The fact kwamba kuna watu wananinyooshea vidole wakikuambia mchambuzi yule pale maana yake ni kwamba wananijua hivyo wana fursa ya kunisalimia lakini pia kuniumiza wakiamua hivyo ingawa humu natumia "mchambuzi";
The fact kwamba nimeweka picha yangu halisi hivyo kujulikana kwa wengi kwamba mimi ni nani inatosha kunipa real identity;isitoshe kama utambulisho duniani ungekuwa ni majina tu ya abdalah, selemani, paulo au rose, basi ingekuwa vigumu sana kutofautisha watu kwa majina, hakuna utambulisho wa maana zaidi ya sura au DNA ya mtu;
The fact kwamba mwana ccm anayeendesha twitter ya ccm huwa ananijadili mimi ni nani kwa ufasaha huku akiumizwa na hoja zangu maana yake kujiita mchambuzi hakujazuia watu kujua my actual identity hata kama natumia "mchambuzi";
The fact kwamba baadhi ya makada wa CCM Lumumba from time to time huwa wananipigia simu kunipa hongera kwa makala nzuri huku pia wakiomba niwasaidie kuweka papers hizi na zile vizuri for presentation maana yake ni kwamba najulikana ni nani hata kama natumia "mchambuzi";
The fact kwamba jumuiya ya wachumi nchini walitafuta namba yangu na kunipigia kuniomba niwasaidie na draft yao iliyochambua uchumi wa taifa kuelekea bajeti ya 2013-14 na pia kunialika blue pearl ubungo kuwa mmoja wa keynote speakers maana yake ni kwamba najulikana ni nani hata kama humu natumia "mchambuzi";
The fact kwamba gazeti la citizen linanitafutaga kwa simu kuomba wachukua some of my material kwa ajili ya makala zao maana yake ni kwamba najulikana ni nani hata kama humu natumia "mchambuzi";
The fact kwamba StarTv walitafuta simu yangu na kunialika kwenye kipindi chao cha asubuhi nikajumuike na zitto, mwigulu, mtatiro na dr mkumbo katika kipindi kile cha star tv cha asubuhi maana yake ni kwamba tayari najulikana ni nani;nilikuwa chumba kimoja siku ile na wahusika hapo juu kasoro kitila ambae alikuwa mapokezi, siku ambayo mwigulu alitoa habari kwamba ana mkanda unaoonyesha mipango ya utekaji etc chadema; katika kipindi kile niliitwa pembeni na mtu mmoja wa star tv na kuambia imetolewa amri kwamba mchambuzi asizungumze;
Last but not least nikiri kwamba mwanzoni: nilianza kwa kuficha sura huku jina nikiweka as mchambuzi lakini baadae nikaona ni unafiki usio na kifani;katika hilo naomba nikupongeze pia wewe kwa kujianika wazi;that said and done - niliwahi jadiliana na
Invisible juu ya uwezekano wa kubadili jina na kuweka jina langu halisi lakini baada ya kushauriana na watu kadhaa nikaona nitapoteza rekodi zangu zote humu kwa kuja na ID mpya, kwahiyo nipo tayari kujibu maswali juu ya jina langu nani ikibidi lakini kubadili jina ni suala ambalo sitafanya kwa hoja hii;
Mwisho - nashukuru kwamba you never bother to talk to me ukiniona in public kwani sidhani kama you will have substance zaidi ya nonsense katika kujadili mustakabali wa taifa, hasa juu ya hatima ya watanzania walio wengi miaka 50 ya uhuru;
Usikatae kwamba wewe sio field marshall es, sio mara moja au mbili huwa unajisahau na kuandika "le mutuz" baada ya kutoa hoja as field marshall es then quickly go back to edit kufuta neno "le mutuz"; habari zisizo njema pengine kwako ni kwamba at least once nili save post yako kabla ya ku edit na zipo kwenye my desktop;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums