Hakuna msanii mwenye pumzi ya kukimbizana na Diamond kiuchumi, biashara zinamlipa kuzidi muziki

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
1638016528059.png


kumlinganisha diamond kiuchumi na wasanii ambao wengi wao hata linapokuja swala la usafiri wanavimba na toyota crown za miaka kumi iliyopita, inakuwa sio fair

Sote tunajua ya kwamba kuanzisha biashara kubwa ni gharama kubwa na ni hatari endapo ukila za uso, unaweza kuanzisha biashara mbili, moja ikatusuana nyingine ikadoda, hata kwa upande wa Diiamond, biashara ya label yake ilitiki lakini kwa upande wa biashara ya perfume, ilikufa kifo cha mende.

Tukiachana na biashara ya label ya wasafi ambayo yeye huwagharamia wasanii kurekodi video za makumi ya mamilioni, kuajiria ma manager wa kuwasimamia. kutumia connectiions zake ili wasanii wasihangaike, kuwapa airtime kwenye radio na tv, n.k kwa makubaliano ya kuchukua mgao wa 60% ya mapato, Diamond kwa sasa kapiga hatua ya ziada kwa kuona fursa mpya ya ziada, katambua ya kwamba umaarufu wake mkubwa sana unaoweza kumuingizia mtonyo mrefu zaidi kwa uhakika.

Diamond kwa sasa anachofanya ni kuwekeza tu jina lake kwenye kampuni ambazo zina uzoefu na mitaji mikubwa lakini zinahitaji booster ya umaaufu ili ziwe maarufu kwa haraka na kupata wateja wengi, na ndipo hapa jina la Diamond au Wasafi linawekezwa kama sehemu ya mtaji muhimu. Chukulia kwa mfano zile karanga za diamond, zingeiingizwa sokoni hivi hivi, huenda hata zisingefikia theluthi ya mauzo yaliyokuwa yakipatikana zilipofahamika sokoni kwa jina la Diamond karanga, baada ya wahindi kuingia tamaa ya kutaka kumpunguzia Diamond mgao wake, kilichofata diamond aliwaambia wapambane kivyao, leo hii karanga zipo wapi.

Kwa kutambua kwamba jina lake ni kubwa, yeye huwekeza jina hilo kwa makubaliano ya kupewa hisa ili awe sehemu ya umiliki, faida, uendeshaji, n.k kwa sasa makubaliano haya yapo wasafi tv, wasafi radio na wasafi bet, yeye sio muanzishaji wa hizi biashara, yeye anachangia tu jina analamba asilimia zake takribani 40% hadi 50%, take it or leave it (chukua ama acha ukapambane kivyako!!)

Kwa pesa anazopata kijana, ni dhahiri kabisa ni nyingi kuzidi hata za mziki anaofanya, hizi jeuri za kununua mikufu ya milioni 200 , gari la rolls royce toleo la mwaka huu huu, escallede mbili za mwaka jana, n.k zimekuja baada ya kuingia hizi deals, hapo zamani kijana hakuwa na uwezo huu.

Kuna msanii yupi hapa bongo ana pumzi ya kumfikia Diamond?
 
View attachment 2025120

kumlinganisha diamond kiuchumi na wasanii ambao wengi wao hata linapokuja swala la usafiri wanavimba na toyota crown za miaka kumi iliyopita, inakuwa sio fair
Huyo Diamond ni mtoto mdogo sana. Msanii anayeongoza kwa utajiri duniani kwa sasa, ni kijana Mtanzania kutoka wilayani Kahama tu hapo mkoani Shinyanga.

Piga keleleeeeeeeeeeeee kwaaaaaaaa msaniiiiiii tajiiiiiiiirrriiiiiiiiiiii

Dj DON NALIMISON
 
itakua mwamba yupo kazini.

Naona kuna nguvu kubwa sana ya kumwelezea simba na mafanaikio yake,sijui ni inside job ama kazi za watu kujipa wenyewe.

Amenunua gari la bei mbaya kuliko hata SSB lakini bado kama watu wameipotezea hivi,so inavuruga.
juzi akapost mapete ya malaki ya $$$$,mpaka nashangaa mdogo wetu tatizo nini!!!!
 
Jamaa umeongea ukweli.mzito jamaa ameweza kutumia sanaa vizuri mwishowe imempa conection ya mabiashara kwa sasa jamaaa mziki hautegemei tena kashawekeza kwenye mabiashara kiufupi huyu sio mwenzetu ni tajiri
 
Ushabiki ukizidi kuliwa hakupo mbalii mtoa mada siri ya mtungi aijua mama yake na mm mjomba wake
LiSquare_20211127224824853.jpg
 
Back
Top Bottom