Mwanamke mmoja apigwa risasi TRA jijini Arusha

Mwanamke mmoja apigwa risasi TRA jijini Arusha

Sijui hata kama unajua ulichouliza!! Kujaribu kutoa una maana gani?!

Kama alipigwa risasi wakat anatoa utasema alijaribu kutoa au alitoa?!

Btw,yote ni makosa, kutoa ama kujaribu kutoa silaha, motive yake ni mbaya na inaalika kujihami! Hiyo ndiyo sheria!

Umesikiliza Kipindi cha Nipashe Radio One asubuhi ya leo tarehe 31/10/2013?

Kama utakuwa umesikiliza vyema taarifa iliyosomwa utaelewa kwa nini nimeuliza hayo maswali...
 
Mbona ni silaha kabisa alichukua na akaikoki? Tena pistol yenyewe inamilikiwa na kigogo!!!! Hakika hana walioshuhudia ni kuwa altoa bastola. Sasa ninajua polisi wataficha jina la mmiliki kwa kuwa ni kigogo. Ingekuwa mimi hapa ungekuta wameshafika kunikamata kwa kosa la kuruhusu silaha yangu itumike na mtu asiye mmiliki. Tanzania hovyo hovyo na dhaifu na legelege tu. Ingekuwa nchi za wenzetu ungekuta kigogo ameshajiuzulu kwa kosa kubwa hili la silaha kumpa kimada.

Mkuu niliposikiliza taarifa hiyo redioni asubuhi ya leo, nilipatwa na hamaki kidogo kwa maana maelezo yao yalikuwa kama yanaegemea upande wa huyo mwanamke ingawa mtoa habari alikuwa anadai kaitoa kwa mashuhuda.

Kumbe ni kweli huyo mwanamama ni chakula ya wakubwa na fujo zote hizo alizokuwa akizifanya ni kiburi cha huyo amuwekaye mjini.

Kweli kazi ipo!!!
 
Mimi ninachokifahamu ni kuwa yule mama alitoa bastola nabkuwafuata askari mahali walipo kuhu akiwambia kama mnaringia silaha na mimi ninayo kisha akakoki, inaonekana askari alishapeleka chemba muda mrefu basi alichokifanya ni kumpa moja kapuuuu na mama wa watu chini huku damu zikimvuja

Basi mkuu wale jamaa wa Radio One inaonesha chanzo chao cha habari hakikushuhudia kwa uzuri tukio zima ndio maana taarifa yao ilikuwa inakosa nyama kama hizi...

Kwa mantiki hiyo huyo mwanamama ana kesi ya jinai ya kujibu.

Shukrani!
 
Huyo mwanamke anaonekana ana kiburi sana looooooooooo```yani wale maaskari wangeanza kwanza na kumtandika viboko; ili hayo mashauzi yamuisheeeeeeeeeee````
 
sasa tujifunze, nyumba ndogo tusiwape vitu zaidi ya uwezo wao, ona sasa tushajua hapa kumbe manati ni ya bwana kaka, kampa, du na arachuga wasivyompenda atakiona cha moto
 
Basi mkuu wale jamaa wa Radio One inaonesha chanzo chao cha habari hakikushuhudia kwa uzuri tukio zima ndio maana taarifa yao ilikuwa inakosa nyama kama hizi...

Shukrani!
Nimeipenda hiyo kapuuuuuuuuuuuuuu jomba langu la Arachuga.
 
Mzee Pindapinda alisema alisema askari wapige tuuu...

Puuuh...fyatua..piga tuuu!!!
 
Inasemekana ni Demu wa Mkuu wa Mkoa wa ARUSHA. anaitwa Violet Matheus! kama alitoa bastola na kukoki imekula kwake mazima. ila kama hakutoa bastola na walirushiana maneno tu askari akapiga risasi itakuwa soo kwa polisi. otherwise Good Job polisi pole Dada Violet Matheus.
 
Kwa wale waliopitia jeshi lolote linalotoa mafunzo ya kutumia silaha za moto,watakubaliana nami kuwa silaha sio kitu cha mzaha. Kitendo cha huyo mwanamama kuonekana na silaha tayari akili ya polisi ilimtuma nini alifundishwa. Firing pin haina mzaha ndugu zangu.
Kanuni ya silaha ni kuona kabla hujaonwa,ua kabla hujauwawa.
Pumbaf** kabisa huyo mwanamama.
Silaha nayo inautani,,.aisee
 
Huyo Askari inabidi apandishwe cheo, amefanya kazi kiweledi sana nampongeza sana.!!!
 
