Taasisi ya Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Foundation) imeandaa mkutano wa mazungumzo kuhusu amani, umoja, haki na maendeleo ya watu, mkutano unaotarajiwa kufanyika Alhamisi ya Januari 22 mwaka huu (2026)
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu Januari 19.2025, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Waryoba Butiku amesema mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi mkubwa wa mikutano wa taasisi hiyo uliopo Posta, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 03 asubuhi, unalenga kutoa nafasi kwa wazee kujadili na kutoa maoni kuhusu misingi iliyoundwa na kudumisha Taifa la Tanzania kuwa nchi ya amani, umoja, haki na yenye matumaini ya maendeleo endelevu ya watu
"Washiriki katika mkutano huu ni wazee katika maana pana ya watu wenye hekima na busara kutoka kwenye makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi wa Dini, wasomi, wazee wastaafu, wanawake, vijana, vyama vya siasa, Tasnia ya Habari na Taasisi za Kiraia (AZAKI)" -Mzee Butiku
Mzee Butiku amesema umuhimu wa kufanya jitihada za kuimarisha amani, umoja, haki na maendeleo ya watu kwa sasa unatokana na matukio ya ghasia na matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.2025
Katika kusindikiza ujumbe huo Mzee Butiku amesema, "mazungumzo ndio nyenzo ya upatanishi na ujenzi wa amani".