Mwekezaji inabidi ampe Diamond takriban nusu ya faida ili kutumia jina la WASAFI lasivyo apambane kivyake

Diamond sio mmiliki mkuu wa makampuni kama wasafi tv, wasafi radio, wasafi bet, Diamond karanga (r.i.p), yeye nafasi yake huwa ni co-owner, anachofanya ni kuwekeza tu jina lake na kuchukua asilimia zake kwenye faida. Uhakika wa 40%-49% ya umiliki na faida upo chini yake kwa kutoa tu jina wasafi litumike kwenye kampuni.

Hata Azam Bakhresa nae hufanya hivyo Kwa baadhi ya makampuni yanayotambulika kwa Brand yake maarufu ya Azam, wawekezaji wanaweza kuwa huko nchi nyingine, wao wanamuomba Bakhresa awaruhusu watumie jina la Azam kwa makubaliano ya mgao kwenye umiliki, faida, menejment, n.k

Kpindi kile Diamond Karanga, wahindi walipoona zinauzika sana walitaka kuleta janja janja na ulafi baada ya kuona biashara inalipa, wakaanza kulalamika kwamba wananyonywa kwasababu Diamond kachangia tu jina na anapata mgao mkubwa wakati hajachangia mtaji, Leo hii hizo karanga zipo wapi? Nadhani mmeiona thamani ya jina hapo.

Na hivi ndivyo hali ilivyo kwenye Wasafi tv na Wasafi fm, Kusaga ndie alieweka mpunga kununua vifaa vingi lakini Diamond alichangia tu jina kwa maelewano kwamba atamiliki hisa zinazompa significant influence.

Hata hii kampuni yake mpya ya kubet ya Wasafi bet, ni makubaliano baina ya kampuni ya kubeti ya nchini Kenya inayoitwa odibet, ni kampuni ambayo ingeingia hapa nchini ingepata wakati mgumu sana kupata jina na wateje, kwa hiyo wameamua kutumia shortcut kwa kutumia jina la Wasafi kwa makubaliano kwamba faida wagawane kwa asilimia ambazo ni si haba.

Kama unaona huu ni unyonyaji, hii ni nchi huru, mlango upo wazi unatafuta kwengine

Hongera sana Diamond
Hawa odibet wana lile tangazo la kibunifu sana jamaa anakula ugali.
Napenda ubunifu wake
 
Hata hizo hisa za wasafi Tv hakutoa jina tu, alitoa pesa pia na aliwahi kusema wakati wanaanzisha alikuwa anatumia milioni 100 kwa mwezi. Hiyo m. 100 inaweza kuwa ni uongo lakini inaonesha kwamba alitoa fungu na yeye.
Unachosema hapa ni biashara kichaa hakuna anaeweza kutoa 45% kwa jina tu. Wewe unaweza kutoa 40% kwenye biashara yako?
sio jina tu, wanatumia pia ushawishi wake kurahisisha biashara.
 
Hujaelewa.. Wewe ndio azam kwani?

Nimekuuliza wewe unaweza kumpa mtu asilimia ngapi ya mtaji wako na biashara yako Kwa kutumia jina lake tu?
Duuuu kazi ipo...

Okey! mm kumpa mtu asilimia za mtaji inategemeana na anachokileta kwenye huo mtaji na kitakavyoleta faida.

Nimeshawahi kumpa mtu nafasi kwenye kampuni kwa sababu tu ana connection na mtu ambaye ni potential sana na alikuwa kati ya wachangiaji wazuri sana wa kodi serikalini.

Sikujutia maana tenda ya kampuni anayotoka huyo mtu simu ikipigwa ya kuhitaji huduma unajua in two to three month mambo angalau ni mazuri hata asipopatikana mteja mwingine.

Huyo mtu pesa alizozileta kwa kufaamiana na huyo mteja zilifikisha kampuni mbali na huenda thamani ya uwepo wake hapa ulizidi jina la kampuni sababu tu ya hiyo connection moja aliyo nayo.

Nadhani nimekujibu.
 
Hujanijibu.

Kwa mfano wako hapo juu, ni kwamba huyo jamaa ulimpa nafasi ya ajira au kuwa partner wa biashara yako? Baada ya kukuletea faida kubwa mligawana hiyo faida pekee au uligawana nae mtaji wako na uwekezaji wako Kwa ujumla?
 
sio jina tu, wanatumia pia ushawishi wake kurahisisha biashara.
Jina ndio ushawishi wenyewe huo. Kama unamaanisha connections serikalini hiyo mbona hata hawamuhitaji Diamond, kuna watu kibao wa kutoa hizo connections kwa bei rahisi tu.

Diamond amechukuliwa sababu wasafi inafahamika hivyo ni rahisi kujulikana bidhaa yako kwa muda mfupi. Kuna njia nyingine za kuitangaza kampuni ijulikane haraka ambapo huhitaji hata kutoa hisa hata moja kwahiyo sio kwamba kuchukuliwa kwa wasafi maana yake hakuna mbadala wao. Jina la wasafi lina thamani ila sio hiyo ya 40%

Tuje kwenye uhalisia wa biashara. Unaweza kurisk 40% ya hisa zako kwa ajili ya jina tu wakati hujui kama hiyo pesa itarudi au lah? Na kama itarudi, je itarudi na faida ile ile uliyoitegemea au lah.
 
Tuje kwenye uhalisia wa biashara. Unaweza kurisk 40% ya hisa zako kwa ajili ya jina tu wakati hujui kama hiyo pesa itarudi au lah? Na kama itarudi, je itarudi na faida ile ile uliyoitegemea au lah.
Waulize wahindi wa Diamond Karanga walipoanza kuleta tamaa na kuona haiingii akilini Diamond kachangia tu jina apewe mgao mnono 😂😂 leo hizo karanga zipo wapi baada ya Diamond kutoa jina lake??
 
Hujanijibu.

Kwa mfano wako hapo juu, ni kwamba huyo jamaa ulimpa nafasi ya ajira au kuwa partner wa biashara yako? Baada ya kukuletea faida kubwa mligawana hiyo faida pekee au uligawana nae mtaji wako na uwekezaji wako Kwa ujumla?

Sikia: Ukiachana na public company ambapo shares zinaweza kugawanyika kwenye ordinary shares(wenye hizi shares ni owners and decision makers, they enjoy profit and suffer loss) na preference shares(wenye hizi shares ni Investors, they enjoy only profit they dont suffer losses), kwa kampuni hizi za kawaida wenye shares ndo wamiliki.

Sasa kwenye case kama hii, Unaweza ukawa na ujuzi ambao una faida au unamiliki jina lenye goodwill kubwa wenye kampuni wakaona wakupe shares lets say 20% ili watumie ujuzi au jina lako, ukishapewa hiyo 20% ina maana katika hiyo kampuni wewe unamiliki 20% ya hiyo kampuni. Kama kuna gawio Eps, utapewa 20% ya total profit na ikitokea hasara itakuhusu kwa 20% ltd to company asset.

Ikitokea mnadissolve kampuni, kwa kutegemeana na memart yenu inavyoelekeza, utapewa 20% ya asset baada ya kulipa kodi na madeni ya watu
SASA HUELEWI NINI?
 
Umefafanua vizuri. Sasa ndio nakuuliza tena. Wewe uko tayari kutoa asilimia ngapi za biashara yako Kwa kutumia jina tu la mtu?

Na mfano ikipatikana loss na mtu hajaweka chochote kwenye biashara zaidi ya Jina lake tu, Je, atatoa pesa mfukoni mwake ku cover hiyo loss? Au utatumika utaratibu gani Kure cover hiyo loss?

Kabla biashara haijafikia kwenye break even point uendeshaji wake kigharama unakuwaje?

Unafahamu kitu kinaitwa economic benefits kwenye partnership za biashara?
 
Umefafanua vizuri. Sasa ndio nakuuliza tena. Wewe uko tayari kutoa asilimia ngapi za biashara yako Kwa kutumia jina tu la mtu?
Inategemeana na hilo jina lina manufaa gani kwenye biashara.
Cocacola wakiniambia tumia jina letu kwenye vinywaji vyako ntawapa hata 60% of shares mm nibakiwe na 40%.
Na mfano ikipatikana loss na mtu hajaweka chochote kwenye biashara zaidi ya Jina lake tu, Je, atatoa pesa mfukoni mwake ku cover hiyo loss? Au utatumika utaratibu gani Kure cover hiyo loss?
Utaratibu wa kugawana hasara ni LTD to company assets.
Kabla biashara haijafikia kwenye break even point uendeshaji wake kigharama unakuwaje?
The question is too general. Uendeshaji wa biashara unategemeana na business plan na memart zinavyoelekeza.
Unafahamu kitu kinaitwa economic benefits kwenye partnership za biashara?
The question is too wide. Ni kama vile unauliza mambo kuonyesha kuwa una uelewa mpana wa mambo ya biashara. Sasa sijajua kama unagoogle au uelewa unao kweli. Ila nikiangalia historia ya hoja naweza weka assumption kuwa unagoogle. Forgive if I am wrong.
 
Mkuu tatizo lipo wapi kwani juu ya hizo kebehi,

Mfano kampuni imeingiza faida ya bilioni 1, Diamond anaweza kupewa asilimia 42 sawa na milioni 420 (wasafi tv na fm anachukua 45%).

Huenda hata zile rolls royce na escallade hajanunua kwa pesa ya muziki, maana deals kama hizi zina mpunga mrefu sana
Kulipa mishahara inakuwa upande wa nani? Au pande zote
 
Ila unapoanzisha brand au kampuni jina nzuri nayo inachangia na inavuta wawekezaji.

Imagine harmonize aje na
Konde tv
Konde fm
Kondebet
Konde karanga

Ni ngumu hata kuvutia wawekezaji
 
Back
Top Bottom