Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?
Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?
Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?
Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?
Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?