...Duh! Kweli 'Ushujaa' Mwingine ni Ujinga Mtupu! Yaani wewe unaona watu wameshika mi-SMG mizito hala unawafuata huku unapunga ka-Bastola kako hewani?? Kweli Ulimbukwni Huu..???!!!!:A S 39:
 
Utasikia askari kaamishwa mkoa nakushushwa cheo kama anacheo badala ya kumpongeza kwa kazi nzuri. Big up motivated afande.
 
Hivi maaskari wetu hawakufundishwa/hawafundishwi namna nyingine ya kupambana na hali ya hatari pasipo matumizi ya silaha za moto??

Ukiambiwa askari ni kazi unabisha!!!!!!

Wewe ungefanyaje kama ingekukuta hii hali????
 
Ahsante mkuu kwa taarifa,hizi pesa za ukubwani zina matatizo sana,ashukuru hajafa

Huyo mwanamke hana asili ya fedha na kazipata bila kuwa na asili nazo ndizo zinazomzuzua.

Alifikiri pesa ni kila kitu.

Kweli wadau na ndio maana wanazuoni wanasema pesa ni matokeo hivyo kama kuna interventions flani flani plus mipango ulikuwa nayo in advance kabla ya kupata pesa, once utakapokuja kuwa na hela hutozuzuka kwa kuwa tayari ulikuwa na mipango kama vile ili upate jibu lazima kuna formula na calculation umefanya na the same kwenye fedha lazima uaanzie sehemu ndipo pesa zije, sasa huyo mwanamke ni sawa na mwanafunzi amepata jibu formula ameshindwa (pesa amepata by chance) mwisho wa siku huwa watu wa design hii wanakuwa malimbukeni na dharau kibao
 
Mjanga said:
Hivi maaskari wetu hawakufundishwa/hawafundishwi namna nyingine ya kupambana na hali ya hatari pasipo matumizi ya silaha zamoto??

Ulitaka askari atumie manati?
 
Mkuu namna ilivyosimuliwa katika kipindi cha Nipashe (Radio One) inaonekana huyo mama alijaribu kutoa silaha lakini hakutoa...

Katika harakati za kutishia kutoa silaha ndipo akapigwa risasi ya begani.

Nipashe wamesimulia kwa mujibu wa mashuhuda walioona kisanga kizima.

Sasa upi ni ukweli mkuu, huyo mwanamama alitoa silaha au alijaribu kutoa silaha?

Mpwa huyo kuchapwa pini ni sawa kabisa.!!!!

Linapokuwa ni suala la defensive mtu anashoot the intention na wala hasubiri the actual movement!!!

Kuna case alikufa mtu kwa risasi ya polisi baada ya kutaka kutoa kitambulisho na polisi though the guy was reaching for the gun!!!

Ana bahati huyo dada!!!!!
 
Kwa wale waliopitia jeshi lolote linalotoa mafunzo ya kutumia silaha za moto,watakubaliana nami kuwa silaha sio kitu cha mzaha. Kitendo cha huyo mwanamama kuonekana na silaha tayari akili ya polisi ilimtuma nini alifundishwa. Firing pin haina mzaha ndugu zangu.
Kanuni ya silaha ni kuona kabla hujaonwa,ua kabla hujauwawa.
Pumbaf** kabisa huyo mwanamama.
Silaha nayo inautani,,.aisee

Halafu untrained huyu hajui hata tofauti ya CCW na Sub Machine Gun hatari sana!!!!!!
How dare she thought of her gun before uniformed officers???? Stiupid she is!!!!
Watu wanapewa silaha hawazijui wala hawajui kanuni zake???!!!!

Angekufa tu iingie kwenye kumbukumbu na iwe fundisho kwa wengine,mzazi wake wa kike atakuwa anamuombea sana huyu dada!!!!! She was supposed to be a cold meat by now!!!!
 
Jamani ndugu zangu Watanzania, tunahitaji kuongeza upana wa kuchanganua hoja. Huyu kapigwa kwa sababu ya kutoa silaha kwa nia ya kupambana na polisi wakiwa katika kazi halali. Suala la pesa, kapata ukubwani mara limbukeni, mara kanbang, jamani linatoka wapi? Unawezaje kuthibitisha kwamba ana hela ama hana? na zinahusianaje na reactions zake? Je kama ni mgonjwa wa akili? Tufike mahali tuwe na uwezo mpana zaidi wa kuchambua hoja badala ya kutoa matusi yenye mtazamo na mwelekeo wa wivu na chuki za matabaka zisizothibitishwa. Nawakilisha. Faizal usione nimeku attack. Nimetumia mchango wako kurespond hat kwenye comments nyingi zenye chuki bila uchambuzi ambazo ni nyingi tu. Nimekuchagua kwa sababu najua wewe ni mtu cool and utanielewa.
Tunamjuwa ni nani ndio maana tukaandika tuliyoandika. Wewe humjui.
 
Back
Top Bottom