Mzee Kikwete, kama hamtaki Dini Kuchanganywa na Siasa mbona CCM na Serikali mnawatumia Kimaombi katika Shughuli zenu?

Mzee aliharibu nchi kwa ufisadi yule hadi uchaguzi wa 2015 wakaamua waandike chagua magufuli na sio Ccm ..wanaosema nchi inaendeshwa kutoka msoga unadhani walikosea? Huyu mzee sijui anataka nini kama mabilioni alishabeba sana yaani hata hivi vichache vilivyopo bado ana uchu navyo...kifo cha nwendazake ni vile akijachunguzwa vizuri tu...
 
Kwenye mialiko viongozi wa dini wanapewa fedha kama asante sana na sadaka na pia wakiitwa alafu wasitokee ni dharau ukikubaliana na viongozi hapo hujachanganya dini na siasa bali ukikinzana ukatofautiana na viongozi hapo tayari umesha changanya dini na siasa. Sarikali ijikite na kkkt pamoja na bakwata hawa tek wamekataa na wana dharau Wakuu

Wamekosea sana kuchanganya dini na siasa Kikwete yupo sahihi hawa askofu wachukuliwe hatua kali za kisheria kwa kuvunja uhuru wa kuabudu. Kwani watu wote tunapinga hapana utasemaje sauti yenu ndiyo ya Mungu wakati mimi nataka bandari iondoke wakabidhiwe wawekezaji waarabu kwani kosa lipo wapi mbona wananunua tumu za mipira na bado mnazishangilia waache wanunue na bandari mshangiliee kama wafuasi wa man city
 
GENTAMYCINE sijawahi kuona Shughuli yoyote ile ya Kiserikali na hata ya Chama Tawala CCM ambayo huwa haiwatumii Viongozi wa Dini Kimaombi / Dua.

Leo hii namshangaa kumuona Mtu ambaye aliharibu kwa kiasi Kikubwa Misingi imara ya nchi (Rais Mstaafu Kikwete) kwa tabia yake ile ile ya Unafiki akijifanya Kukemea Udini Tanzania (kwa kujificha) akiwalenga TEC ambao Ngumi yao Moja tu ya 'Ndoige Katoliki' imewaingia vilivyo Usoni mwao Mafisadi na Majambazi wa Rasilimali za Tanzania na sasa wanatapatapa tu.

Kikwete (Rais Mstaafu) kama kweli hutaki / hupendi Dini Kuchanganywa na Siasa basi nakuomba anza Kwanza kuwaambia wana CCM Wenzako (hasa Mwenyekiti wako Taifa na Rais Samia) wasiwe kamwe Wanawaalika Viongozi wa Dini kuja Kuombea Matamasha yenu (Hafla zenu) za Kichama na Serikali bali muwe mnajiombea tu Wenyewe kwani kuwaita hawa Viongozi wa Dini huko ni Kuchanganya Siasa / Utendaji na Dini.

Nakushauri tu Kikwete acha kutumika na Mama (Mwenyekiti wako Taifa) ili umsaidie katika hili baada ya kuona Chawa wake Ngumi Kali ya 'Ndoige Katoliki' ya TEC imewaingia vilivyo na wameshindwa kuzitetea Hoja Kali za TEC.

TEC wameshamaliza hivyo msitusumbue na Maunafiki yenu. Tena Wengine ndiyo mna Dhambi nyingi tu mmewafanyia Watanzania kwa Kuwaibia Pesa zao na Kuzificha Benki za Cyprus (kwa Kuogopa mkizificha Uswisi zitarejeshwa kiurahisi kwa Watanzania mliowaibia) huku mkijilimbikizia Mali kem kem halafu leo mnajifanya ni Watu Safi, mnajitokeza Kukemea Mambo mkiamini kuwa bado mnapendwa na Watanzania wakati ni Kinyume chake.

Yaani Viongozi wa Dini wakiwa Wanakubali mialiko yenu mkiwaita au wakiwa Wanawasifia au Kukisifia chama Tawala CCM huwa ni wazuri Kwenu na huwa hawachanganyi Dini na Siasa ila Viongozi hawa hawa wa Dini Wakiwakosoa tu kwa Maupuuzi yenu, Dhambi zenu na Upumbavu wenu mnawageuka na kuwaona ni Wabaya, Maadui na Wanachanganya Dini na Siasa huku hadi mkiwatishia na Wengine.

Halafu GENTAMYCINE akiwa Anawaambia hamna Akili mnakasirika na kudhani kuwa anawaonea tu wakati Kiuhalisia huwa anakuwa sahihi.

Naungana na TEC 100% kwa Tamko!
Yale maombi ya watishi kwenye mikutano ya ccm huwa ni zuga tu.

Mafisadi hawa Mungu wamjulie wapi?
 
Tena alienda kwa Wasabato kabisa... Ambao hawali kitimoto kama yeye....
kwa kuhudhuria shughuli ya wasabato, nao watajitoa ufahamu wasijue mapungufu ya mkataba wa bandari watakaa kimya au kuwapinga TEC. Pro mkataba wanatafuta vikundi vya kipuuzi na wapuuzi waungwe mkono is too late, nakoz za TEC zimewaingia hawachomoi hoja
 
Back
Top Bottom