Awali nakupongeza sana ndg. Game Theory kwa kuanzisha uzi huu hata hivyo mimi ningependekeza kuwa kichwa cha habari kingekuwa
ASIYE MTANZANIA NI KONSULA WA TANZANIA UHOLANZI maana kwa kusema
MZUNGU ana access ya siri za serikali, mjadala unaanza kukwepeshwa kwa kuuliza maswali kama vile je Mzungu hawezi kuwa raia wa Tanzania? na pili ni siri gani za serikali zinazotumwa Uholanzi n.k
Pili ingawa haina maana yeyote kubwa, niseme kuwa hii hoja niliianzisha mimi katika uzi mwingine ambapo Lunyungu alikuwa anatutaarifu kupitia jukwaa hili la siasa katika kichwa cha habari
Hatimaye JK kutinga Holland.
Aidha alitutaka tumwandikie maswali sirini ili ayatume kwa 'vijana'wake waje mamuulize JK. ndipo nilipotoka nyikani na sauti ya unabii nikisema, najinukuu;
HAKUNA HAJA YA KUTUMA SWALI HILI SIRINI NA KAMA YEYOTE ANASOMA HAPA NA YUKO KARIBU NA PREZO AU MAMBO YA NDANI AU UBALOZI (UBELGIJI) NAWASOGEZEA SWALI HILI AMBALO NDUGU ZANGU WA HUKO WANAULIZA KILA SIKU, LIULIZWE AU LISIULIZWE RAIS AJIANDAE KUWA NA MAJIBU AU MAELEZO YA SWALI LIFUATALO:
KWA NINI MSAIDIZI WA BALOZI (KONSULA) WA HUKO NETHERLANDS NI MDACHI BADALA YA KUWA MTANZANIA???? NA NI NANI ALIYEMTEUA NA ANAWAJIBIKA KWA NANI MAANA UBALOZI WA UBELGIJI HAUKO JUU YAKE.
Hakika hilo swali langu halikujibiwa, ingawa mwenzetu alijaribu kutoa maelezo ya kuongeza maswali zaidi badala ya majibu maana sasa aliibuka akionyesha kuwa hakuna linaloweza kufanyika maana eti
jamaa kesha penya kwenye siasa zetu na rasilimali, ni mfanyabiashara mkubwa na hata JK anamtegemea kwa namna moja au nyingine.
Nilipoomba ufafanuzi wa kumtegemea kivipi sikujibiwa. Anyway leo baada ya hili kuleta kwa upya katika uzi wake wa kipeee naomba kusema yafuatayo. Kutoka katika vyanzo vyangu vifuatavyo:-
1. Mfanyabiashara Mdachi sasa,aliyekuwa Mtanzania kwa kuzaliwa na akiwa mtumishi wa serikali ya Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 90.
2. Mtanzania afanyaye ubalozi wa Tanzania Ubelgiji
3. wanafunzi watano wanaosoma au waliowahi soma hapo Uholanzi kupitia scholarship za NUFFIC
Ninataarifa za kuaminika kuhusu hili na ninatamka yafuatayo:-
1.Suala la yeye kuwa mfanya biashara mkubwa na Tanzania, na kuelewana au kuwa rafiki na wakubwa fulani silifahamu vizuri na wala kwangu si tija maana hakuna anayezuia Wakuu wa nchi kuwa na marafiki au kuzuia mtu kuwa rafiki ya mkuu wa nchi fulani so long as urafiki huo hauna maana ya kuleta ukiukaji au udhalimu wowote. Lakini,
2. Ni kweli kuna mwanaume asiye mtanzania afanyaye kazi kwa wadhifa wa Konsula kwa jina bwana F.J.Hakkenburg. Huyu jamaa ni Mdachi. Mara kwa mara akutanapo na kundi la Watanzania hujitahidi kuongea misimu na misamiati ya mitaani haijulikani kama huwa anafanya hivyo kwa kuipenda kweli lugha ya kiswahili toka rohoni au huwa ni mbinu yake ya kuzuga kadamnasi.
3.Ni kweli hatuna ubalozi Uholanzi, lakini ni nani anaweza kumwajiri (au kumpa kazi) mtu kuwa KONSULA WAKATI YEYE SI RAIA WA NCHI YETU TANZANIA? Eti kuna mtu humu alijitahidi kueleza kuwa hausika na mambo makubwa bali utamaduni (WA NANI SASA?) na biashara (KWA FAIDA YA NANI?). Huyu jamaa si kweli kuwa eti ana kazi ya kuwapa watu wajaze fomu kwa ajili ya visa tu, HAPANA, YEYE TOKA ZAMANI SANA AMEKUWA ANAKUSANYA FEDHA NA KUWAPA WATU WANAOTAKA VIZA HAPO HAPO OFISINI KWAKWE AMBAKO HAKIKA NI GEREJI NA DUKA KUBWA LA KUUZA NA KUNUNUA MAGARI YA FAMILIA YA VAN- VLIET (
http://www.vanvliet.nl/). KWA MAANA NYINGINE HUYU JAMAA ANA MUHURI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANAOUGONGA KWENYE PASI ZOTE ZA KUSAFIRIA ZA WOTE WANAOKWENDA TANZANIA (kwa taarifa yenu Wadachi ni miongoni mwa watalii wengi katika vivutio vya nchi yangu Tz). YEYE ALIUTOA WAPI NA NI NANI ALIYEMKABIDHI NYENZO HIYO YA SERIKALI? LABDA KAMA AMEANZA HIVI KARIBUNI BAADA YA WATU KUANZA KUULIZA KICHINI CHINI, MIAKA YOTE AMEKUWA ANAWASILIANA MOJA KWA MOJA NA MAMBO YA NDANI DAR, JE NI NANI AMEKUWA ANAMKAGUA KUWA MAWASILISHO YOTE ANAYOKUSANYA NDIYO KWELI ANAYOWASILISHA? KWA NINI AMEKUWA HAWAJIBIKI CHINI YA UBALOZI WA UBELGIJI?
4. Kuna kero nyingine moja iliyowasilishwa na vyanzo vyangu (Wanafunzi). Ok, najua kila nchi Watanzania kwa jinsi wanavyojiorganise wenyewe ughaibuni, huwa wanaungana na wenzao Watanzania kwa kusherehekea pamoja siku mbalimbali za Kitaifa. Mara nyingi ubalozi huwa unahusika/husishwa kwa namna moja au nyingine. Sasa huko Uholanzi ni huyu Mdachi wala si ubalozi wa Ubelgiji wenye kauli wala kuhusika. Mara nyingi yeye humuita jamaa mmoja Mtanzania mdhamini wa Wabongonet.nl ambaye ni mwanachama mzuri wa hii net pia na humuagiza kuwa yeye anataka Watanzania washerehekee siku ipi, wapi na saa ngapi. Sasa huwa anampa taabu sana huyo jamaa maana watu unajua tena katika karne hii, tena wasomi huwa wanamchallenge sana huyo 'kiongozi' kuhusu hayo matangazo yake. Lakini niseme kuwa labda kwa sababu ya Ubalozi wetu kukaa kimya na kwa sababu huwa huyu Mdachi anatanguliza CHANGA LA MACHO KWAMBA YEYE NDIYE ATAGHARIMIA SEHEMU KUBWA YA GHARAMA ZA SHEREHE, basi watu wananywea tu na kuchanga Euro 10 hivi na wanakutana chini ya matakwa ya huyu Mdachi. Kama kuna mtu anabisha aeleze hapa kwa nini mfano alazimishe watu kusherekea NYERERE DAY pekee NA ISIWE UHURU DAY AU MUUNGANO DAY AU SIKU ZOTE HIZO NA ZINGINE ZA KITAIFA? Je ni lini Watanzania wa Uholanzi waliazimia iwe hiyo? Zaidi ya hapo huwa hata kwa kiburi chake anaamua KUTOMWALIKA BALOZI, Je mtu ataniambiaje kuwa anawajibika kwa Balozi???
5. Wanafunzi wasomao Uholanzi walisha wahi kuuliza kuwa 'je fedha anazochangia wakati wa sherehe ni kutoka mfukoni mwake kama Mdachi awapendaye Watanzania au ni mahesabu yanayowasilishwa baadaye (labda na mazidisho) kama matumizi ya ofisi yake kutoka makusanyo ya visa kwenye serikali yangu?' Swali hili yeye binafsi hakuwahi kulijibu. Yaani analikwepa, lakini mwakilishi wake (mdhamini wa Wabongonet.nl) aliwajibu kuwa, hakika hiyo huwa anaiweka kama bill ya matumizi ya ofisi yake na kuisukumiza huko Dar. SASA HAPO NDIO KUTAMU! JE NI NANI AMBAYE HUWA ANAMUIDHINISHIA BAJETI YAKE? MAANA HAWAJIBIKI UBALOZINI? NA ENDAPO SI FEDHA ZAKE KWA NINI SASA AWAAMLIE WATANZANIA KUSHEREHEKEA SIKU NA KWA STAILI YAKE (mfano masaa matatu tu na kufukuzwa ukumbini)? Nasema kuwa kama kuna mwenye majibu ya maswali haya ajibu humu wala hatuna haja ya kusubiri eti rais aje tumuulize maana mengine yanatuhusu sisi wenyewe si kila kitu ni cha JK!
Ndg. zangu ofisi hiyo na majukumu ya Hakkenburg kama mwakilishi wa Serikali yetu kamwe hayawezi pachikwa jina la usamaria mwema au eti anatoa usaidizi kwa sababu ya umaskini wetu wa kutokuwa na mtu wa kufanya kazi hiyo! Huu utakuwa uvivu wa kufikiri maana kwa nini mfano serikali isiruhusu hata mtu mmoja tu toka ubalozini Ubelgiji aje aishi uholanzi (hakuna tofauti kubwa) na afanye kazi hizo? Pili kama ni kusubcontract kazi fulani basi kwa nini kazi hiyo isingetangazwe na sifa ya kwanza iwe ni kuwa mhusika ni lazima awe Mtanzania? Mbona kuna Watanzania kibao ughaibuni wafanyabiashara kama yeyena wenye elimu nzuri ya diplomasia ya uchumi ambao wana uwezo wao tu lakini hawajigambi?
Afterall, kuna Watanzania wengi zaidi Uholanzi kuliko ubelgiji na pia Wadachi wamekuwa na mahusiano ya karibu kwa kutoa misaada mbalimbali kwa serikali yetu kuliko Ubelgiji na Wadachi ni miongoni mwa Watalii wengi Tanzania kuliko Wabelgiji, sasa kwa nini kama ni kubana matumizi Ubalozi usihamie Uholazi na Ubelgiji ndo wawe na Konsula MTANZANIA na si Mflemishi au sijui Mdachi?
SASA MWENYE KUPINGA HII HOJA AJE HAPA NA UTHIBITISHO MADHUBUTI KUWA HAKKENBURG NI MTANZANIA NA ALIPELEKWA ROTTERDAM KUPITIA UTARATIBU WA KAWAIDA WA KUSHIKIZWA (ATTACHEE)KUTOKEA UBALOZINI AU MAMBO YA NDANI NA HUWA ANAKAGULIWA SAWIA MAKUSANYO YA MAPATO TOKA VIZA ANAZOTOA!! VINGINEVYO HILI NI SUALA LA KUSAHIHISHA KOSA HILI MARA MOJA NA KUSONGA MBELE KAMA TUNATAKA KUWA NA MWAKA WA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA, UNABII TUNAOUTEGEMEA!