My Political Analysis:- The Ndoto Ya Lowassa & Its Syndrome!!

My Political Analysis:- The Ndoto Ya Lowassa & Its Syndrome!!

Wanaokuelewa kuanzia huko nyuma wanadai uhovyo huu umeuanza hivi karibuni, kwa nini nisideduce kwamba unayoaandika hapa yalianzia chumbani someone, yakawasilishwa sebuleni na sasa umeyahamishia hapa.

- naona kama unajisema mwenyewe kaka kumbe ndio tabia zako? duh!

Le Mutuz
 
- Anyerushiwa hicho kinyesi ni nani kaka maana naona wote mnalia lia point yangu ni ile ile Guninita hawezi kumpa urais Lowasa wala Msiandi, au unasemaje wanaweza kweli? ha1 ha!

Le Mutuz

Ndiyo ujione usivyoelewa hata maana ya democrasia? au bado unafikiri mtu akisimamishwa na ccm basi ndo kawa rais. angalia utachanganyikiwa au hauna mafao ya kutumia uzeeni?
 
Mkuu naona hawa jamaa wanakutoa kwenye hoja yako ya Msingi.......always never loose your enemy, it is your target Mr Le Mutuz so keep focused, 2015 is near

- Kaka kunitoa kwenye hoja yangu ya msingi hawawezi ila sometimes lazima niwape luxury ya kuamini so kama wewe!! si bado naandika na gazeti kaka sasa wananitoa vipi?

Le Mutuz
 
Ndiyo ujione usivyoelewa hata maana ya democrasia? au bado unafikiri mtu akisimamishwa na ccm basi ndo kawa rais. angalia utachanganyikiwa au hauna mafao ya kutumia uzeeni?

- Kaka gazeti linakuja Jumapili ndio utajua jinsi nisivyoelewa Demokrasia, ha1 ha! ha
1

Le Big Show
 
Amesema....? ulimsikia au umeambiwa? za kuambiwa changanya na zako!Umesahau msemo huo wa mwenyekiti wako unayemlamba viatu siku hizi baada ya kumponda sana enzi hizo?

- Kaka labda wewe hukumsikia alisema ahukumiwe kwa nia sio kupokea, ha1 ha! rushwa!!

Le Mutuz
 
Mkuu Le Mutus,
By the time tunakutana tulikuwa tumeishawahi kubishana humu jf, hivyo niliamini ulikuwa unanifahamu fika, ili kama ulikuwa hunifahamu, then mimi ndio Pasco wa jf, tukikutana in reality, tunachat poa, tukidanganyana humu jf, tunarekebishana na kuambiana ukweli, bila kuoneana haya eti kwa sababu tunajuana!. Na hata baada ya kupishana humu jf, tukikutana tunasalimia na kuchat as if nothing happened!.

Nashukuru kwa recognition ya kudhani lile ni gari langu, naomba nisijifagilie, ni gari la wife, mimi usafiri wangu ni boda boda (zile big bike) sina gari!.

Japo umeufunga mlango, siku tukikutana pale mahali, au pengine popote, mimi always nitakusalimia tuu, hata kama hutaijibu salaam yangu, kila nikikukuta nitaendelea tuu kukusalimia, sie wengine tunakaa na kuishi vibandani, mlango ni wa gunia, hivyo hatunaga mlango wala dirisha la kufunga!.

Tuendelee kubishana kwa hoja, kukubaliana kwa hoja, na tukipishana kwa hoja na kufikia kukubaliana kutokubaliana ila we are one, we all have something in common, ni jf members!. Kwa Lowassa, najua tunatofautiana tango day 1, na kuna wengi humu tunatofautiana kwa hoja, lakini bado tunaendelea kubishana kwa hoja hadi kufikia kukubaliana kutokubaliana bila kufungiana milango wala kupandishiana madirisha!.

Mimi Pasco wa jf, huwa ninao msimamo wangu fulani dhabiti sana kuhusu wasusaji, let me not add an insult to an injury ila tuendelee kukata hoja za msingi kwa maslahi ya taifa, nothing personal!.

Pasco.
Pasco. The consistent one.
 
Le Mutuz....EL anawatu wengi na ndio maana timu zenu zimeungana bila usajili maalum kumpinga kwa kila njia kila kukicha.Kweli haujawah kujiuliza yeye ni nani mpaka Mzee wetu Jumanne aungane na konda na wengine wengi kupayuka kama machizi kujaribu kuuamijisha uma wa watanzania kwamba lowassa ni mbaya bora hata tuhamie sudan?...Mgekja na hao waliiongea akiwemo na Mzee kingunge wana watu pia ndio maana ni wenyeviti au unadhani kwenye siasa ukubalikaji upo kwenye ubunge na udiwanI tuu?..Hao wamechaguliwa na Mikoa yao na si majimbo kama wabunge.Kaa chini na utafajari
 
- Lowassa atapewa Urais na Msindai? Guninita? Mgeja? kweli kaka unaaamini hawa watampa Urais mgombea wako?

Le Mutuz

Kaka Wile mi nimekuelewa tafakuri yako, kwamba mheshimiwa kazungukwa na wasio washindi ambao ni vigumu kumsaidia kupata ushindi na kutimiza ndoto yake. Angalizo; hao uliowataja wamejitokeza hadharani kumuunga mkono, haijatabanaishwa kuwa ndio wajumbe/washauri au wamo kwenye uongozi wa timu ya kampeni kama tayari imeshaundwa na mheshimiwa. Muda wa kuunda timu yake anao, nani awemo, nani aongoze kikosi kazi, mbinu gani zitumike, nk. Ameonesha nia, na ameanza safari ya ndoto yake, tumpe muda, tumshauri kama wewe ulivyofanya, na mwisho wa siku kura yako na za wajumbe wenzako wa mkutano mkuu ndio zitaamua kusuka au kunyoa 2015!
 
- Kaka kasome kichwa cha mada kwanza, jina langu humu unalijua ni William j. Malecela anyejamba jamba unamjua kaka ni wewe jaribu kuweka jina lako la kweli hapa kama mimi uone, kuna mbunge mmoja wa Chadema mwanamke anakujua sana huwa nakuangalia tu unavyojifanya unajua sana na huku uliwahi kuuza kata ya Chadema kwa Mahanga au sio wewe kaka? ha! ha! ha!

- Kuna Mbunge mmoja wa kike wa Chadema siku moja alinionyesha wewe ninakupotezea kaka au nasema uongo? ha1 ha!

Le Mutuz

Tatizo lako una ujanja wa kizamani sana, kwanza mimi wewe utanijuria wapi? Kwenye vilabu vya pombe na mabonanza?

Kama huwa unatembelea library au unapita British council kweli unaweza kunijuwa lakini si vijiwe vya wauza unga pale kwenye mgahawa wenu.

Hivi nikuulize si nini wewe uliyekuwa unatembea kama fisi ili ukidhani mkono wa binadamu utaanguka?

Au umesahau baada ya kila mtu kuamini Makongoro Mahanga atavuliwa ubunge kutokana na mwenendo wa kesi ukaja na thread yako ya kifisifisi hapa eti ujiandae kugombea segerea kama plan b endapo Mahanga atavuliwa ubunge hivi huu ndio ubinadamu wa ccm?

Na bila aibu siku ya hukumu ukajipenyeza mpaka ukaongozana na Mahanga mahakamani lakini hukumu iliposomwa ulihuzunika kuliko hao Chadema wenyewe mchawi wewe.
 
Tatizo lako una ujanja wa kizamani sana, kwanza mimi wewe utanijuria wapi? Kwenye vilabu vya pombe na mabonanza?

Kama huwa unatembelea library au unapita British council kweli unaweza kunijuwa lakini si vijiwe vya wauza unga pale kwenye mgahawa wenu.

Hivi nikuulize si nini wewe uliyekuwa unatembea kama fisi ili ukidhani mkono wa binadamu utaanguka?

Au umesahau baada ya kila mtu kuamini Makongoro Mahanga atavuliwa ubunge kutokana na mwenendo wa kesi ukaja na thread yako ya kifisifisi hapa eti ujiandae kugombea segerea kama plan b endapo Mahanga atavuliwa ubunge hivi huu ndio ubinadamu wa ccm?

