Mama Mdogo
JF-Expert Member
- Nov 21, 2007
- 2,976
- 2,176
zamani nikiwa bado Form 3 nilikuwa nasoma tabora boys mwaka 2004,nikaja huku dsm rikizo ya mwezi wa kumi na mbili kwa shangazi yangu aliyekuwa anaishi karibu na ubungo praza kwenye nyumba za national house.Alikuja akawa anamsimulia shangazi,kuna kesi alitoka kuisimamia kama wakiri wa serikali morogoro ilikuwa kati ya serikali na tajiri mmoja wa kihindi.Alipofika Morogoro kesho yake ndiyo kesi yenyewe alifikia guest ya kawaida alafu akajifungia ndani tu siku nzima,akawaambia wahudumu akija mtu kumuulizia aseme hamna mgeni.Basi yule Mhindi alihaha siku hiyo kila guest Morogoro akienda anamuulizia anatembea na picha yake anaenda anaulizia amefika mgeni anaonyesha picha yake.Yule mhindi alitaka amhonge kabla hawajasimama mahakamni.Mhindi alimkosa Morogoro nzima.Nayeye alilijuwa hilo,nayeye hakutaka hata kuonana naye.Kesho yake wakati wakesi mahakamani mhindi mbele ya hakimu anashangaa kumuona ghafla na ni mbele ya mahakama.Alifanya mambo kwa haki pasipo influence ya rushwa.Ni mtu wa dini sana na mpenda haki.Mimi Mwenyewe ni Graduate mwaka 2011 pale UDSM sijapata ajira ,nachukia system iliyopo ,inayoendekeza urasimu.Cake ya taifa inaliwa na watu wachache katika taifa.Viongozi wanatembea na maprado na maisha ya kifahari huku wengine wakiwa katika umasikini wa kutisha.Tofauti na wakati wa Nyerere cake ya taifa ilikuwa inagawanywa kwa watu wote kwenye taifa,Mbuge wa zamani wakati wa nyerere ukimumuona saiz huwez kuamin kama alikuwa mbuge,cake ya taifa ilikuwa inagawanywa kwa watu wote sawa.Uingereza yenyewe Siasa siyo sehemu ya kutokea ni kazi ya kujitolea.Nimeona nilisemee hili siyo kwamba namtetea.
My God, mbona hueleweki??? Unanikumbusha mambo ya Comic Ally!!!