Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, Ikulu Chamwino

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika tarehe 21 Mei, 2023 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


4 (5).jpg
G1.jpg
2 (12).jpg
 
naamini changamoto ya TRA na wafanyibiashara imetoka na suluhisho muafaka I guess kutakua na mabadiliko TRA
 
Tunataka kuona matokeo chanya ya hivyo vikao kwenye maisha ya wakulima na watu wa hali ya chini na sio matajiri na Wafanyabiashara wakubwa.

Hiyo ndio CCM ya Karume na Nyerere.
 
CCM haitaki kupitwa katika kulizindua jengo Kwa kikao cha kwanza ndani yake kila la kheri.
 
Chadema huwa hawana matamko ya vikao kila mwana Chadema ni msemaji wa Chama God bless lema anaita kazi ya bodaboda laana mwenyekiti Mbowe na Lisu wanasindikizwa na bodaboda na kuheshimu boda boda

Mbowe anaongelea na kuheshimu Maridhiano Lisu anaita maridhiano hayana maana

Lisu anasema Katiba Mpya ndio agenda muhimu Mbowe anasema tunahitaji maridhiano ya kitaifa

Chadema Taifa hakitangazi maandamano ya kutaka wabunge wa Chadema walioko Bungeni waondoke Bawacha yenyewe inajiamulia kuingia barabarani kivyake

Yaani Chadema kwa sasa haiko organised kabisa haina Central voice kila anayejisikia kubweka chochote anabweka tu
 
Bi Mjema amebadili upashanaji habari? Mbon siku hizi tunashitukizwa tu na vikao.

Chama chetu kinazidiwa hadi na ACT kwenye kupashana habari?. Au kuna bango sehemu linaongelea hiki kikao?
 
Siyo
Hiyo ni CCM ya Azimio la Zanzibar. Viongozi wawe wafanyabiashara
Tunataka kuona matokeo chanya ya hivyo vikao kwenye maisha ya wakulima na watu wa hali ya chini na sio matajiri na Wafanyabiashara wakubwa.

Hiyo ndio CCM ya Karume na Nyerere.
 
Ikulu tena??Si wangeenda kwenye office za CCM. Ila CCM wanadharau sana huu ujinga hauwezi ukuta nchi zingine.
Chama Chenyewe Kinajiogopa Kinakwenda Kujifia Taratibu Tanzania 🇹🇿
Hakitakiwi Ila Kinategemea Hawa Hapa Tu:-NEC,DPP, COURT, JW,TISS,PCCB,POLICE, PRISON, IMMIGRATION, FIRE, MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA
 
Back
Top Bottom