU KWAMBA AUNA CONTROL!

Code:
Hapa wabongo wa Holland wanazidi kukubali kazi ya Damian jamani mimi nataka sasa muone maneno ya Nabii kama kweli huyu mtu anachukiwa anajipendeza .Naweza comment za wengine na barua ya Damian kwa Balozi Mlay.

NAKANDAMIZA KIBARA, NASHUKURU KWA KUTUONYESHA KAZI NZURI YA HUYU BWANA, MAANA UMEJITAHIDI KUWA MKWELI KATIKA KUNAKIRI ILIVYO YALIYOMO KATIKA BARUA YAKE (KUONYESHA KUWA ANAPIGANIA HAKI) LAKINI PIA NIKUKUMBUSHE KUWA UMEGUSHI SAINI YA MTUMA UJUMBE HUO KWA KUKANDAMIZA KI-(BARA)X2, UMEANDIKA IFUATAVYO:
“… Damian
Katibu wa muda wa Watanzania
”

LAKINI VYANZO VYANGU VYA HABARI VIMELETA HIYO SAINI KAMA ILIYOANDIKWA NAYE KAMA IFUATAVYO.
“…
Damian
Katibu wa Watanzania wa Holland”


HAPA NDIPO TUNASEMA ‘WE SMELL A RODENT’, NI WAZO LA BUSARA TU LITOLEWALO KWAMBA HILO NENO ULILOONGEZA LA ‘MUDA’ HUWA LINAPASWA KUJULIKANA YAANI MUDA GANI? TATIZO SI YEYE NI UTARATIBU NDIO UNAGOMBA HAPO. AMA UCHAGULIWE (MAANA UNAFAA) AU USIJIITE KIONGOZI WA WATANZANIA WA HOLLAND! MTU AKIPENDEKEZA UCHAGUZI USIMCHUKULIE KUWA HAKUPENDI ANAKUSAIDIA UWE NA LEGITIMACY YA KUONGOZA.
***************************

KAFARA
Code:
ni vyema kama malalamiko ya nabii yamepelekwa kunakohusika kama
mkuu mwawado alivyoshauri na naamini wahusika watafuatilia.

SHWARI!


Code:
awali kulikuwapo na visa za muhuri. hii viza ilikuwa muhuri mkubwa unapigwa kwenye page kisha maeneo yanayohusika yanajazwa kwa mkono kwa mfano, muda viza, tarehe ya kutolewa
balozi iliyotowa viza nk. hata hivyo mfumo huu wa viza nadhani sasa umepitwa na wakati na balozi nyingi
zinatoa viza za kubandika (sina hakika kama balozi zote za tanzania zinatoa viza za kubandika
)

ASANTE KWA MAELEZO MAZURI NA NADHANI SASA HATA MKAMP ANAWEZA KUELEWA TUNACHOKIELEZA JUU YA VIZA ZA MIHURI
*********************


MKAMAP
Code:
Ila nilivyojitahidi kuelewa maudhuhi ya waandishi si kweli wanalaumu mholazi kuwa consula Bali kuna baadhi ya watanzania wanafaidika na kuwepo kwa mholanzi na wengine hawafaidiki sasa hapo ndipo beef linapoanza the better soln ni kumuondoa ili wote watoke suluhu ,hapa wabongo ndipo hua nawapenda yani loss-loss Big yes win-null Big no
Am sorry Nabii kama mtazamo wangu ni ndivyo sivyo

NDG. MKAMAP, HUNA HAJA YA KUOMBA MSAMAHA MAANA KAMA ULIVYOSEMA HUO NI MTAZAMO WAKO. LAKINI WANGU NI KUWA SIDHANI KAMA KUNA MTU ANAFAIDI HAPA AU LA, SUALA NI KUWA HUDUMA ANAZOTOA KONSULI, ENEO LA OFISI YAKE NA MAWASILIANO YAKE HAYARIDHISHI NDIYO MAANA WOTE TUNAKUBALI KUWA ANA MATATIZO MPAKA IKABIDI MALALAMIKO YAWASILISHWE KWA RAIS ALIYEPITA. TUNAPOTOFAUTIANA NI KUWA, LIYUNGU ANAONA HATUWEZI KUFANYA CHOCHOTE ETI KWA KUWA HUYU JAMAA ANAFANYA HIVYO KWA SABABU YA AMA ANA FEDHA NYINGI, ETI HATA RAIS WA SASA ANAMTEGEMEA NA AU ANA MAHUSIANO NA WAKUU, MIMI NASEMA HILO HALIKUBALIKI NA KAMA MTU HATOI HUDUMA NZURI KWA UMMA KATIKA OFISI ALIYOKABIDHIWA ANATAKIWA KUREKEBISHWA NA KAMA HAREKEBIKI AWAACHIE WENGINE WAHUDUMU. HIVYO TUTAENDELEA KUTOA TAARIFA POPOTE NA NINA UHAKIKA HILI LITAREKEBISHWA!
***************************

ZOMBA
Code:
Mbona Oman tulikuwa na konsela mwarabu, mmanga, muomani ambae alizaliwa bukoba na akaukana uraia alipofika oman, na aliwakilisha vizuri tuu.

ZOMBA, FUATILIA LIZUNGUMZWALO HAPA. WATU HAWAZUNGUMZII RANGI YA NGOZI YA MTU WALA NASABA YAKE BALI KUTORIDHIKA NA UTENDAJI WA MTU ALIYEKABIDHIWA OFISI AU MAJUKUMU YA SERIKALI.

Mchoro wa hitimisho lako unakwenda hivi:

Kiongozi Mwarabu alifanya kazi nzuri huko Oman kwa niaba ya Tanzania,
Katibu Mzungu wa Nyerere pamoja na kujua siri nyingi za serikali alifanya kazi nzuri.
Kwa hiyo ‘Consul’ Mzungu wa Uholanzi lazima naye atafanya kazi nzuri tu.


Zomba utakuwa unakabiliwa na gonjwa hatari lijulikanalo kama ‘Dicto simpliciteritis’ na pengine ‘the slippery slope argumentitis’, maana unaridhika na kujiachia tu katika utelezi.
Mpaka utakapotibiwa, hitimisho lako katika thread hii linaitwa taka.


Code:
Mie nnauhakika wewe ni Mwanga, mchawi mkubwa wee! na kama si mwanga basi unatoka kwenye ukoo wa wanga.

Asante kwa sifa!

Back to the topic.

Malalamiko ya kutoridhika na Mtendaji wa ofisi na mawasiliano yake na Watanzania na pia Ubalozini na mahala ofisi ilipo, yameshafikishwa kunakohusika, subirini uchunguzi ufanywe na Wakuu wake na maboresho yakifanyika tutajulishana..
 
Nabii ahsante sana kwa kuujuwa ugonjwa unaonisibu, duuh, ulijuwaje wewe? wee mwanga kweli!

Mie nakwambia huna lolote ni wivu na roho mbaya inakusumbuwa. Jee ulitaka wewe uwe huyo konsela? au wewe unaona wivu kwa kuwa wenzako wameweza kuwa karibu nae nawe ukashindwa? ndio kiroho kinakuuma na matumbo yanakukata kwa roho mbaya? Hebu sema kweli! au alikataa kukukopesha gari?

Yaani wewe umeleta hoja ya utumbo kabisa, ni hoja ya mtu mwenye roho mbaya kabisa. mimi kwa upande wangu, hunijuwi sikujuwi wala huyo mzungu simjuwi lakini kwa maandishi yako, yalivyo jaa chuki na wivu wa kichawi ni bora nikutane na nyoka mwenye vichwa saba kuliko kukutana na mwanga wewe.

Hivi mimi nakuuliza ni watu wangapi ambao umesha wagombanisha kutokana na fitna zako? zaidi ya hii kwa huyu mzungu sasa hivi.

Pole sana kaka, nachukulia kuwa wewe ni Mu-Islam (kutokan na maandishi yako yaliyopita), kama ni hivyo, basi naomba urudi kwa mola wako na uombe toba kwa sana. Hakuna kitu kibaya kama kuwa fitna, mwanga na mchawi.

Mie nadhani hapo uholanzi hata wabongo wengine wamesha-kustukia kuwa wewe ni hatari sana. Kwenye maandishi tu unaonesha una-chuki za kijinga, Jee live inakuwaje? au huijuwi system ni nini?
 
"NDG. MKAMAP, HUNA HAJA YA KUOMBA MSAMAHA MAANA KAMA ULIVYOSEMA HUO NI MTAZAMO WAKO. LAKINI WANGU NI KUWA SIDHANI KAMA KUNA MTU ANAFAIDI HAPA AU LA, SUALA NI KUWA HUDUMA ANAZOTOA KONSULI, ENEO LA OFISI YAKE NA MAWASILIANO YAKE HAYARIDHISHI NDIYO MAANA WOTE TUNAKUBALI KUWA ANA MATATIZO MPAKA IKABIDI MALALAMIKO YAWASILISHWE KWA RAIS ALIYEPITA. TUNAPOTOFAUTIANA NI KUWA, LIYUNGU ANAONA HATUWEZI KUFANYA CHOCHOTE ETI KWA KUWA HUYU JAMAA ANAFANYA HIVYO KWA SABABU YA AMA ANA FEDHA NYINGI, ETI HATA RAIS WA SASA ANAMTEGEMEA NA AU ANA MAHUSIANO NA WAKUU, MIMI NASEMA HILO HALIKUBALIKI NA KAMA MTU HATOI HUDUMA NZURI KWA UMMA KATIKA OFISI ALIYOKABIDHIWA ANATAKIWA KUREKEBISHWA NA KAMA HAREKEBIKI AWAACHIE WENGINE WAHUDUMU. HIVYO TUTAENDELEA KUTOA TAARIFA POPOTE NA NINA UHAKIKA HILI LITAREKEBISHWA! "

Nabii sikuelewi!!!!!!!!!!!!!!
Hoja yako ni ipi haswa?? maana naona unakula Uturn la nguvu
maana mwanzo ulidai ana access nyaraka za serikali saizi wasema huridhishwi naye ktk uwajabikaji wake.
kuwa mwazi ni yepi yanayokusibu ndugu yangu????
 
"NDG. MKAMAP, HUNA HAJA YA KUOMBA MSAMAHA MAANA KAMA ULIVYOSEMA HUO NI MTAZAMO WAKO. LAKINI WANGU NI KUWA SIDHANI KAMA KUNA MTU ANAFAIDI HAPA AU LA, SUALA NI KUWA HUDUMA ANAZOTOA KONSULI, ENEO LA OFISI YAKE NA MAWASILIANO YAKE HAYARIDHISHI NDIYO MAANA WOTE TUNAKUBALI KUWA ANA MATATIZO MPAKA IKABIDI MALALAMIKO YAWASILISHWE KWA RAIS ALIYEPITA. TUNAPOTOFAUTIANA NI KUWA, LIYUNGU ANAONA HATUWEZI KUFANYA CHOCHOTE ETI KWA KUWA HUYU JAMAA ANAFANYA HIVYO KWA SABABU YA AMA ANA FEDHA NYINGI, ETI HATA RAIS WA SASA ANAMTEGEMEA NA AU ANA MAHUSIANO NA WAKUU, MIMI NASEMA HILO HALIKUBALIKI NA KAMA MTU HATOI HUDUMA NZURI KWA UMMA KATIKA OFISI ALIYOKABIDHIWA ANATAKIWA KUREKEBISHWA NA KAMA HAREKEBIKI AWAACHIE WENGINE WAHUDUMU. HIVYO TUTAENDELEA KUTOA TAARIFA POPOTE NA NINA UHAKIKA HILI LITAREKEBISHWA! "

Nabii sikuelewi!!!!!!!!!!!!!!
Hoja yako ni ipi haswa?? maana naona unakula Uturn la nguvu
maana mwanzo ulidai ana access nyaraka za serikali saizi wasema huridhishwi naye ktk uwajabikaji wake.
kuwa mwazi ni yepi yanayokusibu ndugu yangu????
mkamap, huyo nabii ni kama nilivyoeleza hapo juu, hana lolote ni roho mbaya tuu, ndio maana anazunguka-zunguka bila mpango. Au haijuwi system ni nini?
 
Mimi nimekuwa kwa muda natafuta ukweli wa huu nuongo wa huyu Nabii sijui wa wapi .Sasa nimepata namba za watuhumiwa na ni bora sana sana .Mwanakijiji kama kawaida ukatuletea hawa watu kila mmoja akajibu tuhuma zake .

Namba za Mzungu yaani Consula Frans J Hakkenburg ni +31653245838 ama direct line ni +31 180330059

Damian wa Wabongo network ni +31641998601

Hii ni kutaka kusikia kama tuhuma za huyu Nabii zina ukweli ama ana majungu na chuki binafsi ?
Pia bwana Nabii naona hujanijibu ila umekezana na quotes za Lunyungu je mimi maneno yangu na yale ya watanzania wa Holland kumpa pongezi jamaa umeyaona hapa ? Maana najua unapokea mails z Wabongo je kazi ya jamaa kuna bado dispute kama unavyo dai ?
 
....................Tuletee Habari Zaidi Ili Wengine Tuweze Kuwauliza Wahusika Vizuri Nimeongea Na Kijana Mmoja Anafanya Kazi Hapo Anakataa Hakuna Kitu Kama Hicho Huyu Ni Mtaalamu Wa Mambo Ya Mawasiliano Nilisoma Nae Chuo Kimoja Na Sasa Kama Itakuwa Ni Kweli Basi Hata Huyu Kijana Haina Maana Ya Yeye Kuendelea Kuwa Katika Nafasi Hiyo Aliyopo Pale

Kule Chuoni Alikula Viapo Zaidi Ya 3 Kutokana Na Kumbu Kumbu Zangu

shehe alikula viapo gani hivyo???
alisomea udaktari? maana kwa ubongo wangu naamini kuwa polisi, wanajeshi na madaktari ndio wanakula viapo...... (usukununu tu usiogope)
 
Code:
[COLOR="DarkRed"]Zomba
Pole sana kaka, nachukulia kuwa wewe ni Mu-Islam (kutokan na maandishi yako yaliyopita), kama ni hivyo, basi naomba urudi kwa mola wako na uombe toba kwa sana. Hakuna kitu kibaya kama kuwa fitna, mwanga na mchawi[/COLOR]
.



Shukrani tele Zomba kwa kunijalia sifa. Rejea katika SURATUL ANBIYAA, iliyoteelemka Makka kwa ajili yangu na wewe katika khali kama tuliyonayo sasa juu ya ninenayo nabii na kuchukuliwa kama ya Wakureshi;

’Sema; Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayo mbinguni
na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.



Code:
MkamaP
...naona unakula Uturn la nguvu, maana mwanzo ulidai ana access nyaraka za serikali...


MkamaP fuatilia kwa makini thread hii toka mwanzo. Aliyepresent hoja ya ‘mzungu na access ya siri’ si mimi bali GT na akaungwa mkono na wengi tu. Rejea post yangu ya mwanzo mimi binafsi na hata Liyungu mwenyewe tulieleza matatizo aliyonayo huyo jamaa na mahala ilipo ofisi yake. Kuna watu walichangia humu pia kuwa Konsul sio lazima awe Mtanzania na wakatoa mifano ya waliofanya vizuri kwingineko. Lakini pia hakuna anayeeleza humu kuwa utaratibu ni kwamba Konsuli lazima awe asiye Mtanzania hata kama kazi yake hairidhishi. Zaidi ya yote hakuna alieeleza jinsi huyu jamaa alivyopewa huu Ukonsul zaidi ya kuambiwa na Luyungu ambaye anadai amefanya kazi naye karibu sana na ana siri zake nyingi kuwa SABABU KUBWA NI UWEZO WAKE WA KIFEDHA NA URAFIKI WAKE NA WAKUU NA KWAMBA MATATIZO YAKE HAYAWEZI KUFANYIWA CHOCHOTE. Je hivi ndivyo vigezo vinajitosheleza vya ukonsul? In the actual fact rekebisho langu lilianza kwa kusema waziwazi kuwa,
Kwa kusema MZUNGU ana access ya siri za serikali, mjadala unaanza kukwepeshwa kwa kuuliza maswali kama vile je Mzungu hawezi kuwa raia wa Tanzania? na pili ni siri gani za serikali zinazotumwa Uholanzi n.k


NAKANDAMIZA KIBARA hoja zitililike kufuatana na mada. Mahojiano unayopendekeza yatakuwa mazuri sana tena sana lakini hebu tuyapange vizuri na siyo kudivert mjadala kutoka kwa Konsuli na huduma za Ukonsul Uholanzi kwenda kwa mtu mwingine yeyote. Ukitaka tuongelee mambo ya umoja wa Watanzania Uholanzi tuanzishe thread nyingine vinginevyo maelezo niliyoyatoa yalikuwa ni majibu ya maswali ya liyokuwa yameulizwa.

Wanaotakiwa kwenye masahili watakuwa kama ifuatavyo:

I. Konsuli mwenyewe: Aulizwe mahala ofisi yake ilipo na namna ya kufika hapo, alichaguliwaje au alipewaje hiyo tenda au ajira kivipi na mkataba wake ausome ulisainiwa na nani na ataendelea mpaka lini na majukumu ya kazi yake aliyopewa ni nini, uajibikaji wake uko chini ya nani (Ubalozi ulioko Ubelgiji au mambo ya ndani).
Je amewahi kutoa viza au la katika ofisi yake na ni za aina gani (muhuri au stika). Amtaje aliyemfanyia external auditing toka aanze kazi yake mpaka sasa na auditors and management report hizo za kila mwaka nani anazo( ubalozini na Mambo ya ndani) ili hao nao watuweke sawa kuonyesha kuwa Nabii ni mwongo maana taarifa hizo za ukaguzi zipo na kazi yake ni shwari. Aeleze mahusiano yake na Balozi au ofisi ya ubalozi -Ubelgiji. Akisena ni mzuri au mzuri sana aeleze kwa nini mara nyingi anapokutana na Watanzania katika sherehe Uholanzi huwa hamwaliki Balozi au sijui tuseme balozi hajialiki au kwa nini Balozi huwa mara nyingi huwa hayupo.Akisema mahusiano si mazuri sana aseme sababu.
Aulizwe je michango anayotoa kwa Watanzania hususan wakati wa sherehe hizo huwa anatoa mfukoni mwake au katika makusanyo ya mapato ya visa. Na ni nani (specific person au kamati) ambayo huwa inapitisha bajeti ya matumizi yake ikiwa ni pamoja na hayo matumizi.

II. Balozi Ubelgiji aulizwe kukanusha au kukubali juu ya yale Konsuli ameeleza (yanayohusiana na utumishi wake, uwajibikaji na reports na mahusiano yao).

III. Mambo ya ndani( dawati lenye dhamana ya eneo la Ulaya) waulizwe kama Balozi aliyeko Ubelgiji.


IV. Wateja wa huduma za Ukonsuli Uholanzi hawa si wengine bali ni mfano Wadachi wanaohangaika kupafikia mahala ofisi ilipo maana lazima uende na usafiri wako binafsi na Watanzania wengine hususani wanafunzi waulizwe hata zile salamu zake za kebehi za wasela wa vijiweni nao waseme kama huwa wanapenda kuitwa hivyo!!


Do this, you will either know Nabii is a R.Monger or you'll smell a rodent!
. Vinginevyo subilini tu maana tayari SYSYEM TAYARI INALIFANYIA KAZI JAMBO HILI.

