Mwanaume, kitu muhimu kwenye Mahusiano ni kumuongoza Mwanamke

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Kama kuna kitu hujajifunza basi kitu pekee ukichukue ni uongozi. Muongoze mwanamke tangu unamsalimia ‘mambo’ hadi mkiwa kitandani. Na kama unaendelea naye na mahusiano, endelea kumuongoza hadi pale kifo kitawatenganisha. Ukiacha kumuongoza ndo mazoea huanza.

Wote mnakosa hamu ya kimapenzi kwa mwenzi. Wote hamtojisikia wazima kwenye mahusiano. Haijalishi una pesa kiasi gani.

Mahusiano yanakua ya kuvumiliana tu kwa sababu tofauti tofauti badala yawe furaha.

Mwanamke anataka kitu kimoja tu, kufurahi. Kwa kumuongoza utampunguzia mawazo, majukumu na lawama na utamfanya ajiachie kuwa nawe. Na atakua na furaha.

Wanakupa ishara tu za mvuto, kazi yako ni kuzisoma na kumuongoza. Hatotaka kuongoza chochote ili asionekane mchonganishi, asipate lawama, asionekane malaya kwa kujiachia kwako, au asionekane mbaya ili mwisho wa siku awe na cha kujitetea.

Kitu pekee mwanamke anaweza kuongoza mahusiano ni atayaongoza muwe marafiki, au wapenzi msio na mapenzi na utaishia kumlaumu akupi raha au kuvunja mahusiano.

Akikumisi tengeneza mazingira ya kukutana na kufurahi pamoja, sio kujadili alivyokumisi kama mwanamke mwenzake. Akikubali umvue nguo, ongoza njia hadi mfike kileleni, sio ukae kusubiri ruhusa yake kufanya kitu.
Akikwama muongoze kimawazo na kama utaona sawa kumsaidia kifedha. Akikubali kuongea nawe ongoza mawasiliano, sio ukae usubiri aanzishe mada yeye. Akikubali uwe na mahusiano naye, yaongoze mahusiano, sio ukae kusubiri akuambie mfanyaje.

Achana na habari ya usawa kwenye kuongoza mahusiano.
Kadri unavyoongoza ndivyo unaongeza uwezekano wako wa kufanikiwa kwenye mahusiano.

Na akikataa kuongozwa nawe basi amepoteza nafasi ya kuwa na mtu ambaye angempatia furaha. Nenda kampe nafasi hiyo mwingine.

Jinsi ya kujua umuongozeje.
Inaanza kwako kwa kujua unachokitaka.
Jiulize “unataka matokeo gani ukiwa naye?”
Jibu lako litakuambia umuongozeje. Kisha ujue kwa kila hatua unayokua na mwanamke ufanye nini. Itakusaidia ujue unafanya nini kwa kila hatua mnayopiga. Kumbuka. Hata kama mmepiga hatua kiasi gani, bado mwanamke anataka umuongoze akufuate.

Ukijidanganya kuwa mmefika mbali, umuachie, au upumzike atapunguza upendo haijalishi mna muda gani.

Hivyo, panga mwenendo mzima wa furaha yenu.

Jitahidi uwe jasiri na usimuogope mwanamke.
Uoga huondoa ujasiri. Ukimuogopa/ kuogopa hutopata matokeo itakufanya usiwe mkweli, yani maneno yako na matendo havitaendana. Utamkosa.

Wengine wanaogopa mwanamke mwenye iPhone, wengine wanaogopa wanawake wenye elimu au fedha. Usiwe hivyo. Ni watu wa kawaida tu.

Usiogope kumpoteza.
Usipoogopa kumpoteza hautakua na wasiwasi wa matokeo. Japo unajua matokeo unayotaka lakini ufurahie mchakato kwanza. Mchakato mzima wa mapenzi. Ukifurahia mchakato mzima wa mahusiano utapata urahisi zaidi kuliko kukimbilia matokeo. Na mwanamke anapenda hivyo zaidi. Hata wewe utajifunza zaidi.

Muhimu ujue, mwanamke muda wowote anabadilika, uwe tayari kwa hilo na lisikubabaishe ukaanza kumuomba awe nawe.

Usipindishe mambo.
Jiamini katika unachokitaka. Fanya unachokitaka, bila kuficha nia yako. Mwanamke atakua hana jinsi. Na yeye ataamini katika unachokitaka. Ila ukizunguka zunguka, hueleweki unataka nini utaonekana hujiamini/ huna uwezo wa kuongoza.

Usimfanye mwanamke akuambie, “ongea ueleweke” au kitu kama iko. Akikuambia ivo ujue thamani yako imeshashuka. Nyoosha maelezo/ nia yako na usiogope vipingamizi vya mwanamke bali vishinde.

Kadri unavyonyoosha mambo unajipunguzia mawazo. Unajipunguzia kumnyenyekea mwanamke kwa kuficha nia yako.

Ukifanikiwa hayo, utamuongoza mwanamke kirahisi.
 
Ongoza huku huna hela kenge wewe

Kama unafikiri kuongoza kitu/mtu inabidi uwe na pesa umefahulu kwenye wazo lako ila ukweli wa uongozi sio pesa

Kama amezifata pesa kwako inabidi afate maelekezo kutokana na pesa zako na kama ulipokea mahali au wewe mwanamke ndio umetoa mahali utaelewa kitu hapo
 
Kumwongoza mwanamke ni rahisi sana hasa ukimfaham. Ongeza pia MFANYE AKUONE OIMBILIO yaani awe na uhuru wa kukirleza hisia zake muda wowote jitahidi sana kumsikiliza haijaloshi wwwe uko busy kiasi gani
 
Moja ya uzi muhimu sana. Ila wanaume wa Dar hawauoni kabisa. Wanajadili tu namna ya kufanya uzinzi kimasihara.
 
Nowdays wanaume hatujui saikolojia ya mwanamke na mahusiano ndo maana kilio kinazidi kuwa kikubwa
 
Back
Top Bottom