My Political Analysis:- The Ndoto Ya Lowassa & Its Syndrome!!

My Political Analysis:- The Ndoto Ya Lowassa & Its Syndrome!!

Joined
Apr 27, 2006
Posts
26,584
Reaction score
10,466
- Baada tu ya Mh. Lowassa kutangaza ndoto yake kwenye Sherehe za Mwaka Mpya huko jimboni kwake, kukaaanza malumbano yakiongozwa na watu wake wa karibu sana wa kwanza alikuwa Msindai, Mgeja, Guninita, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar na Mwenyekiti wa CCJ chama kilichokufa kabla hakijaanza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha. Hawa ndio kweli Mh. Lowassa anayetaka Urais wa Jamhuri hii ndio aliowaona credible Leaders wa kumzungumzia kwa huu umma na kama sikosei kwa maneno mengine anatuambia kwamba akishika Urais wa Jamhuri hii hawa ndio tuwategemee kama Viongozi wakuu wa Taifa.

- Msindai aligombea Ubunge akashindwa, Mgeja chini ya uongozi wake Mkoa wa Shinyanga CCM imepoteza viti vingi vya ubunge kuliko mikoa yote huku Bara, Guninita amegombea Uenyekiti wa Mkoa wa Dar akashindwa na chini ya uongozi wake Majimbo mawili muhimu sana yameenda Upinzani, lakini kweli Lowassa anaamini kwamba hawa wanaweza kumsaidia kuifikia ndoto yake hiyo ya muda mrefu sana kama alivyosema mwenyewe.

- Well, simchukii wala simuungi mkono na mbio zake, lakini kwa hayo machache niliyokwisha yaona na kuyasikia maana yake ni moja kwamba sitapata shida ya kuamua kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa kuamua mgombea ambao mimi ni mjumbe kama nimpe kura yangu au hapana, iwapo jina lake litkuwepo!!

- MAKALA YANGU NZIMA YA HII HABARI ITAKUWA KWENYE GAZETI LA JAMBO LEO JUMAPILI.

Le Mutuz
 
W. J. Malecela Hata siku moja mtoto wa kenge hawezi akageuka kuwa mjusi,we unafikiri hao wanaompiga EL ndio watu ambao wana uwezo ?mfano mzuri ni abdala (mzee malecela) baba yako.fanya kwanza uchambuzi wa hao wanaompinga ukishajua uwezo wao ndio uje hapa anza na mzee malecela aka abdala aliyebadilisha dini ili apate support ya kugombea urais.
 
Last edited by a moderator:
Hata siku moja mtoto wa kenge hawezi akageuka kuwa mjusi,we unafikiri hao wanaompiga EL ndio watu ambao wana uwezo ?mfano mzuri ni abdala (mzee malecela) baba yako.fanya kwanza uchambuzi wa hao wanaompinga ukishajua uwezo wao ndio uje hapa anza na mzee malecela aka abdala aliyebadilisha dini ili apate support ya kugombea urais.

Mkuu, kwani John amebadili jina anaitwa Abdallah siku hizi?
Mi mgeni hapa Posta tafadhali nijuze. Koz recently nilisikia kuna baadhi ya viongozi wengi wamesilimu (wamebadili dini) eti kisa................. Daaah.. nchi hii ina mambo sana.
Tehe tehe tehe tehe
 
- Msindai aligombea Ubunge akashindwa, Mgeja chini ya uongozi wake Mkoa wa Shinyanga CCM imepoteza viti vingi vya ubunge kuliko mikoa yote huku Bara, Guninita amegombea Uenyekiti wa Mkoa wa Dar akashindwa na chini ya uongozi wake Majimbo mawili muhimu sana yameenda Upinzani, lakini kweli Lowassa anaamini kwamba hawa wanaweza kumsaidia kuifikia ndoto yake hiyo ya muda mrefu sana kama alivyosema mwenyewe.
Le Mutuz
Hapo kwenye RED nampongeza huyo jamaa maana alikubali demokrasia ichukue mkondo wake, unaposema alipoteza viti vya ubunge kwa wapinzani maana yake unatamani kwamba angefanya wizi wa kura kuhakikisha CCM inapata "ushindi wa kishindo"

Kama hizo mbinu chafu ndo zinamfanya mtu kuwa kiongozi mzuri ni bora hasiwe kiongozi, We ni kijana lakini unaonekana na wewe ushalishwa sumu ile ile, kama baba,kama mtoto!
 