Nasema kuwa watu walioeleza hadharani mwanzoni habari za ubadhilifu ndani ya BOT, watu lukuki walibaki kusema aha ndio za wapinzani hao, kwamba ni uzushi, na roho za korosho kama niitwavyo sasa. Leo ukweli uko barazani tunarudi kuwapongeza

Mie sipendi pongezi za leo wala kesho naomba tu kuwa makosa yarekebishwe na huduma za ukonsuli ziimarishwe. Kwanza kwa nini tusiwe na ubalozi kamili Uholanzi ukilinganisha na Ubelgiji?
 
JAMBO FORUM inaonekana tuna set the AGENDA halafu foreign wanafuata

inasemekana kuwa sasa wanaaangalia namna ya kupiga stop haya mamabo ya kuwapa WAZUNGU na mijitu isiyoeleweka access za siri za nchi

anyway sina hakika na hili lakini stay tuned


 
Hili ni kweli nimepata nyeti hizi na nimeweka mada yake tofauti kule juu .Issue ni kwamba hawa watu wanapewa nafasi hizi za uheshikiwa na Rais .Je nini itakuwa nafasi ya Foreign kwa rais na uteuzi wake ?
 
hizi nafasi inawezekana kuwa mabalozi wenyewe tu wanazitoa.

Japani niliwahi kukutana na mama mmoja anaitwa SHIMIZU mjapani, na aliponipatia busness card yake alikuwa imeandikwa ni honorary somebody to the embassy of Tanzania at the Kansi region.

sitegemei kama anafanya kazi yoyote ya maana zaidi ya kutengeneza fashion show za khanga na cultural exchange.

kwa maneno ya wenyeji wa Kansai, mama huyo ni nyumba ndogo wa balozi mtango
 
Badala ya watanzania kupoteza nauli zao kwenda kuweka fingure print kule brusell balozi ndogo inawasaidia kuchukua hizo data zao na kuzipeleka ktk balozi.
Wanabodi jamani twendeni kwa kituo kidogo ili nasi kina mbumbumbu ktk maswala haya tupate kuelewa vizuri.
Inakuwaje mzungu ambaye siii raia anapewa nguvu ya:-
1. Kukukusanya passport za watu (watalii) wanaotaka kuingia nchini Tanzania?...
2. Kutoa maagizo ama mapendekezo ya upatikanaji wa visa za kuingia Tanzania hali mtu huyu sii raia...
Na mengine mengi ambayo yanaweza kabisa kuwa na hatari ktk usalalma wa nchi yetu na pengine wizi mkubwa kufanyika kupitia watu kama hawa. Nitatoa mfano mmoja huyu mzungu naweza kuwa agent wa kampuni moja ya Utalii na kwa kupitia kampuni hiyo tu ndio watalii wanaweza kupata visa tena basi malipo yafanyike huko huko nje ktk kampuni ama account fulani...
Jamani tuwe makini sana na nchi yetu na mapenzi yetu yaanze kwa TANZANIA kabla hatujatetea mzungu, rais ama balozi yeyote kwani vitendo kama hivi pamoja na kuwa hawa jamaa ni wafanyabiashara tunaweza poteza mengi sana... Na yawezekana kutokana na vitu kama hivi ndio maana passport zetu rahisi sana kupigwa chapa na kuuzwa kwa wapopo (Wa Ghana na Wa Nigeria)..
 
mkuu mkandara maswali mazuri sana.
tatizo ni kwamba kutokuwa na ofisi kama hizo
itabidi wageni wahamasishwe kuchukua viza kwenye
kituo cha kuingilia (point of entry) au wazitume passpoti
zao kwa posta kwenda ubalozi unaoshughulikia nchi walizopo
au ofisi ya uhamiaji dar. sasa hii inamatatizo mengi ya
kiutendaji ndio maana ofisi hizo (consul) zinaweza saidia.

hata hivyo inabidi kuwe na umakini mkubwa katika kuteua
hao ma-consul. inabidi wafanyiwe uhakiki (vetted) ili
kuona kama wanaweza aminika. sasa kama hili halifanyiki
naamini basi system yetu inamatatizo.

aidha inabidi kuwepo na ufuatiliaji wa karibu wa
shughuli zao na sio kuachwa kufanyakazi kama ubalozi
mdogo. wakaguzi wa mahesabu wanabidi wawapitie
na kukagua vitabu vyao.

kuna mtu ameuliza hapo juu kwa nini hatufungui ubalozi uholanzi.
ubalozi uholanzi ulikuwepo lakini ulifungwa. huu ulikuwa kipindi
ambacho marehemu malima alikuwa waziri wa fedha. si uholanzi tuu balozi kadhaa zililengwa kufungwa wakati huo na ilibidi mambo ya nje wajenge hoja hasa kupunguza idadi ya balozi ambazo zililengwa kufungwa.
 
