Kwanini tunalipwa mgao wa shilingi inayoshuka thamani kutoka kwenye migodi yetu badala ya kuchukua dhahabu isiyoshuka thamani?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Dhahabu ni pesa isiyoshuka thamani,tangu kuumbwa kwa dunia,dhahabu haijawahi tetereka katika soko la dunia,tukisubiri kugawana pesa baada ya hesabu wajanja watatangaza hasara,na kwa nini pesa na si dhahabu isiyoshuka thamani, tubadili sheria, tugawane Gold Bars(vitofali),Wazalendo wa nchi hii Wakili Boniface Mwabukusi, Mh Luhaga Mpina, Profesa Shivji, Maria Sarungi, Dkt Wilbroad Slaa, Askofu Mwamakula, Freeman Mbowe, Mdude Nyagali, Chadema, Sauti ya Watanzania na Wazalendo wote hii ndio ajenda ya kuiongeza na kwenda nayo baada ya Okoa bandari Katiba Mpya, tukifanya hivyo,hatutakuwa chawa wala hatutashangilia tena kukopeshwa 1.5 trillion kujengea madarasa na vyoo!!

Wakati Botswana wakipiga breki kumuangalia Rais John Pombe Magufuli akipambana kuzuia mchanga wa Makinikia mwaka 2017 walidhani angeendelea kuwepo na kufikia kuanzishwa mara moja mgawanyo wa mali na si pesa katika mikataba yote kupewa mgao wa vitofali vya dhahabu,vito, almasi, nickel, helium, magogo, gesi, mafuta, kilimo cha mashamba makubwa ya wawekezaji na petrol ni mgao wa mali kwa mali badala ya tarakimu za kwenye balance sheet ambazo kuna makandokando mengi,na mgawanyo uwe unakwenda serikali kuu, pia halmashauri za wilaya ambapo mgodi upo mfano Geita ili wananchi wachague maendeleo wanayoona ni kipaumbele kwao yaweze kuwa ni barabara za zege / mawe, hospitali, shule, maji safi ya bomba, umeme Tanzania n.k na siyo kununua gari la kifadhari la V8 la mkurugenzi wa Halmashauri n.k lakini bahati mbaya Hayati Rais John Pombe Magufuli hayupo tena,na Rais wa Botswana aliweka wazi kwenye hotuba yake siku ya mazishi ya Hayati Rais John Pombe Magufuli, alisema "Watanzania,You have a big shoes to wear after the departure of President John Pombe Magufuli".

Julai 2023 nchi ya Botswana ilipata jibu lake kwenye maliasili zake Botswana itapata mara moja asilimia 30 ya mawe machafu (almasi ambayo bado kuchongwa) yaliyochimbwa, kutoka asilimia 25, na itapanda hadi asilimia 50 ndani ya muongo mmoja,Kampuni ya De Beers na maafisa wa serikali kwa pamoja walitangaza jambo hilo, makubaliano haya kwa Tanzania yangekuwa hivi, kwa kila lmkataba wa mgodi kati ya Tanzania na mwekezaji wagawane vitofali vya dhahabu na serikali badala ya kusubiri faida ya kwenye balance sheet, Mgawanyo wa vitofali au almasi au tanzanite inaipa uhuru Tanzania kuhifadhi kitu halisi na kukiuza kwa thamani ya uhakika bila makando kando ya kusubiri mwekezaji asafirishe madini yote nje na mwisho wa siku akuambie faida ni ndogo kama ripoti yake ya katika mahesabu ya mwaka yanavyoonesha.

Zimbabwe imetengeneza sarafu ya Dhahabu yenye thamani sawa na USD 900 baada ya pesa Yao kutoimarika, sisi Watanzania tumebinafsisha migodi yetu, wachimbe dhahabu halafu watupe pesa kwenye makaratasi, tena kwa makadirio na wakati mwingine wanatangaza hasara na kubadili majina ili kukwepa,Napendekeza kuwa waagizaji wa mafuta waweze kutumia dhahabu kama njia ya malipo kununua mafuta. Pendekezo hili linaweza kutekelezwa kwa kushirikiana na taasisi na vyama vinavyohusika na sekta hii, kama vile EWURA, Chama cha Waagizaji na Wasambazaji Mafuta Tanzania, Wizara ya Madini, Chama cha Wanunuzi na Wauzaji Madini Tanzania (TAMIDA), PBPA, na Wizara ya Nishati.Waagizaji wa mafuta wanaweza kutumia dhahabu kama njia ya malipo kununua mafuta nje ya nchi kwenye soko la kimataifa.

Mafuta yakiuzwa nchini, shilingi zitakazopatikana kutokana na mauzo ya mafuta zinaweza kutumika kununua madini ya dhahabu hapa nchini,baada ya kununua dhahabu,waagizaji wa mafuta wanaweza kubadilisha dhahabu hiyo na dola kwenye soko la kimataifa,dola zilizopatikana zinaweza kutumika kununua mafuta ya petroli, dizeli, na bidhaa zingine za mafuta kutoka nje ya nchi kwenye soko la kimataifa.

Nimalizie kwa tafakuri na maoni yafuatayo,tuweke wazalendo kwenye kila mgodi pale jikoni vinapotengenezwa vitofali yaani gold bars, moja letu,moja lao mwanzo mwisho,kwa kufanya hivyo,nchi ingepata vitofali vingapi kwa siku? ni dhahabu kiasi gani inapelekwa nje ukizingatia wanafanya kazi day and night?kwanini Stamico haisitishi vibali vya utafiti na uchimbaji madini yetu kwa makampuni ya nje Ili yenyewe iunde na kusimamia migodi itayochimba dhahabu yetu na tukapata share kubwa zaidi? kwanini Benki kuu isianzishe sarafu ya dhahabu yenye ubora wa kimataifa ili kuimarisha currency yetu ya Tshs,kwani madini yetu Mungu alitupa tuwagawie majirani au tulipewa yatutajirishe,Watoto wanakaa chini wakati Dhahabu yetu inaenda kutajirisha wageni ambao hawakujaliwa raslimali hizo!

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Maokoto hiki ni kipindi kuelekea uchaguzi mkuu sasa nimuda wa kila mwenye nafasi kula kwa urefu wa kamba yake!

Tanganyika itarudi ikiwa imechoka sana.
 
Nilileta Uzi humu wenye maudhi kama haya usemao:

"Kama Dhahabu ni pesa,iweje tupokee mgao wa makaratasi Badala ya dhahabu?"- Rabbon.

Ilikuwa Sept 13.
 
Back
Top Bottom