Yawezekana kuna watu wachache sana hapa wanaoweza kunielewa. Naona unarudia yale yale ya uswahilini ya
Hivi unaweza kuthibitisha na kujiridhisha kwa namna gani yule mama simfaham eti wewe unamjua?
Unafahamu hata kilichoendelea nyuma ya pazia baada ya hilo tukio la hapo TRA? Anatibiwa wapi na nani anamhudumia na hali ikoje kwa ujumla?
Hata kama ni viwango, lakini ukijitahidi kutoa hoja zenye muelekeo wenye uhakiki, nadhani ni bora kwako na wadau wako pia.
Usiku mwema.
Violeth Mathias sasa alazwa ICU Na Mussa Juma, Mwananchi Posted Jumanne,Novemba5 2013 saa 24:0 AM KWA UFUPI Ni kweli huyu mgonjwa yupo ICU, mimi nipo nje ya hospitali ila
kabla ya kuondoka nilimwacha akiwa katika chumba hicho
akipatiwa matibabu Arusha.Mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite,Vailet
Matias (37), Mkazi wa Njiro
Arusha aliyepigwa risasi na
polisi Oktoba 31 mwaka
huu mkoani Arusha,
amehamishiwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi
(ICU) katika Hospitali ya
Arusha Lutheran Medical
Center inayomilikiwa na
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT). Mfanyabiashara huyo
alipigwa risasi baada ya
kudaiwa kutaka kumpiga
risasi polisi aliyekuwa
lindoni, akitumia bastola
yake kutokana na malumbano ya maegesho
ya magari. Awali alikuwa
amelazwa katika Hospitali
ya Mkoa ya Mount Meru,
akiwa chini ya uangalizi
mkali. Kaimu Mkurugenzi wa
hospitali hiyo, Dk Paulo
Kisanga alisema jana kuwa
Vailet alihamishiwa
chumba cha wagonjwa
mahututi tangu juzi kutokana na hali yake
kuwa mbaya kutokana na jeraha. Ni kweli huyu mgonjwa yupo ICU, mimi nipo nje ya hospitali ila kabla
ya kuondoka nilimwacha akiwa katika chumba hicho akipatiwa
matibabu alisema Dk Kisanga. Taarifa ya Dk Kisanga ilitolewa wakati kukiwa na uvumi wa kufariki
kwa mfanyabiashara huyo, ambao jana ulisambaa katika maeneo
mbalimbali ya Jiji la Arusha. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema jana
kuwa alikuwa hana taarifa kamili za afya ya mgonjwa huyo. Alisema awali baada ya mfanyabiashara kuegesha gari hilo mbele ya
lango kuu la kuingia katika Tawi la Benki ya CRDB, alitakiwa kulitoa
na akagoma ndipo polisi walilitoa upepo na kwamba alipokuta
limetolewa upepo ndipo alipoanza kulumbana na polisi hadi
akapigwa risasi. Hata hivyo wakati mfanyabiashara huyo akiwa mahututi, uchunguzi
wa awali wa polisi unaonyesha kuwa bastola aliyotumia ni mali yake.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Violeth-Mathias-sasa-alazwa-ICU/-/1597296/2060348/-/o3nd09z/-/index.html