Shukran,
Hili swala tatizo lake kubwa nadhani ni pale limeingia rangi ya mtu lakini tukiondoa hiyo rangi na kulitazama kama hoja nadhani bado yapo maswali ambayo yanahitaji kupata jibu hasa kwa wale mnaofahamu utaratibu wa hizi Consul. najua fika kwamba hata Mzee Ally Sykes alikuwa consul wa Eretria nchini -Tanzania, sijui kama bado anaendelea na nafasi hiyo hadi leo. Hata hivyo basi kwa wale mnaofahamu vizuri swala hili nadhani itakuwa bora sana kama mtatueleza kwa lugha ya hoja badala ya kumshindilia madongo ndugu yetu maanake kuna sisi akina Yakhe nao tunapita watupu.... maanake nikiziangalia zile kazi za Consul nadhani hapo kunahitajika CV ya mtu pia mbali kabisa na Uraia wa mtu huyo. Elimu ktk fani hizo na pengine Kuielewa nchi unayoitumikia sio kwa kupitia darasani tu bali umewahi kuishi Tanzania na kuelewa baadhi ya mambo iwe Utamaduni, biashara ama mazingira kwani unaweza kuulizwa...
Kikubwa zaidi kulingana na hali ya Uhujumu uchumi unaotembea nchini hivi sasanadhani vipo vipengele ambavyo sisi mbumbumbu bado hatujapatiwa hoja inayojitosheleza maanake mimi sifahamu kama kweli uhakiki unafanyika na pia hii nafasi ya consul hutolewa kama part ya ku represent nchi kibiashara na wapi ukingo wa huduma zake.
 
Awali nakupongeza sana ndg. Game Theory kwa kuanzisha uzi huu hata hivyo mimi ningependekeza kuwa kichwa cha habari kingekuwa
ASIYE MTANZANIA NI KONSULA WA TANZANIA UHOLANZI maana kwa kusema MZUNGU ana access ya siri za serikali, mjadala unaanza kukwepeshwa kwa kuuliza maswali kama vile je Mzungu hawezi kuwa raia wa Tanzania? na pili ni siri gani za serikali zinazotumwa Uholanzi n.k

Pili ingawa haina maana yeyote kubwa, niseme kuwa hii hoja niliianzisha mimi katika uzi mwingine ambapo Lunyungu alikuwa anatutaarifu kupitia jukwaa hili la siasa katika kichwa cha habari Hatimaye JK kutinga Holland.
Aidha alitutaka tumwandikie maswali sirini ili ayatume kwa 'vijana'wake waje mamuulize JK. ndipo nilipotoka nyikani na sauti ya unabii nikisema, najinukuu;




Hakika hilo swali langu halikujibiwa, ingawa mwenzetu alijaribu kutoa maelezo ya kuongeza maswali zaidi badala ya majibu maana sasa aliibuka akionyesha kuwa hakuna linaloweza kufanyika maana eti jamaa kesha penya kwenye siasa zetu na rasilimali, ni mfanyabiashara mkubwa na hata JK anamtegemea kwa namna moja au nyingine.
Nilipoomba ufafanuzi wa kumtegemea kivipi sikujibiwa. Anyway leo baada ya hili kuleta kwa upya katika uzi wake wa kipeee naomba kusema yafuatayo. Kutoka katika vyanzo vyangu vifuatavyo:-

1. Mfanyabiashara Mdachi sasa,aliyekuwa Mtanzania kwa kuzaliwa na akiwa mtumishi wa serikali ya Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 90.
2. Mtanzania afanyaye ubalozi wa Tanzania Ubelgiji
3. wanafunzi watano wanaosoma au waliowahi soma hapo Uholanzi kupitia scholarship za NUFFIC

Ninataarifa za kuaminika kuhusu hili na ninatamka yafuatayo:-

1.Suala la yeye kuwa mfanya biashara mkubwa na Tanzania, na kuelewana au kuwa rafiki na wakubwa fulani silifahamu vizuri na wala kwangu si tija maana hakuna anayezuia Wakuu wa nchi kuwa na marafiki au kuzuia mtu kuwa rafiki ya mkuu wa nchi fulani so long as urafiki huo hauna maana ya kuleta ukiukaji au udhalimu wowote. Lakini,

2. Ni kweli kuna mwanaume asiye mtanzania afanyaye kazi kwa wadhifa wa Konsula kwa jina bwana F.J.Hakkenburg. Huyu jamaa ni Mdachi. Mara kwa mara akutanapo na kundi la Watanzania hujitahidi kuongea misimu na misamiati ya mitaani haijulikani kama huwa anafanya hivyo kwa kuipenda kweli lugha ya kiswahili toka rohoni au huwa ni mbinu yake ya kuzuga kadamnasi.

3.Ni kweli hatuna ubalozi Uholanzi, lakini ni nani anaweza kumwajiri (au kumpa kazi) mtu kuwa KONSULA WAKATI YEYE SI RAIA WA NCHI YETU TANZANIA? Eti kuna mtu humu alijitahidi kueleza kuwa hausika na mambo makubwa bali utamaduni (WA NANI SASA?) na biashara (KWA FAIDA YA NANI?). Huyu jamaa si kweli kuwa eti ana kazi ya kuwapa watu wajaze fomu kwa ajili ya visa tu, HAPANA, YEYE TOKA ZAMANI SANA AMEKUWA ANAKUSANYA FEDHA NA KUWAPA WATU WANAOTAKA VIZA HAPO HAPO OFISINI KWAKWE AMBAKO HAKIKA NI GEREJI NA DUKA KUBWA LA KUUZA NA KUNUNUA MAGARI YA FAMILIA YA VAN- VLIET (http://www.vanvliet.nl/). KWA MAANA NYINGINE HUYU JAMAA ANA MUHURI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANAOUGONGA KWENYE PASI ZOTE ZA KUSAFIRIA ZA WOTE WANAOKWENDA TANZANIA (kwa taarifa yenu Wadachi ni miongoni mwa watalii wengi katika vivutio vya nchi yangu Tz). YEYE ALIUTOA WAPI NA NI NANI ALIYEMKABIDHI NYENZO HIYO YA SERIKALI? LABDA KAMA AMEANZA HIVI KARIBUNI BAADA YA WATU KUANZA KUULIZA KICHINI CHINI, MIAKA YOTE AMEKUWA ANAWASILIANA MOJA KWA MOJA NA MAMBO YA NDANI DAR, JE NI NANI AMEKUWA ANAMKAGUA KUWA MAWASILISHO YOTE ANAYOKUSANYA NDIYO KWELI ANAYOWASILISHA? KWA NINI AMEKUWA HAWAJIBIKI CHINI YA UBALOZI WA UBELGIJI?

4. Kuna kero nyingine moja iliyowasilishwa na vyanzo vyangu (Wanafunzi). Ok, najua kila nchi Watanzania kwa jinsi wanavyojiorganise wenyewe ughaibuni, huwa wanaungana na wenzao Watanzania kwa kusherehekea pamoja siku mbalimbali za Kitaifa. Mara nyingi ubalozi huwa unahusika/husishwa kwa namna moja au nyingine. Sasa huko Uholanzi ni huyu Mdachi wala si ubalozi wa Ubelgiji wenye kauli wala kuhusika. Mara nyingi yeye humuita jamaa mmoja Mtanzania mdhamini wa Wabongonet.nl ambaye ni mwanachama mzuri wa hii net pia na humuagiza kuwa yeye anataka Watanzania washerehekee siku ipi, wapi na saa ngapi. Sasa huwa anampa taabu sana huyo jamaa maana watu unajua tena katika karne hii, tena wasomi huwa wanamchallenge sana huyo 'kiongozi' kuhusu hayo matangazo yake. Lakini niseme kuwa labda kwa sababu ya Ubalozi wetu kukaa kimya na kwa sababu huwa huyu Mdachi anatanguliza CHANGA LA MACHO KWAMBA YEYE NDIYE ATAGHARIMIA SEHEMU KUBWA YA GHARAMA ZA SHEREHE, basi watu wananywea tu na kuchanga Euro 10 hivi na wanakutana chini ya matakwa ya huyu Mdachi. Kama kuna mtu anabisha aeleze hapa kwa nini mfano alazimishe watu kusherekea NYERERE DAY pekee NA ISIWE UHURU DAY AU MUUNGANO DAY AU SIKU ZOTE HIZO NA ZINGINE ZA KITAIFA? Je ni lini Watanzania wa Uholanzi waliazimia iwe hiyo? Zaidi ya hapo huwa hata kwa kiburi chake anaamua KUTOMWALIKA BALOZI, Je mtu ataniambiaje kuwa anawajibika kwa Balozi???

5. Wanafunzi wasomao Uholanzi walisha wahi kuuliza kuwa 'je fedha anazochangia wakati wa sherehe ni kutoka mfukoni mwake kama Mdachi awapendaye Watanzania au ni mahesabu yanayowasilishwa baadaye (labda na mazidisho) kama matumizi ya ofisi yake kutoka makusanyo ya visa kwenye serikali yangu?' Swali hili yeye binafsi hakuwahi kulijibu. Yaani analikwepa, lakini mwakilishi wake (mdhamini wa Wabongonet.nl) aliwajibu kuwa, hakika hiyo huwa anaiweka kama bill ya matumizi ya ofisi yake na kuisukumiza huko Dar. SASA HAPO NDIO KUTAMU! JE NI NANI AMBAYE HUWA ANAMUIDHINISHIA BAJETI YAKE? MAANA HAWAJIBIKI UBALOZINI? NA ENDAPO SI FEDHA ZAKE KWA NINI SASA AWAAMLIE WATANZANIA KUSHEREHEKEA SIKU NA KWA STAILI YAKE (mfano masaa matatu tu na kufukuzwa ukumbini)? Nasema kuwa kama kuna mwenye majibu ya maswali haya ajibu humu wala hatuna haja ya kusubiri eti rais aje tumuulize maana mengine yanatuhusu sisi wenyewe si kila kitu ni cha JK!

Ndg. zangu ofisi hiyo na majukumu ya Hakkenburg kama mwakilishi wa Serikali yetu kamwe hayawezi pachikwa jina la usamaria mwema au eti anatoa usaidizi kwa sababu ya umaskini wetu wa kutokuwa na mtu wa kufanya kazi hiyo! Huu utakuwa uvivu wa kufikiri maana kwa nini mfano serikali isiruhusu hata mtu mmoja tu toka ubalozini Ubelgiji aje aishi uholanzi (hakuna tofauti kubwa) na afanye kazi hizo? Pili kama ni kusubcontract kazi fulani basi kwa nini kazi hiyo isingetangazwe na sifa ya kwanza iwe ni kuwa mhusika ni lazima awe Mtanzania? Mbona kuna Watanzania kibao ughaibuni wafanyabiashara kama yeyena wenye elimu nzuri ya diplomasia ya uchumi ambao wana uwezo wao tu lakini hawajigambi?

Afterall, kuna Watanzania wengi zaidi Uholanzi kuliko ubelgiji na pia Wadachi wamekuwa na mahusiano ya karibu kwa kutoa misaada mbalimbali kwa serikali yetu kuliko Ubelgiji na Wadachi ni miongoni mwa Watalii wengi Tanzania kuliko Wabelgiji, sasa kwa nini kama ni kubana matumizi Ubalozi usihamie Uholazi na Ubelgiji ndo wawe na Konsula MTANZANIA na si Mflemishi au sijui Mdachi?

SASA MWENYE KUPINGA HII HOJA AJE HAPA NA UTHIBITISHO MADHUBUTI KUWA HAKKENBURG NI MTANZANIA NA ALIPELEKWA ROTTERDAM KUPITIA UTARATIBU WA KAWAIDA WA KUSHIKIZWA (ATTACHEE)KUTOKEA UBALOZINI AU MAMBO YA NDANI NA HUWA ANAKAGULIWA SAWIA MAKUSANYO YA MAPATO TOKA VIZA ANAZOTOA!! VINGINEVYO HILI NI SUALA LA KUSAHIHISHA KOSA HILI MARA MOJA NA KUSONGA MBELE KAMA TUNATAKA KUWA NA MWAKA WA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA, UNABII TUNAOUTEGEMEA!

JIBU

BWANA NABII HAPA KADONDOKA. HEBU TUMRUDISHE SHULE ANGALAU KWA DAKIKA MOJA. UTAMADUNI WA MAKONSULA UMEJENGWA JUU YA SHERIA ZA KIAMTAIFA. SIO LAZIMA MTU AWE RAIA WA NCHI YAKO ILI AWE KONSULA WAKO. UTARATIBU NI KWAMBA NCHI YAWEZA KUMTEUA RAIA WA NCHI INAPOTAKA KUANZISHA UBALOZI MDOGO - CONSULATE - ILI KUWA CONSULA WAKE. HILI ULIE AMA UTEME MATE KIASI GANI NDIO UKWELI. HIVYO TUTAFUTE HOJA NYINGINE ZAIDI YA KWAMBA HUYO MTU SI RAIA WA KWETU. HILI SIO KOSA. YULE YONA ALIYEKUWA WAZIRI ALIWAHI KUWA CONSULA WA MAURITIUS KABLA HAJAINGIA SIASA.
 
JIBU

BWANA NABII HAPA KADONDOKA. HEBU TUMRUDISHE SHULE ANGALAU KWA DAKIKA MOJA. UTAMADUNI WA MAKONSULA UMEJENGWA JUU YA SHERIA ZA KIAMTAIFA. SIO LAZIMA MTU AWE RAIA WA NCHI YAKO ILI AWE KONSULA WAKO. UTARATIBU NI KWAMBA NCHI YAWEZA KUMTEUA RAIA WA NCHI INAPOTAKA KUANZISHA UBALOZI MDOGO - CONSULATE - ILI KUWA CONSULA WAKE. HILI ULIE AMA UTEME MATE KIASI GANI NDIO UKWELI. HIVYO TUTAFUTE HOJA NYINGINE ZAIDI YA KWAMBA HUYO MTU SI RAIA WA KWETU. HILI SIO KOSA. YULE YONA ALIYEKUWA WAZIRI ALIWAHI KUWA CONSULA WA MAURITIUS KABLA HAJAINGIA SIASA.



Mzee hapa tunazungumzia suala la NATIONAL SECURITY.Kwani kuna ugumu gani wa kuwapata maofisa waTanzania kufanya kazi hizo?
 
hizi nafasi inawezekana kuwa mabalozi wenyewe tu wanazitoa.

Japani niliwahi kukutana na mama mmoja anaitwa SHIMIZU mjapani, na aliponipatia busness card yake alikuwa imeandikwa ni honorary somebody to the embassy of Tanzania at the Kansi region.

sitegemei kama anafanya kazi yoyote ya maana zaidi ya kutengeneza fashion show za khanga na cultural exchange.

kwa maneno ya wenyeji wa Kansai, mama huyo ni nyumba ndogo wa balozi mtango

JF kwa umbeya!
Hii ndio ikampa accreditation?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom