Mwanaume, kutojiamini ndo adui yako mkubwa kwenye mahusiano na sio pesa wala mwanamke. Kwanini?

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Kutojiamini inajionesha kwenye tabia yako.

Hata kama ulijificha lakini matendo yako yataonesha tu hujiamini. Na kama ulipata mwanamke anaweza kukuacha au kukusaliti. Sababu unaonesha tabia za kutojiamini.

Kwanini wanawake wanawaacha watu wasio jiamini? Kwanini kutojiamini ni adui yako mkubwa?

Kwasababu kutojiamini ni tabia ya kike. Ye anahitaji mtu anayejiamini ili awe mwamba kwake. Awe msingi kwake ili hata akiwa na hisia tofauti tofauti anajua ana mtu anayeweza kumuongoza/ kumtegemea.

Ila usipojiamini, mwanamke ni rahisi kukuendesha.

Kukuendesha sio tu kwamba akikuambia kitu unafanya. Hapana. Bali hata kimawazo anaweza kukuendesha pale unapompa nafasi kubwa.

Kukuendesha kimawazo, kama vile kuogopa kumkosea, kufanya vitu ukiwaza atakufikiriaje, kumuweka kama jaji wako, kumuwazia utamrudishaje/ utamvutiaje/ utapataje penzi toka kwake. Yani unamfukuzia kupita kiasi na upo tayari kufanya lolote kwa ajili yake.

Na akiona anaweza kukuendesha hatojisikia amani kujiachia kwako.
Wala hatokua na hisia za mapenzi na wewe tena.

Kutojiamini kunajionesha ukiwa na tabia hizi;
  • Kuwa na wivu uliopitiliza,
  • Kumuuliza maswali mengi mno,
  • Kuhisi atakuacha muda wowote,
  • Kumtegemea yeye kihisia na kimawazo,
  • Kumng’ang’ania na kumfukuzia kupita kiasi,
  • Kuogopa kufanya maamuzi (magumu/ rahisi) ukihofia atakataa,
  • Kujihisi huna usalama kwenye ndani yako kwa kuwa naye kwenye mahusiano,
  • Kumtegemea yeye aongoze mahusiano, (ukiona huchukui hatua unasubiria mwanamke aanzishe kitu ujue unaangukia hapa).

Jitahidi ubadilishe hayo na ujiamini katika kile unachompa mwanamke, muda wako na uwepo wako.
Kuwa na maamuzi na uongoze jahazi lenu.

Na chanzo kikubwa cha mahusiano kuyumba, kuvunjika au mwanamke kuchepuka ni mwanaume kutojiamini au kutokua na maamuzi au kaacha uongozi kwenye mahusiano.

Jiamini Sasa Kwa Unachompatia Mwanamke, Usimamie Uongozi Wako Kwenye Mahusiano na Uwe Na Wiki Njema Yenye Baraka.
.
Share Na Wengine Wapate Kujifunza.
 
Kama huna chapaaa hio confidence unaipata wapi?????
Hakuna kitu kibaya kama combination ya ujinga na confidence
 
Back
Top Bottom