Mzee Kikwete, kama hamtaki Dini Kuchanganywa na Siasa mbona CCM na Serikali mnawatumia Kimaombi katika Shughuli zenu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,117
GENTAMYCINE sijawahi kuona Shughuli yoyote ile ya Kiserikali na hata ya Chama Tawala CCM ambayo huwa haiwatumii Viongozi wa Dini Kimaombi / Dua.

Leo hii namshangaa kumuona Mtu ambaye aliharibu kwa kiasi Kikubwa Misingi imara ya nchi (Rais Mstaafu Kikwete) kwa tabia yake ile ile ya Unafiki akijifanya Kukemea Udini Tanzania (kwa kujificha) akiwalenga TEC ambao Ngumi yao Moja tu ya 'Ndoige Katoliki' imewaingia vilivyo Usoni mwao Mafisadi na Majambazi wa Rasilimali za Tanzania na sasa wanatapatapa tu.

Kikwete (Rais Mstaafu) kama kweli hutaki / hupendi Dini Kuchanganywa na Siasa basi nakuomba anza Kwanza kuwaambia wana CCM Wenzako (hasa Mwenyekiti wako Taifa na Rais Samia) wasiwe kamwe Wanawaalika Viongozi wa Dini kuja Kuombea Matamasha yenu (Hafla zenu) za Kichama na Serikali bali muwe mnajiombea tu Wenyewe kwani kuwaita hawa Viongozi wa Dini huko ni Kuchanganya Siasa / Utendaji na Dini.

Nakushauri tu Kikwete acha kutumika na Mama (Mwenyekiti wako Taifa) ili umsaidie katika hili baada ya kuona Chawa wake Ngumi Kali ya 'Ndoige Katoliki' ya TEC imewaingia vilivyo na wameshindwa kuzitetea Hoja Kali za TEC.

TEC wameshamaliza hivyo msitusumbue na Maunafiki yenu. Tena Wengine ndiyo mna Dhambi nyingi tu mmewafanyia Watanzania kwa Kuwaibia Pesa zao na Kuzificha Benki za Cyprus (kwa Kuogopa mkizificha Uswisi zitarejeshwa kiurahisi kwa Watanzania mliowaibia) huku mkijilimbikizia Mali kem kem halafu leo mnajifanya ni Watu Safi, mnajitokeza Kukemea Mambo mkiamini kuwa bado mnapendwa na Watanzania wakati ni Kinyume chake.

Yaani Viongozi wa Dini wakiwa Wanakubali mialiko yenu mkiwaita au wakiwa Wanawasifia au Kukisifia chama Tawala CCM huwa ni wazuri Kwenu na huwa hawachanganyi Dini na Siasa ila Viongozi hawa hawa wa Dini Wakiwakosoa tu kwa Maupuuzi yenu, Dhambi zenu na Upumbavu wenu mnawageuka na kuwaona ni Wabaya, Maadui na Wanachanganya Dini na Siasa huku hadi mkiwatishia na Wengine.

Halafu GENTAMYCINE akiwa Anawaambia hamna Akili mnakasirika na kudhani kuwa anawaonea tu wakati Kiuhalisia huwa anakuwa sahihi.

Naungana na TEC 100% kwa Tamko!
 
Naunga Mkono Hoja.

Sisi Kanisa Moja Takatifu Katoliki La Mitume hutoa Mashauri ya Enjili pamoja na Mashauri ya Siasa.

Issa Al Masih aliwahi kuulizwa kutoa fafanuzi za Kisiasa na aliweza kujibu vizuri tuu.

Sisi Kanisa Moja Takatifu Katoliki la Mitume Tumepinga Haya makubaliano ya kitapeli Yenye bhalagha ndani yake.

Sis Kanisa Moja Takatifu Katoliki la Mitume Tumekataa na tutaendelea kukataa Rasilimali Zetu Watanzania Kuibwa.

Uje Roho Mtakatifu...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom