Mwekezaji inabidi ampe Diamond takriban nusu ya faida ili kutumia jina la WASAFI lasivyo apambane kivyake

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
1637921294792.png

Diamond sio mmiliki mkuu wa makampuni kama wasafi tv, wasafi radio, wasafi bet, Diamond karanga (r.i.p), yeye nafasi yake huwa ni co-owner, anachofanya ni kuwekeza tu jina lake na kuchukua asilimia zake kwenye faida. Uhakika wa 40%-49% ya umiliki na faida upo chini yake kwa kutoa tu jina wasafi litumike kwenye kampuni.

Hata Azam Bakhresa nae hufanya hivyo Kwa kuyapa ruhusa baadhi ya makampuni kutumia jina la azam kwenye bidhaa zao kwa makubaliano ya kugawana umiliki, faida, menejment, n.k

Kuna kipindi flani wahindi waliokuwa wanstengeneza dismond karanga waliona zinauzika sana na kuingiwa tamaa , ulafi na wivu kuona kwamba Diamond hastahili mgao mkubwa kwasababu kachangia tu jina, wakati wao wametia mtaji mrefu keenye pesa, kununua mashine, n.k Diamond akaachana nao ili wapambane kivyao na wajue thamani halisi ya jina lake, Leo hii hizo karanga zipo wapi ??

Na hivi ndivyo hali ilivyo kwenye Wasafi tv na Wasafi fm, Kusaga ndie alieweka mtaji, uzoefu wake, connection zake, n.k lakini Diamond alichangia tu jina kwa maelewano kwamba atamiliki hisa zinazompa umiliki si haba, mgao wa faida mnono na pia kuwa na maaumuzi kwa kiasi mfano kuwa ceo wa kampuni.

Hata hii kampuni mpya ya kubet ya Wasafi bet, ni makubaliano baina ya kampuni ya kubeti ya nchini Kenya inayoitwa odibet, ni kampuni ambayo ingeingia hapa nchini kichwa kichwa ingepata wakati mgumu sana kufahamika na kuoata wateje, kwa hiyo wameamua kutumia shortcut kwa kutumia jina kubwa la Wasafi kwa makubaliano ya mgao katika umiliki, faida, usimamizi, n.k.

Take it or leave it

Hongera sana Diamond
 
Wasafibet ni tawi la odibets kutoka kenya... Ilianza mwaka 2018, na ina ofisi nyingine ghana. Kwa tanzania wamemake partinership na diamond...

Kwahiyo diamond ni co-owner wa wasafibet kibongo
Yes, ni kweli, kuna makubaliano hapo kwamba kuna mgao wa maana tu kwa Diamond,
 
Diamond huwa anakuwa silent partner, yeye anachofanya ni kuwekeza tu jina lake na kuchukua asilimia zake kwenye faida.

Mfano leo hii mtu akitaka kuanzisha mabasi yake na hana jina, anaweza kuyafanya mabasi yake kuwa maarufu kwa kutumia jina la wasafi kwa maelewano kwamba faida iwe pasu kwa pasu.
Diamond hata akipata 10% kwenye biashara ya kamari kawin. Huu mziki ulivyo unapo vuma ndipo kipindi cha kupiga hela. Kipindi hiki kikipita benki acc inacheka,una vitega uchumi kibao, unatulia unafanya mambo mengine.
 
Diamond huwa anakuwa silent partner, yeye anachofanya ni kuwekeza tu jina lake na kuchukua asilimia zake kwenye faida.

Mfano leo hii mtu akitaka kuanzisha mabasi yake na hana jina, anaweza kuyafanya mabasi yake kuwa maarufu kwa kutumia jina la wasafi kwa maelewano kwamba faida iwe pasu kwa pasu.
💪🏿
 
Ila sisi wa kubeti hatuangalii jina, tunaangalia vitu kadhaa. na ndio maana wabetiji kibao wanaacha kampuni kibao za hapa na kubeti za ulaya na urusi huko.
1. Hatutaki kulipa kodi kwa sababu hatusaidiwi hata kidogo na TRA kutafuta odds.

2. Tunataka customercare nzuri coz kubeti ni kazi ngumu nyie! we unafikiri kubashiri mambo yajayo kwa usahihi wakati huna taaluma ni kazi rahisi!

3. Urahisi wa kuwithdraw na kudeposit.

4. Hatutaki kubaniwa option.
 
Mkuu kama huwezi, Mlango upo wazi, hakuna anekulazimisha, kwani tatizo lipo wapi.

View attachment 2024018
Hata hizo hisa za wasafi Tv hakutoa jina tu, alitoa pesa pia na aliwahi kusema wakati wanaanzisha alikuwa anatumia milioni 100 kwa mwezi. Hiyo m. 100 inaweza kuwa ni uongo lakini inaonesha kwamba alitoa fungu na yeye.
Unachosema hapa ni biashara kichaa hakuna anaeweza kutoa 45% kwa jina tu. Wewe unaweza kutoa 40% kwenye biashara yako?
 
Hata hizo hisa za wasafi Tv hakutoa jina tu, alitoa pesa pia na aliwahi kusema wakati wanaanzisha alikuwa anatumia milioni 100 kwa mwezi. Hiyo m. 100 inaweza kuwa ni uongo lakini inaonesha kwamba alitoa fungu na yeye.
Unachosema hapa ni biashara kichaa hakuna anaeweza kutoa 45% kwa jina tu. Wewe unaweza kutoa 40% kwenye biashara yako?
Mkuu umekunywa chai?? 😂😂
Hebu pitia hapo kwa mama kimbo akupe chapati mbili na maharage, baadae ntapitia kulipa .

Wacha watu wanaojua biashara watumie fursa ili mradi kuwe na faida
 
Back
Top Bottom