Mzee Machano: Nilikuwa nafungwa kila ikikaribia maadhimisho ya sikukuu ya Mapinduzi

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,949

Lambart Stanislaus mtangazaji wa Dar24 Media akiwa Mombasa Zanzibar alimuhoji Mzee Muchano Hamis Ally kuhusu Sakata la yeye kufungwa kila maadhimisho sikuu za Mapinduzi zinapokaribia.

Lambart: Tuambie hasa wewe ni nani tangu enzi zile za Afro Shiraz

Mzee Machano: Mimi ni Machano Hamis Ally kwenye Afro Shiraz nilikuwa Youth na nilikuwa miongoni mwa vijana wanaharakati mpaka Mapinduzi ya 1964. Baada ya Mapinduzi nilipewa kazi katika Idara ya Usalama wa Taifa mpaka mwaka 1969.

Lambart: Ulikuwa na cheo gani ndani ya usalama wa Taifa?

Mzee Machano: Vyeo vyao nimevisahau lakini nilikuwa mtu wa kawaida tu. Nikaondolewa Usalama wa Taifa nikapelekwa polisi kuanzisha Usalama wa Taifa ndani ya polisi kama Sejant Major mpaka nikafikia cheo cha Kamisaa Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Cheo cha kisiasa.

Kama nilivyokwambia cheo change kilikuwa cha kisiasa niliruhusiwa kuingia kwenye Sias ana wkati huo huo nikigombea nafasi kwenye Baraza la Wawakilishi. Na wakati ule Uwakilishi haukuwa Jimbo kwa Jimbo ulikuwa Uwakilishi wa watu maalumu wanateuliwa na kupigiwa kura kupitia humuhumu kwenye Baraza.

Kwahiyo mimi nikachaguliwa kuwa Mbunge, katika Ubunge wangu huo kwa tiketi la Baraza la Wawakilishi.

Lambart: Wakati huo ilikuwa bado unavaa magwanda? Yaani Mbunge lakini bado ni Polisi?

Mzee Machano: Ndiyo, nikiwa kwenye shughuli za Kibunge sivai gwanda kwingine huko navaa gwanda. Tumekwenda mpaka ikafikia vuguvugu la kuanzishwa kwa Vyama Vingi vya Siasa. Tanzania ilikubali kuingia kwenye vyama vingi vya siasa. Sisi pia katika jeshi tuliruhusiwa kuingia katika siasa.

Lambart: Wakati mapinduzi yanafanyika wewe ulikuwa kijana, ulikuwa unaziona siasa na harakati zinavyoenda. Kwa unavyofahamu, Waasisi wa Mapinduzi wenyewe dhamira yao ilikuwa ni nini hasa?

Dhamira ya Mapinduzi ni kukomboa watu wote kuwa katika Maisha bora bila ubaguzi, hiyo ndo dhamira yao kubwa

Lambart: Hivi karibuni Rais Samia amesikika akisema tuache mapinuzi ya kisiasa pekee, tuyahamishie Mapinduzi hayo kwenye Uchumi na Maendeleo. Nini mtazamo wako kuhusu kauli hii

Mzee Machano: Mimi nakubaliana naye lakini ni maneno hayo kwa sababu suala la maendeleo na kuacha mambo ya kubaguana hayakuanza jana na leo. Toka kipindi cha Karume alilenga kuwaweka watu pamoja. Na alitaka kusiwe na uchaguzi mpaka ipite miaka 50 ili watu wawe kitu kimoja. Sasa nia hiyo ilikuwa akilini mwake na aliamua hivyo lakini miongoni mwa watu wake hawaamini lugha wala utaratibu huo.

Lambart: Kwanini unasema hivyo?
 
Kama kweli sio chai uyu mzee kweli alkua usalama, basi USALAMA imekua taasisi ya ovyo tangu enzi na enzi
Kama usalama kuna vichaa unashangaa nini? Kama usalama kuna magaidi unadhangaa nini, kama usalama kuna majambazi unadhangaa nini?
 
Back
Top Bottom