Adui yako si Mwanamke. Adui yako huyu hapa

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,697
Ebu jaribu kuvuta picha, upo kwenye bustani ambayo wewe ndiye mlinzi na mtawala. Bustani ambayo, simba na wanyama wote wanakutii, wanaitikia uwaitapo kwa sababu wewe ndiye sababu ya wao kupata majina yao, hivyo, hata yule aliyekuumba ameheshimu maamuzi yako.

Ghafla yule aliyekuumba akaona uzito wa kazi yako, upweke wako ukamfikia, licha ya kupendezesha bustani aliyokupa kwa maua mazuri na mito yenye maji safi, ila hakuuona uzuri wake, akaamua kukupa usingizi mzito, ili toka ubavuni kwako apatikane atakayefanana na wewe. Akakupa msaidizi, mfariji na rafiki; lakini awali alikupa majukumu yaani; kulinda na kutunza bustani, na ikiwa utachoka, ubavu wako utakufariji, kukuliwaza, yaani mwanamke. Ni raha, asikwambie mtu, ila kwa bahati mbaya, raha hii aliisikia mwanamume mmoja tu duniani. Adam. Ambaye naye hakudumu nayo. Yule ibilisi aliyemlaghai Mwanamke, hakuwa anamtafuta Mwanamke, bali alikuwa anamtafuta Mwanamume kupitia Mwanamke. Hivyo, mlengwa ni Mwanamume.

Badae tulipokea huruma ya Mungu, tukapewa mitume, manabii na walimu. Unadhani adui yetu atapenda? Ngoja nikwambie, ziliposimama dini zote, zilimpa nguvu Mwanamume. Namaanisha ZOTE!! Adui yetu hapendi. Hata leo hii.

Unaweza kujiuliza, kwanini wanawake wanajaza makanisa lakini ndio hao wanajaza nyumba za waganga? Jibu ni rahisi, hawawezi kusimama peke yao kiroho na kama hujui hakuna mwanamke mwenye msimamo. Yeye husimamiwa kile kilichoasisiwa na kupandikiza rohoni mwake, ndio mana aneweza kumsikiliza mchungaji na mganga kuliko wewe. Hawa wamewekeza na kuikamata roho yake. Upo?

Nakuibia siri moja kwenye somo la Consuming Psychology, hii ni Saikolojia ambayo kwenye upande wa biashara inatumika kutengeneza wateja. Watu hununua bidhaa na huduma sio kwa akili zao, bali hisia (emotions) na wanawake ndiyo wateja wazuri kwa sababu ni dhaifu kihisia. Kwani si ulimtongoza? Yaani ulimshawishi! Sasa inashindikanaje asishawishike na wanaume wengine? USIOGOPE ni hivi.

Adui yako ni Globalists; hawa ni Mabepari ambao maslahi yao yanatawala dunia nzima, yawe kibiashara au kisiasa, na wao ndio wanao control mfumo wa fedha duniani, na ndio mana wanaweza kuishawishi serikali yako kufanya lolote; kikwazo pekee cha wao kutawala ni sisi wanaume, kwa sababu, kila mwanamume anataka mamlaka. Kumbuka alipewa kule awali, kulinda, kutunza na kuamua majina. Mbinu ni ile ile na haijabadilika, ili wakupate wewe, lazima wamtumie mwanamke. Kwao mwanamke sio tatizo. Kwani si unamkumbuka Dellila? Mke wa Ayubu? Hawa? Hawa kwao si tatizo, kwa sababu Mungu hakai nao, anakaa na wewe, ndio mana wao wanatumia nguvu kubwa kumtafuta kuliko wewe. Kwanza wewe mara ya mwisho kwenda kwenye nyumba ya ibada ilikuwa lini? Na wewe unadhani Mungu alikuwa wapi wakati hawa anapigwa sound?

Skia, huko Magharibi kuna watu wamewekeza kiasi cha $798 m-$1.4bn kwenye video za maudhui ya ngono (x) halafu wakakuacha wewe uangalie bure; ni nani huyu asiyetaka hela yake? Watakuja watu kukwambia wanazipata kupitia matangazo, basi nikwambie unapodhoofika wewe ndio mwanzo wa kufa kwa ndoa ambamo wewe ndiye kiranja. Kuanguka kwa ndoa ni mabilioni ya dollar. Kwanza utaingia kwenye emotional freezing, Utawatumia tu wanawake, watakosa kiranja, wataanza kurandaranda. Eeh!! Piga mchungaji tu, kondoo watatawanyika; watu watapiga hela kupitia mauzo ya dildos, vibrators, sex toys; na kwa kuwa sasa hivi unamuona mwanamke kama chombo cha ngono, fashion industry itampamba kwa kila aina ya nguo ya kukuvutia, watu watauza cosmetics za kutosha! Hivi unajua lipstic na wanja vilitumika Misri ya kale kama kiashiria cha Mwanamke aliye tayari kufanya tendo kwa mumewe? Naam! Kale kadude kana nguvu bwana. Pole sana.

Wakaona huko hapatoshi, wakakupiga na Feminism! Uliambiwa feminism ina uhusiano na gender equality? Basi umedanganywa, feminism inahusu women empowerment, lengo kuu ni “power” kumpa mamlaka mwanamke, na si usawa. Hakuna usawa kwenye mamlaka. Kupitia feminism hakuna ndoa itakayodumu, humu mitandaoni mnakutana na waraibu wengi wa ngono wanaojiita feminists. Poleni; ingawa, wengine ni wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia unaotokana na kundi la wanaume wasioweza kuwa viranja na kusimamia mamlaka yao ipasavyo. Kwani unadhani ni wajinga kuondoa elimu ya Jando na Unyago iliyokuandaa kuwa baba/mume bora? Ona leo na ma digirii yako ya procurement and supply lakini hujui hata namna ya kuwa baba tu.
 
Adui wa mwanaume si globalists wala mwanamke kwenye mahusiano, ni mwanaume mwenyewe.
Globalists hawakuchagulii mwanamke, unajichagulia mwenyewe, tena bila ushauri, so matokeo yeyote ya mahusiano yanatokana na uchaguzi wako na huna budi kuyapokea na eidha upambane nayo au uachane nayo.
 
Nakubaliana nawe kwa asilimia kubwa mnoo.
Kiimani Kuna misingi tumeiacha ndio tatizo lilipoanza, mie naimani na mungu yupo, hivyo naamini tungeishi wote katika misingi aliyotuwekea yeye nahisi dunia ingekuwa sehemu salama saana, ila ndio hivyo mtaalam ibilisi alishaahidi kuwa atawapata wa kuingia nae motoni, so hili jambo limeanzia mbali mnooo
 
Adui wa mwanaume si globalists wala mwanamke kwenye mahusiano, ni mwanaume mwenyewe.
Globalists hawakuchagulii mwanamke, unajichagulia mwenyewe, tena bila ushauri, so matokeo yeyote ya mahusiano yanatokana na uchaguzi wako na huna budi kuyapokea na eidha upambane nayo au uachane nayo.
Unajichagulia mwanamke kwenye ulimwengu ambao Globalists wame manipulate mifumo ya mila ku profiteer biashara?
Come on bro!!
 
Bro, hata kama kuna mchafuko, wasafi wapo. Ni jukumu lako kufanya uchunguzi kabla ya kuingia mzimamzima.
Wanaume wasio malaya wapo, na wanawake wasio malaya wapo.
Either hutak hoja yako ikataliwe au unapiga kwa sababu hujamuelewa....ye kamaanisha mfumo ndo unaongoza, unampa nguvu mwanamke ili iwe rahis kucontrol dunia kama mpango wao ulivyo...ni kama leo ulalamike kiongoz fulan mbovu huku wazur wapo. Maslahi yao yapo kwa hao wabaya kwako na ndo wazuri kwao.
 
Ahsante kwa kunisaidia, Brother
 
Ebu jaribu kuvuta picha, upo kwenye bustani ambayo wewe ndiye mlinzi na mtawala. Bustani ambayo, simba na wanyama wote wanakutii, wanaitikia uwaitapo kwa sababu wewe ndiye sababu ya wao kupata majina yao, hivyo, hata yule aliyekuumba ameheshimu maamuzi yako.
Hubrus.., yaani hii kitu ndio inatumika kwa baadhi ya watu matabaka fulani kuwatawala wengine kwamba sisi ndio tuna hati miliki ya kuwatawala wengine hii ni kutokea kwenye Binadamu na viumbe wengine; jinsia hata mataifa tofauti (kwamba sisi tuna akili kuliko wao hivyo tuwatawale)
Ghafla yule aliyekuumba akaona uzito wa kazi yako, upweke wako ukamfikia, licha ya kupendezesha bustani aliyokupa kwa maua mazuri na mito yenye maji safi, ila hakuuona uzuri wake, akaamua kukupa usingizi mzito, ili toka ubavuni kwako apatikane atakayefanana na wewe. Akakupa msaidizi, mfariji na rafiki; lakini awali alikupa majukumu yaani; kulinda na kutunza bustani, na ikiwa utachoka, ubavu wako utakufariji, kukuliwaza, yaani mwanamke.
Kwamba hakujua hapo mwanzo ? Yaani alikuwa anafanya na kuangalia outcomes ni zipi ? na kama hivyo ndivyo na kesho anaweza kubadilika kutokana na mazingira ? (Sasa ili ya kwamba kila kitu kimpengwa kuanzia mwanzo ni uongo)
Ni raha, asikwambie mtu, ila kwa bahati mbaya, raha hii aliisikia mwanamume mmoja tu duniani. Adam. Ambaye naye hakudumu nayo. Yule ibilisi aliyemlaghai Mwanamke, hakuwa anamtafuta Mwanamke, bali alikuwa anamtafuta Mwanamume kupitia Mwanamke. Hivyo, mlengwa ni Mwanamume.
Opposite attract na hio raha ipo na itaendelea kuwepo sababu ya propagation..., iwe kwa wanyama au binadamu nature imefanya hivyo uwepo mvuto ili species zivutane zizaane na kuwa chakula cha species nyingine (ecosystem).., Kwamba mlengwa mwanaume ili iweje ? Kuna Mwanaume bila ya kuwepo mwanamke?
Badae tulipokea huruma ya Mungu, tukapewa mitume, manabii na walimu. Unadhani adui yetu atapenda? Ngoja nikwambie, ziliposimama dini zote, zilimpa nguvu Mwanamume. Namaanisha ZOTE!! Adui yetu hapendi. Hata leo hii.

Unaweza kujiuliza, kwanini wanawake wanajaza makanisa lakini ndio hao wanajaza nyumba za waganga? Jibu ni rahisi, hawawezi kusimama peke yao kiroho na kama hujui hakuna mwanamke mwenye msimamo. Yeye husimamiwa kile kilichoasisiwa na kupandikiza rohoni mwake, ndio mana aneweza kumsikiliza mchungaji na mganga kuliko wewe. Hawa wamewekeza na kuikamata roho yake. Upo?
Hao wachugaji wote ni wanawake ? Au sasa kama hakusikilizi wewe mwanaume na anamsikiliza mchungaji mwanaume au mganga mwanaume au mwananamke huoni logically ni contractions tupu kwenye maelezo yako ?
Nakuibia siri moja kwenye somo la Consuming Psychology, hii ni Saikolojia ambayo kwenye upande wa biashara inatumika kutengeneza wateja. Watu hununua bidhaa na huduma sio kwa akili zao, bali hisia (emotions) na wanawake ndiyo wateja wazuri kwa sababu ni dhaifu kihisia. Kwani si ulimtongoza? Yaani ulimshawishi! Sasa inashindikanaje asishawishike na wanaume wengine? USIOGOPE ni hivi.
Kudhania kwamba unaweza kummiliki binadamu mwenzako mwenye akili zake, tamaa na madhaifu nadhani ni kuishi kwenye dunia ya kusadikika..., wewe enjoy the moment na kama leo mpo naye na amekushiba haimaanishi kesho lazima awe nawe na akushibe (huyo sio mwanaserere kwamba unammiliki) na kiumbe chenye tamaa na madhaifu kama wewe mwenye ulivyo na madhaifu na kesho unaweza kumwacha mke wako na kwenda pengine
Adui yako ni Globalists; hawa ni Mabepari ambao maslahi yao yanatawala dunia nzima, yawe kibiashara au kisiasa, na wao ndio wanao control mfumo wa fedha duniani, na ndio mana wanaweza kuishawishi serikali yako kufanya lolote; kikwazo pekee cha wao kutawala ni sisi wanaume, kwa sababu, kila mwanamume anataka mamlaka. Kumbuka alipewa kule awali, kulinda, kutunza na kuamua majina. Mbinu ni ile ile na haijabadilika, ili wakupate wewe, lazima wamtumie mwanamke. Kwao mwanamke sio tatizo. Kwani si unamkumbuka Dellila? Mke wa Ayubu? Hawa? Hawa kwao si tatizo, kwa sababu Mungu hakai nao, anakaa na wewe, ndio mana wao wanatumia nguvu kubwa kumtafuta kuliko wewe. Kwanza wewe mara ya mwisho kwenda kwenye nyumba ya ibada ilikuwa lini? Na wewe unadhani Mungu alikuwa wapi wakati hawa anapigwa sound?
Hao ma-globalist wanakutana wapi na kupanga sera zao wapi ? Yaani wewe kudhani kwamba kuna some individuals wanaweza kutawala na kuchezesha wanadamu wote wakati wote kama mwanaserere ni kumpa binadamu a lot of credit..., no one can control the outcomes hata kama wangeweza kwa faida ya nani, ukizingatia sio kwamba kuna mtu ataishi milele kwahio anachowekeza leo ni kwa ajili ya nani ? Maiti yake kaburini
Skia, huko Magharibi kuna watu wamewekeza kiasi cha $798 m-$1.4bn kwenye video za maudhui ya ngono (x) halafu wakakuacha wewe uangalie bure; ni nani huyu asiyetaka hela yake? Watakuja watu kukwambia wanazipata kupitia matangazo, basi nikwambie unapodhoofika wewe ndio mwanzo wa kufa kwa ndoa ambamo wewe ndiye kiranja. Kuanguka kwa ndoa ni mabilioni ya dollar. Kwanza utaingia kwenye emotional freezing, Utawatumia tu wanawake, watakosa kiranja, wataanza kurandaranda. Eeh!! Piga mchungaji tu, kondoo watatawanyika; watu watapiga hela kupitia mauzo ya dildos, vibrators, sex toys; na kwa kuwa sasa hivi unamuona mwanamke kama chombo cha ngono, fashion industry itampamba kwa kila aina ya nguo ya kukuvutia, watu watauza cosmetics za kutosha! Hivi unajua lipstic na wanja vilitumika Misri ya kale kama kiashiria cha Mwanamke aliye tayari kufanya tendo kwa mumewe? Naam! Kale kadude kana nguvu bwana. Pole sana.
Wewe enjoy maisha kwa wakati huu Sex has always sell and will always sell unaongelea kwamba unaachiwa uangalia ngono bure ? umeambiwa yule actor na mwenye hati miliki ametoa kazi yake bure au ni piracy ? Kwamba anayekupa ngono bure ili uje ununue dildo ni yule yule ? Ni kampuni moja ? aisee nadhani unatatizo la kufanya ovesimplification na bila kuangalia the whole equation....

Wakaona huko hapatoshi, wakakupiga na Feminism! Uliambiwa feminism ina uhusiano na gender equality? Basi umedanganywa, feminism inahusu women empowerment, lengo kuu ni “power” kumpa mamlaka mwanamke, na si usawa. Hakuna usawa kwenye mamlaka. Kupitia feminism hakuna ndoa itakayodumu, humu mitandaoni mnakutana na waraibu wengi wa ngono wanaojiita feminists. Poleni; ingawa, wengine ni wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia unaotokana na kundi la wanaume wasioweza kuwa viranja na kusimamia mamlaka yao ipasavyo. Kwani unadhani ni wajinga kuondoa elimu ya Jando na Unyago iliyokuandaa kuwa baba/mume bora? Ona leo na ma digirii yako ya procurement and supply lakini hujui hata namna ya kuwa baba tu.
Kwamba wao wanapitia mlango wa kumshusha mwanaume ili wapige pesa (sijui wao ni wanawake) alafu wewe unatumia mlango gani ili upige pesa ungekuwa unatoa Elimu kitabu chako ungekiuza ?

Anyway to each his/her own...., ila nadhani ni mawazo myopic kwa binadamu kama specie kuona kwamba nusu (actually zaidi ya nusu) ya binadamu wote ni inferior na wanahitaji kutawaliwa..., (That is backward thinking) and that is spoken from a man with no bias
 
Hubrus.., yaani hii kitu ndio inatumika kwa baadhi ya watu matabaka fulani kuwatawala wengine kwamba sisi ndio tuna hati miliki ya kuwatawala wengine hii ni kutokea kwenye Binadamu na viumbe wengine; jinsia hata mataifa tofauti (kwamba sisi tuna akili kuliko wao hivyo tuwatawale)

Kwamba hakujua hapo mwanzo ? Yaani alikuwa anafanya na kuangalia outcomes ni zipi ? na kama hivyo ndivyo na kesho anaweza kubadilika kutokana na mazingira ? (Sasa ili ya kwamba kila kitu kimpengwa kuanzia mwanzo ni uongo)

Opposite attract na hio raha ipo na itaendelea kuwepo sababu ya propagation..., iwe kwa wanyama au binadamu nature imefanya hivyo uwepo mvuto ili species zivutane zizaane na kuwa chakula cha species nyingine (ecosystem).., Kwamba mlengwa mwanaume ili iweje ? Kuna Mwanaume bila ya kuwepo mwanamke?

Hao wachugaji wote ni wanawake ? Au sasa kama hakusikilizi wewe mwanaume na anamsikiliza mchungaji mwanaume au mganga mwanaume au mwananamke huoni logically ni contractions tupu kwenye maelezo yako ?

Kudhania kwamba unaweza kummiliki binadamu mwenzako mwenye akili zake, tamaa na madhaifu nadhani ni kuishi kwenye dunia ya kusadikika..., wewe enjoy the moment na kama leo mpo naye na amekushiba haimaanishi kesho lazima awe nawe na akushibe (huyo sio mwanaserere kwamba unammiliki) na kiumbe chenye tamaa na madhaifu kama wewe mwenye ulivyo na madhaifu na kesho unaweza kumwacha mke wako na kwenda pengine

Hao ma-globalist wanakutana wapi na kupanga sera zao wapi ? Yaani wewe kudhani kwamba kuna some individuals wanaweza kutawala na kuchezesha wanadamu wote wakati wote kama mwanaserere ni kumpa binadamu a lot of credit..., no one can control the outcomes hata kama wangeweza kwa faida ya nani, ukizingatia sio kwamba kuna mtu ataishi milele kwahio anachowekeza leo ni kwa ajili ya nani ? Maiti yake kaburini

Wewe enjoy maisha kwa wakati huu Sex has always sell and will always sell unaongelea kwamba unaachiwa uangalia ngono bure ? umeambiwa yule actor na mwenye hati miliki ametoa kazi yake bure au ni piracy ? Kwamba anayekupa ngono bure ili uje ununue dildo ni yule yule ? Ni kampuni moja ? aisee nadhani unatatizo la kufanya ovesimplification na bila kuangalia the whole equation....

Kwamba wao wanapitia mlango wa kumshusha mwanaume ili wapige pesa (sijui wao ni wanawake) alafu wewe unatumia mlango gani ili upige pesa ungekuwa unatoa Elimu kitabu chako ungekiuza ?

Anyway to each his/her own...., ila nadhani ni mawazo myopic kwa binadamu kama specie kuona kwamba nusu (actually zaidi ya nusu) ya binadamu wote ni inferior na wanahitaji kutawaliwa..., (That is backward thinking) and that is spoken from a man with no bias
Had gone through, but calling my views Myopic made me realize the kind of mind entitled into this criticism, you must be an egotistic swam into discussion unconsciously.
Sijakulazimisha ukubaliane nami, or sijahubiri ownership of other being. This isn't agreeing or disagreeing phenomenon, but understanding or not understanding.

We dont preach here, we share views.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom