Mwanasheria mkuu mpya wa Serikali ni dhaifu sana!

Mwanasheria mkuu mpya wa Serikali ni dhaifu sana!

Hata mimi nimemuona bungeni leo ila inawezekana ni kwasababu ya ugeni wa kuongea ndani ya bunge tu.Tumpe muda kwanza.
 
Hebu Fikiria,Unatoka kuamka Usingizini halafu cha Kwanza kukutana nacho ni kofi la Uso!Ndicho George (AG) alichofanyiwa na Lissu.Ashukuru Mungu imebaki miezi michache tu kabla ya uchaguzi,otherwise angeomba kubadilishwa
 
jamani lisu kamtia adabu huyu AG ebu cheki hii kauli
"wewe si mshauri wa bunge bali wewe ni wanasheria wa serikali"
 
huyu AG sasa atakuwa kajua kile werema alichokuwa anakumbana nacho chezea lisu wewe
 
Tundu Lissu pia leo amemuanza kuwa kumkosoa kisheria katulia kimyaaa hadi nimemuonea huruma, eti yeye ndo mshauri wa bunge, Lissu kambamiza hapo hapo, nimweupe kweli kweli kichwani
 
Huyu ag co mbaya me naona mchapakazi ila wamemzomea asubuh mpaka akapoteza consecration ya alichotaka kuongea "u just be on his shoes ungefanyaje kama n ww ungezomewa' hafu hata hujamaliza toa hoja yako
 
Mungu tunakushukuru watz kwa kutupatia zawadi ya kijana Tundu Lissu. Amekuwa sauti yetu Mungu tunakusihi umsikie. Mlinde dhidi ya maadui wa kila namna. Hapa unaweza kuelewa kwa nini jk aliwaomba wana Singida mashariki wasimpe kura za ubunge badala yake kura zake (jk) za urais wampe Dr slaa. Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki Tundu Lissu.
 
Kwa hakika huyu AG mpya ni pigo kubwa kwa watanzania.Kwa kweli amepwaya kupita kiasi!

Tangu aingie ofisini kwa mwezi sasa huwezi kuamini kama ni mwamasheria aliyeiva kiasi cha kupewa cheo kikubwa namna hiyo!

Akiitisha vikao vya kiofisi hadi unamuonea huruma! Kujieleza hajui! Kichwani anaonekana kama haijui sheria kwa kiasi kikubwa mno! Mikataba haijui vizuri kama mtu mwenye cheo cha juu serikalini!

Ikiwa hayo hayajatulia leo akaongea bungeni kwa mara ya kwanza kwenye hoja nzito! Kujieleza kukamshinda tena! Hajui kutofautisha kati ya waziri wa mambo ya nje na waziri wa mambo ya ndani! Hivi kweli Mathias Chikawe ni waziri wa mambo ya nje? Ameishia kutoa maelezo ya juu juu tu eti jambo liko mahakamani lisijadiliwe! Kwa kiwango kipi lisijadiliwe? Kweli ameshindwa kuweka vigezo vya kipi kijadiliwe na ni kipi kisijadiliwe? Mbona spika ambaye ni bush lawyer ameweza?
Miongoni mwa sifa za anayepewa cheo kikubwa kama hicho ni kujiamini na kuhakikisha makosa ya hovyo wakati wa kujieleza hayatokei! Vingine basi huo utakuwa ni udhaifu mkubwa!

Huyu AG kwa kweli ukifanya naye kikao hadi unamuonea huruma! Ni mweupe na asiyejiamini!

Huyu cheo alichopewa ni mzigo mzito kwake na watanzania hatuna siku mbili mtajionea haya ninayowaambieni leo!

Please Mods! Let's talk free!

Tafadhali pendekeza jina la mtu yeyote toka sehemu yoyote ambaye we unafikiri anafaa kuwa AG badala ya huyu.
Maana sio unalaumu tu wakati huna solution...!
 
unachosema mleda mada ni kweli kabisa hili nilikuwa najiuliza sana kiasi kwamba nashidwa kupata jibu kwa kuwa huyu alikuwa naibu tuseme jamaa alishindwa kujifunza kutoka kwa werema ila nilichojifunza hapa werema alikuwa mbinafsi alishindwa kufanya delegation of power for part time atleast minor issues

Leo Werema amekuwa mzuri? Ukistaajabu ya musa utayaona ya bavicha
 
inaelekea humjui vizuri Hugo unayemjadili ndio unaishia kumshambulia kwa hoja nyepesi na za kitoto sana. Ulizia ni kesi ngapi kazisimamia na ameshinda ? kwa tunaomjua Raisi hakufanya kosa kumchagua ni mtu makini sana na mwerevu na Nguli katika sheria

vichwa vya wanasheria wa 999ccm + 1AG MASANJU = 0.5tundu lisu
 
alivaa suti yake ikampendeza hapo tu basi!




hilo bunge la 2016 sijui litakuweje Mungu niweke hai nione
 
Na tundu lissu anawajua kuwa wote mnapewa vyeo kishkaji kichwan hamna kitu ndo maana ana wachana chana tu si mambumbu ninyi,yaani kuanzia rais na team yake nzima ya mawazir wote hawamuwez tundu lisau hata kiduchu
 
Hapana mimi nina undugu naye kwa mbali,zamani nikiwa bado Form 3 nilikuwa nasoma tabora boys mwaka 2004,nikaja huku dsm rikizo ya mwezi wa kumi na mbili kwa shangazi yangu aliyekuwa anaishi karibu na ubungo praza kwenye nyumba za national house.Alikuja akawa anamsimulia shangazi,kuna kesi alitoka kuisimamia kama wakiri wa serikali morogoro ilikuwa kati ya serikali na tajiri mmoja wa kihindi.Alipofika Morogoro kesho yake ndiyo kesi yenyewe alifikia guest ya kawaida alafu akajifungia ndani tu siku nzima,akawaambia wahudumu akija mtu kumuulizia aseme hamna mgeni.Basi yule Mhindi alihaha siku hiyo kila guest Morogoro akienda anamuulizia anatembea na picha yake anaenda anaulizia amefika mgeni anaonyesha picha yake.Yule mhindi alitaka amhonge kabla hawajasimama mahakamni.Mhindi alimkosa Morogoro nzima,kama tujuwavyo wahindi wanaongoza kwa rushwa.Nayeye alilijuwa hilo,nayeye hakutaka hata kuonana naye.

Kesho yake wakati wakesi mahakamani mhindi mbele ya hakimu anashangaa kumuona ghafla na ni mbele ya mahakama.Alifanya mambo kwa haki pasipo influence ya rushwa.Ni mtu wa dini sana na mpenda haki.Na watu wenye akiri sana siyo waongeaji sana ni watu wa action.Kwa hii thread nimejifunza kitu kimoja usimhukum mtu pasipo sababu.
 
Back
Top Bottom