Na bila aibu siku ya hukumu ukajipenyeza mpaka ukaongozana na Mahanga mahakamani lakini hukumu iliposomwa ulihuzunika kuliko hao Chadema wenyewe mchawi wewe.

- ha1 ha! mbona umepanic kaka, tuliza boli mada inahusu Lowassaa sio mahanga!1

Le Mutuz
 
Kaka Wile mi nimekuelewa tafakuri yako, kwamba mheshimiwa kazungukwa na wasio washindi ambao ni vigumu kumsaidia kupata ushindi na kutimiza ndoto yake. Angalizo; hao uliowataja wamejitokeza hadharani kumuunga mkono, haijatabanaishwa kuwa ndio wajumbe/washauri au wamo kwenye uongozi wa timu ya kampeni kama tayari imeshaundwa na mheshimiwa. Muda wa kuunda timu yake anao, nani awemo, nani aongoze kikosi kazi, mbinu gani zitumike, nk. Ameonesha nia, na ameanza safari ya ndoto yake, tumpe muda, tumshauri kama wewe ulivyofanya, na mwisho wa siku kura yako na za wajumbe wenzako wa mkutano mkuu ndio zitaamua kusuka au kunyoa 2015!

- ha! ha! ha1 ha! umenivunja mbvu sana kaka!!,

Le Mutuz
 
- Umesema mengi sana lakini yote hayahusu, pole sana kaka mimi ni William J. Malecela kama jina langu linavyosema siku moja kuna mtu alinionyesha kuwa Mchambuzi ni yule pale nikakupotezea maana huwa sipendi kujuana sana na watu humu wanaotumia majina ya bandia, kaka ushauri wangu kwako wa mwisho ni kwamba kama kweli wewe ni mkweli kama mimi tumia jina lako la kweli kama mimi otherwise tuliza boli.

Le Mutuz

The fact kwamba kuna watu wananinyooshea vidole wakikuambia mchambuzi yule pale maana yake ni kwamba wananijua hivyo wana fursa ya kunisalimia lakini pia kuniumiza wakiamua hivyo ingawa humu natumia "mchambuzi";

The fact kwamba nimeweka picha yangu halisi hivyo kujulikana kwa wengi kwamba mimi ni nani inatosha kunipa real identity;isitoshe kama utambulisho duniani ungekuwa ni majina tu ya abdalah, selemani, paulo au rose, basi ingekuwa vigumu sana kutofautisha watu kwa majina, hakuna utambulisho wa maana zaidi ya sura au DNA ya mtu;

The fact kwamba mwana ccm anayeendesha twitter ya ccm huwa ananijadili mimi ni nani kwa ufasaha huku akiumizwa na hoja zangu maana yake kujiita mchambuzi hakujazuia watu kujua my actual identity hata kama natumia "mchambuzi";

The fact kwamba baadhi ya makada wa CCM Lumumba from time to time huwa wananipigia simu kunipa hongera kwa makala nzuri huku pia wakiomba niwasaidie kuweka papers hizi na zile vizuri for presentation maana yake ni kwamba najulikana ni nani hata kama natumia "mchambuzi";

The fact kwamba jumuiya ya wachumi nchini walitafuta namba yangu na kunipigia kuniomba niwasaidie na draft yao iliyochambua uchumi wa taifa kuelekea bajeti ya 2013-14 na pia kunialika blue pearl ubungo kuwa mmoja wa keynote speakers maana yake ni kwamba najulikana ni nani hata kama humu natumia "mchambuzi";

The fact kwamba gazeti la citizen linanitafutaga kwa simu kuomba wachukua some of my material kwa ajili ya makala zao maana yake ni kwamba najulikana ni nani hata kama humu natumia "mchambuzi";

The fact kwamba StarTv walitafuta simu yangu na kunialika kwenye kipindi chao cha asubuhi nikajumuike na zitto, mwigulu, mtatiro na dr mkumbo katika kipindi kile cha star tv cha asubuhi maana yake ni kwamba tayari najulikana ni nani;nilikuwa chumba kimoja siku ile na wahusika hapo juu kasoro kitila ambae alikuwa mapokezi, siku ambayo mwigulu alitoa habari kwamba ana mkanda unaoonyesha mipango ya utekaji etc chadema; katika kipindi kile niliitwa pembeni na mtu mmoja wa star tv na kuambia imetolewa amri kwamba mchambuzi asizungumze;

Last but not least nikiri kwamba mwanzoni: nilianza kwa kuficha sura huku jina nikiweka as mchambuzi lakini baadae nikaona ni unafiki usio na kifani;katika hilo naomba nikupongeze pia wewe kwa kujianika wazi;that said and done - niliwahi jadiliana na Invisible juu ya uwezekano wa kubadili jina na kuweka jina langu halisi lakini baada ya kushauriana na watu kadhaa nikaona nitapoteza rekodi zangu zote humu kwa kuja na ID mpya, kwahiyo nipo tayari kujibu maswali juu ya jina langu nani ikibidi lakini kubadili jina ni suala ambalo sitafanya kwa hoja hii;

Mwisho - nashukuru kwamba you never bother to talk to me ukiniona in public kwani sidhani kama you will have substance zaidi ya nonsense katika kujadili mustakabali wa taifa, hasa juu ya hatima ya watanzania walio wengi miaka 50 ya uhuru;

Usikatae kwamba wewe sio field marshall es, sio mara moja au mbili huwa unajisahau na kuandika "le mutuz" baada ya kutoa hoja as field marshall es then quickly go back to edit kufuta neno "le mutuz"; habari zisizo njema pengine kwako ni kwamba at least once nili save post yako kabla ya ku edit na zipo kwenye my desktop;




Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Quote of the decade from a ccm stalwart' Ukiwa mwana ccm usiwe mkweli'
Mkuu Mtoboa siri, kwanza Pasco wa jf, sio CCM, pili hana chama, tatu ni mkweli daima no matter what!.

Ni ukweli usiopingika, CCM na serikali yake, hawapendi kuambiwa ukweli, na hawawapendi watu wanaosimama kwenye kweli au kusimamia ukweli!. Nape aliopusema ule ukweli wa ukodishaji jengo la UVCCM, alitaka kufukuzwa CCM. Kwenye Richmond, mwenye zigo sio EL, hivyo EL alijiuzulu ili kumkingia kifua mwenye zigo lake na kuiokoa CCM!. CCM kimehodhiwa na matajiri, mafisadi na wala rushwa wakuu, mwenye afadhani ni EL angalau anarudisha kidogo kwenye jamii!. Siasa za CCM ni rushwa, majungu, fitna, zengwe na uongo mwiingi!. Ukijifanya mkweli, CCM itakushinda!. Mkuu Mchambuzi ni mkweli mon, niliisha mwambia yuko on a wrong party!. Huyu jamaa yangu na baadhi ya makala zake, anataka kujidai kuiambia CCM ukweli!, they'll not like it, and kwa kujifanya mkweli, he'll soon end up a looser!. Ili kuweza kusurvive CCM, lazima uwe
  1. Muongo, au muongo muongo.
  2. Mtu wa fitna
  3. Uwe mpika majungu mzuri.
  4. Uwe mnafiki, kwa kusema hili huku you don't mean ti, na kushangilia hata lisiloshangillika.
  5. Mla rushwa na ukiutaka uongozi, uwe mtoa rushwa mzuri, hata ile pilau tuu, au t=shirt na kofia hadi rushwa kubwa kubwa!.
  6. Uwe mtu wa kujikomba komba kwa sana!.
Pasco.
 
Nimecheka sana baada ya kusoma hii so called "Political Analysis"
Le Mutuz, hivi vyuo vya Mamtoni particularly in New York ndiyo wanafundisha ku-analyze issue(s) kama ulivyoteleza hapa!!?? Mie sina hata hako kabachala lakini sioni analysis yoyote hapo. Labda nikikapata hako kabachala ndipo nitaweza hata ku-analyze analysis. Ngoja nitafute ka-skolashipu ka New York.
 
Back
Top Bottom