Hongera CCM: Umelijenga Taifa imara Kwa vizazi vijavyo

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Leo Tanzania ni Mwalimu katika mambo mengi, inaaminiwa katika mengi na inatambulika Kwa mengi sio tu Afrika bali duniani Kwa ujumla. Licha ya kwamba wanasema Nabii hakubaliki kwao lakini anayeifanya Tanzania kuwa hivi alivyo Leo ni Nabii anayekubalika ndio maana nataka hongera kwake, HONGERA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Hongera CCM mwanamapinduzi wa kweli kwenye uchumi,siasa na maendeleo. Bila CCM pengine Tanzania tuliyonayo ingekuwa ni historia. Unaamini uchumi bora na maendeleo na siasa safi yanaletwa na utulivu na umoja na msingi huo umetusaidia kujenga na kuleta Mapinduzi makubwa ya kimaendeleo. Hakika wewe ni Chama Cha Mapinduzi.

Hongera CCM, Umetusaidia kuonesha njia ya kutokuwa na Tamaa ya madaraka kwa viongozi, tunajivunia Hilo. Tangu awamu wa ya kwanza mpaka sasa hatujasikia wala kusimuliwa kwamba Kuna kiongozi aliyewahi kugoma kutoka madarakani na umekuwa mstari wa mbele kutukumbusha falsafa ya kuachiana vijiti vya uongozi.

Hongera CCM, mpaka sasa umetupatia wenyeviti 6 ,ambao wameomesha dhamira ya dhati katika utumishi na uongozi. Viongozi mashujaaa wenye kiu ya kulibadilisha Taifa na kuwa kielelezo Cha demokrasia duniani.

Hongera CCM, busara na hekima zako za uongozi zimevuka mipaka na bahari na kama Afrika Leo ingekuwa nchi ninaamini Bado ungekuwa ni Chama tawala.

Hongera CCM, Mwalimu bora wa wakati wote wa siasa safi, demokrasia ,uhuru wa kutoa maoni , uvumilivu na mageuzi ya kiuchumi. Bila wewe hivi vitu vingekuwa ni anasa kwenye maisha ya watanzania.

Hongera CCM, kutupatia Rais Samia ambaye ni nembo ya mabadiliko ya kisera Kwa Taifa letu katika karne ya 21. Tanzania inajivunia wewe.

Hongera sana CCM ,wewe ni zawadi bora katika vifurushi vya zawadi walizozawadiwa watanzania.HONGERA CCM
 
I see
1. Taifa imara halina umeme

2. Taifa imara halina maji

3. Taifa imara halina SUKARI

4. Taifa imara dollar hamna ukiipata ni 3,000

4. Taifa imara wezi wa pesa za umma

5. Taifa imara la mafisadi

6. Waziri mkubwa mkubwa muongi.

7. Chama chenye mwenezi mtekaji na mvamizi cc. Clouds
 
Mnafaidika nini kubadilisha ukweli kuwa uongo?
Hakuna kazi ngumu kama kubadili uongo kuwa ukweli na matokeo yake mara nyingi sio zote anayefanya hivyo anaweza kuumbuka lakini Kwa hongera hii Kwa CCM ,ni ya kweli, ya dhati na ya kheri.
 
Mwongo we !
Siku moja kaa chini kama nusu saa ,itafakari historia ya nchi yetu na mwisho jaribu kilichofanikisha historia hiyo najua hutotamani mawazo ya CCM yaingie akilini mwako lakini ndio ukweli ,historia ya nchi hii haijajiumba wala kujitengeneza bali imetengenezwa na CCM .
 
Leo Tanzania ni Mwalimu katika mambo mengi, inaaminiwa katika mengi na inatambulika Kwa mengi sio tu Afrika bali duniani Kwa ujumla. Licha ya kwamba wanasema Nabii hakubaliki kwao lakini anayeifanya Tanzania kuwa hivi alivyo Leo ni Nabii anayekubalika ndio maana nataka hongera kwake, HONGERA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Hongera CCM mwanamapinduzi wa kweli kwenye uchumi,siasa na maendeleo. Bila CCM pengine Tanzania tuliyonayo ingekuwa ni historia. Unaamini uchumi bora na maendeleo na siasa safi yanaletwa na utulivu na umoja na msingi huo umetusaidia kujenga na kuleta Mapinduzi makubwa ya kimaendeleo. Hakika wewe ni Chama Cha Mapinduzi.

Hongera CCM, Umetusaidia kuonesha njia ya kutokuwa na Tamaa ya madaraka kwa viongozi, tunajivunia Hilo. Tangu awamu wa ya kwanza mpaka sasa hatujasikia wala kusimuliwa kwamba Kuna kiongozi aliyewahi kugoma kutoka madarakani na umekuwa mstari wa mbele kutukumbusha falsafa ya kuachiana vijiti vya uongozi.

Hongera CCM, mpaka sasa umetupatia wenyeviti 6 ,ambao wameomesha dhamira ya dhati katika utumishi na uongozi. Viongozi mashujaaa wenye kiu ya kulibadilisha Taifa na kuwa kielelezo Cha demokrasia duniani.

Hongera CCM, busara na hekima zako za uongozi zimevuka mipaka na bahari na kama Afrika Leo ingekuwa nchi ninaamini Bado ungekuwa ni Chama tawala.

Hongera CCM, Mwalimu bora wa wakati wote wa siasa safi, demokrasia ,uhuru wa kutoa maoni , uvumilivu na mageuzi ya kiuchumi. Bila wewe hivi vitu vingekuwa ni anasa kwenye maisha ya watanzania.

Hongera CCM, kutupatia Rais Samia ambaye ni nembo ya mabadiliko ya kisera Kwa Taifa letu katika karne ya 21. Tanzania inajivunia wewe.

Hongera sana CCM ,wewe ni zawadi bora katika vifurushi vya zawadi walizozawadiwa watanzania.HONGERA CCM
Umesahau kuweka number ya simu na jina kamili.
 
.....unemployment rate 36%,uimara huu upo wapi?,ujinga, umasikini, maradhi na rushwa ya hali ya juu imetamalaki nchini, mtoa mada pls orodhesha hapa nini serikali ya ccm imeifanyia nchi yangu
 
Kwakweli haina budi tuipongeze CCM imetutoa mbali, ila yote na yote ashukuriwe aliye juu maana kuna wengine hawana kabisa hata amani ktk nchi zao
 
Huwa nikisoma nyuzi za aina hii,huwa nabaki nacheka tu.Tanzania ni taifa la kawaida sana hapa duniani halina maajabu yoyote ya kushangaza Ulimwengu huu.

Kukosa exposure kwa Watanzania wengi kumefanya wawe wajinga ndio maana Wana hofia hata kitaifa kidogo kama Rwanda
 
I see
1. Taifa imara halina umeme

2. Taifa imara halina maji

3. Taifa imara halina SUKARI

4. Taifa imara dollar hamna ukiipata ni 3,000

4. Taifa imara wezi wa pesa za umma

5. Taifa imara la mafisadi

6. Waziri mkubwa mkubwa muongi.

7. Chama chenye mwenezi mtekaji na mvamizi cc. Clouds
Bado nasisitiza tena na tena,historia itatuhukumu kama tusipoweka jitihada za kuijua. Katika salamu zake kwenye msiba wa Mzee Mwinyi, Waziri mkuu mstaafu Jaji Warioba amenukuliwa akisema ' wakati mzee mwinyi anaingia madarakali hali ilikuwa mbaya kuliko Sasa kwenye lakini tukavuka'

Kauli hiyo inatukumbusha nyakati ngumu hazidumu milele na Kuna siku zinapotea kabisa. Mfano, Leo hii Marekani inazungumzwa kama Taifa lenye demokrasia kubwa duniani lakini historia inatukumbusha kwamba hapo nyuma mtu mweusi aliteseka Sana.

Kuna kipindi wakati ni ukuta lakini pia Kuna kipindi wakati ni funzo. Ninaamini, Kuanzia Sasa kama vile Marekani ilipobadili wakati kuwa funzo hivyo na Tanzania itafanya hivyo.
 
Kwakweli haina budi tuipongeze CCM imetutoa mbali, ila yote na yote ashukuriwe aliye juu maana kuna wengine hawana kabisa hata amani ktk nchi zao
Umenena kweli, msingi wa maendeleo sio Kasi ya kushindana na wengine katika maendeleo, kwamba Kenya , Marekani imefanya vile na sisi tufanye hivi bali ni amani ,umoja na utulivu. Tuipe Hongera CCM Kwa kutujenga katika msingi huu
 
Nchi nyingi duniani hakuna kitu kinachoitwa kumwachia Mungu bali hupigania haki zao mwanzo mwisho tofauti na hapa kwetu wengi wanaoitwa wanyonge haki zai zikiporwa wao huishia kumwachia Mungu na hiki ndicho kinaifanya CCM ibakie madarakani.

Viongozi wengi wa Afrika wanatamani wangekuwa wanaongoza wanyonge kama Watanzania.
 
Leo Tanzania ni Mwalimu katika mambo mengi, inaaminiwa katika mengi na inatambulika Kwa mengi sio tu Afrika bali duniani Kwa ujumla. Licha ya kwamba wanasema Nabii hakubaliki kwao lakini anayeifanya Tanzania kuwa hivi alivyo Leo ni Nabii anayekubalika ndio maana nataka hongera kwake, HONGERA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Hongera CCM mwanamapinduzi wa kweli kwenye uchumi,siasa na maendeleo. Bila CCM pengine Tanzania tuliyonayo ingekuwa ni historia. Unaamini uchumi bora na maendeleo na siasa safi yanaletwa na utulivu na umoja na msingi huo umetusaidia kujenga na kuleta Mapinduzi makubwa ya kimaendeleo. Hakika wewe ni Chama Cha Mapinduzi.

Hongera CCM, Umetusaidia kuonesha njia ya kutokuwa na Tamaa ya madaraka kwa viongozi, tunajivunia Hilo. Tangu awamu wa ya kwanza mpaka sasa hatujasikia wala kusimuliwa kwamba Kuna kiongozi aliyewahi kugoma kutoka madarakani na umekuwa mstari wa mbele kutukumbusha falsafa ya kuachiana vijiti vya uongozi.

Hongera CCM, mpaka sasa umetupatia wenyeviti 6 ,ambao wameomesha dhamira ya dhati katika utumishi na uongozi. Viongozi mashujaaa wenye kiu ya kulibadilisha Taifa na kuwa kielelezo Cha demokrasia duniani.

Hongera CCM, busara na hekima zako za uongozi zimevuka mipaka na bahari na kama Afrika Leo ingekuwa nchi ninaamini Bado ungekuwa ni Chama tawala.

Hongera CCM, Mwalimu bora wa wakati wote wa siasa safi, demokrasia ,uhuru wa kutoa maoni , uvumilivu na mageuzi ya kiuchumi. Bila wewe hivi vitu vingekuwa ni anasa kwenye maisha ya watanzania.

Hongera CCM, kutupatia Rais Samia ambaye ni nembo ya mabadiliko ya kisera Kwa Taifa letu katika karne ya 21. Tanzania inajivunia wewe.

Hongera sana CCM ,wewe ni zawadi bora katika vifurushi vya zawadi walizozawadiwa watanzania.HONGERA CCM
Umesahau kuweka namba zako kama yule Mwanani
 
Huwa nikisoma nyuzi za aina hii,huwa nabaki nacheka tu.Tanzania ni taifa la kawaida sana hapa duniani halina maajabu yoyote ya kushangaza Ulimwengu huu.

Kukosa exposure kwa Watanzania wengi kumefanya wawe wajinga ndio maana Wana hofia hata kitaifa kidogo kama Rwanda
Hakuna kitu nakishangaa kama mtu kuifanisha Tanzania na nchi kama Rwanda ,nchi ambayo inalingana ukubwa na Mkoa wa Tanga.

Tanzania ni kubwa Kwa Kila kitu kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati ,ukiachana na Congo na Ethiopia lakini kabla Tanzania ilikuwa kubwa sana.

Tanzania ni nchi yenye watu wengi sana katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Bado Kuna utulivu na amani. Kaa chini utafakari wingi wa watu unavyoweza kuwa ni tishio la usalama lakini Tanzania hakuna tishio Hilo. Tuipe Hongera CCM.

Katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ni Tanzania yenye makabila mengi sana na Bado mpaka sasa hatujasikia ukabila ukiwa ni agenda ya kisiasa.

Ardhi ya Tanzania ni kubwa sana na nyingi ni mapori makubwa lakini hatujasikia uwepo vikundi vya kujitoa mhanga vya maporini kama kule Congo.

Tanzania ingekuwa kama Rwanda Leo hii Tanzania ingekuwa ni nchi iliyoendelea Kwa sababu mabadiliko ya uongozi ni kichocheo kwenye maendeleo.

Demokrasia ya Tanzania ni kama ya mambele huko, na tunaweza kuwa tumezizidi nchi za mambele kwenye eneo hili
 
Nchi nyingi duniani hakuna kitu kinachoitwa kumwachia Mungu bali hupigania haki zao mwanzo mwisho tofauti na hapa kwetu wengi wanaoitwa wanyonge haki zai zikiporwa wao huishia kumwachia Mungu na hiki ndicho kinaifanya CCM ibakie madarakani.

Viongozi wengi wa Afrika wanatamani wangekuwa wanaongoza wanyonge kama Watanzania.
Kama unafikiri CCM inaendelea kutawala Kwa sababu ya unyonge wa watu basi mtazamo wako hauko sahihi. Ni kweli haki inapiganiwa inapoporwa lakini CCM haijawahi kupora haki ya yeyote ndio maana huwezi kuona watu wakizipigania.
 
Hongera CCM, Mwalimu bora wa wakati wote wa siasa safi, demokrasia ,uhuru wa kutoa maoni , uvumilivu na mageuzi ya kiuchumi. Bila wewe hivi vitu vingekuwa ni anasa kwenye maisha ya watanzania.
ccm hii hii inayong'ang'ania kukaa madarakani kwa gilba, hila, utapeli na wizi wa kura kinyume na matakwa ya umma?!!!
 
Back
Top Bottom