sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,034
Diamond sio mmiliki mkuu wa makampuni kama wasafi tv, wasafi radio, wasafi bet, Diamond karanga (r.i.p), yeye nafasi yake huwa ni co-owner, anachofanya ni kuwekeza tu jina lake na kuchukua asilimia zake kwenye faida. Uhakika wa 40%-49% ya umiliki na faida upo chini yake kwa kutoa tu jina wasafi litumike kwenye kampuni.
Hata Azam Bakhresa nae hufanya hivyo Kwa kuyapa ruhusa baadhi ya makampuni kutumia jina la azam kwenye bidhaa zao kwa makubaliano ya kugawana umiliki, faida, menejment, n.k
Kuna kipindi flani wahindi waliokuwa wanstengeneza dismond karanga waliona zinauzika sana na kuingiwa tamaa , ulafi na wivu kuona kwamba Diamond hastahili mgao mkubwa kwasababu kachangia tu jina, wakati wao wametia mtaji mrefu keenye pesa, kununua mashine, n.k Diamond akaachana nao ili wapambane kivyao na wajue thamani halisi ya jina lake, Leo hii hizo karanga zipo wapi ??
Na hivi ndivyo hali ilivyo kwenye Wasafi tv na Wasafi fm, Kusaga ndie alieweka mtaji, uzoefu wake, connection zake, n.k lakini Diamond alichangia tu jina kwa maelewano kwamba atamiliki hisa zinazompa umiliki si haba, mgao wa faida mnono na pia kuwa na maaumuzi kwa kiasi mfano kuwa ceo wa kampuni.
Hata hii kampuni mpya ya kubet ya Wasafi bet, ni makubaliano baina ya kampuni ya kubeti ya nchini Kenya inayoitwa odibet, ni kampuni ambayo ingeingia hapa nchini kichwa kichwa ingepata wakati mgumu sana kufahamika na kuoata wateje, kwa hiyo wameamua kutumia shortcut kwa kutumia jina kubwa la Wasafi kwa makubaliano ya mgao katika umiliki, faida, usimamizi, n.k.
Take it or leave it
Hongera sana Diamond