Nani anasoma Jambo Leo? Gazeti la wauza....... unajua!
 
CCM sasa wanakutumia weye kufikisha message? kumbuka tu kwamba mziki wa EL si wa kitoto kabla ya maamuzi yoyote litambueni hilo.
 
-
- Well, simchukii wala simuungi mkono na mbio zake, lakini kwa hayo machache niliyokwisha yaona na kuyasikia maana yake ni moja kwamba sitapata shida ya kuamua kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa kuamua mgombea ambao mimi ni mjumbe kama nimpe kura yangu au hapana, iwapo jina lake litkuwepo!!

- MAKALA YANGU NZIMA YA HII HABARI ITAKUWA KWENYE GAZETI LA JAMBO LEO JUMAPILI.

Le Mutuz
Mkuu Le Mutus, with due respect, Lowassa, haihitaji kabisa kura yako!, nashukuru at least this time umekuwa mkweli kuwa "humchukii!", hilo la kumuunga mkono sio issue sana kwa sababu ndani ya CCM, kwa sababu, kwa maoni yako, nadhani ndani ya CCM, wewe utakuwa huna impact yoyote ya maana kufikia kiwango cha kuitishia kasi yake au hata kuipunguza kasi!, kama aliyewahi kuwa Makamo Mwenyekiti amelonga na kapuuzwa, itakuwa wewe?!, nakushauri endelea tuu ku symphasize na Mzee wako ili angalau mmalize salama!.

Tena nakupa ushauri wa bure, ukiwa mwana CCM, usijifanye kuwa mkweli saana kivile!. CCM haiwapendi wakweli wa type yako!. Kama kuanzia Mwenyekiti wako, JK, Katibu wako Mkuu, Kinana, mabosi wenu wa jumuiya za Chama, Wazazi, Wanawake na Vijana, wenyeviti wa CCM karibu wote ni watu wa Lowassa, who are you, hata usipomuunga mkono?!, Mwenzio Nape keshaujua ukweli, hebu mfuatilie kama anaendelea kupayuka lolote kumhusu mtu huyu!.

Nakushauri just keep on the good job you do kwenye blog yako, I think as of now, that is the best you can do, and make a lot money!, please make them more and more, ilihata 2015 ukiamua kujaribu tena, angalau utakuwa nazo za kutosha kuchagulika, kwa sara, EL achana nae kabisa!.

Pasco.
 
Mkuu kwani wewe mmoja unapiga kura mia! Mpaka uone kura yako n muhimu sana?
 
weka wazi unamuunga mkono nani? aya asante ila fahamu kuwa hakuna wa kumzuia lowasa, wewe ni 1, hao uliowataja ni 4. bado wengine nyuma kibao.
 
Lazima uungane na babako!

Umezungumzia sana suala la kushindwa chaguzi na je unamzungumziaje babako alivyoshindwa na kibajaji?
Hivi na wewe kushindwa kwako ubunge afica mashariki umejigrade vipi?
 
Le mutuz analysis yako iko poa kwani unawakilishaa mawazo yako huru. Kuhusu hao wapiga filimbi uliowataja ndo aina kubwaa ya tabia za wajumbe wa vikao vya CCM.
Angalizo: Lowasaa anaonekana kuwa na nguvu kubwa ndani ya vikao vya chama hasa NEC na mkutano mkuu kutokana na tabia ya wajumbe wengi kupenda kulamba mkono na kwa hilo amejijenga na kujiandaa vemaa.
 
Back
Top Bottom