Mwanamke mmoja apigwa risasi TRA jijini Arusha

Mwanamke mmoja apigwa risasi TRA jijini Arusha

Violeth Mathias sasa alazwa ICU Na Mussa Juma, Mwananchi Posted Jumanne,Novemba5 2013 saa 24:0 AM KWA UFUPI “Ni kweli huyu mgonjwa yupo ICU, mimi nipo nje ya hospitali ila
kabla ya kuondoka nilimwacha akiwa katika chumba hicho
akipatiwa matibabu” Arusha.Mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite,Vailet
Matias (37), Mkazi wa Njiro
Arusha aliyepigwa risasi na
polisi Oktoba 31 mwaka
huu mkoani Arusha,
amehamishiwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi
(ICU) katika Hospitali ya
Arusha Lutheran Medical
Center inayomilikiwa na
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT). Mfanyabiashara huyo
alipigwa risasi baada ya
kudaiwa kutaka kumpiga
risasi polisi aliyekuwa
lindoni, akitumia bastola
yake kutokana na malumbano ya maegesho
ya magari. Awali alikuwa
amelazwa katika Hospitali
ya Mkoa ya Mount Meru,
akiwa chini ya uangalizi
mkali. Kaimu Mkurugenzi wa
hospitali hiyo, Dk Paulo
Kisanga alisema jana kuwa
Vailet alihamishiwa
chumba cha wagonjwa
mahututi tangu juzi kutokana na hali yake
kuwa mbaya kutokana na jeraha. “Ni kweli huyu mgonjwa yupo ICU, mimi nipo nje ya hospitali ila kabla
ya kuondoka nilimwacha akiwa katika chumba hicho akipatiwa
matibabu” alisema Dk Kisanga. Taarifa ya Dk Kisanga ilitolewa wakati kukiwa na uvumi wa kufariki
kwa mfanyabiashara huyo, ambao jana ulisambaa katika maeneo
mbalimbali ya Jiji la Arusha. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema jana
kuwa alikuwa hana taarifa kamili za afya ya mgonjwa huyo. Alisema awali baada ya mfanyabiashara kuegesha gari hilo mbele ya
lango kuu la kuingia katika Tawi la Benki ya CRDB, alitakiwa kulitoa
na akagoma ndipo polisi walilitoa upepo na kwamba alipokuta
limetolewa upepo ndipo alipoanza kulumbana na polisi hadi
akapigwa risasi. Hata hivyo wakati mfanyabiashara huyo akiwa mahututi, uchunguzi
wa awali wa polisi unaonyesha kuwa bastola aliyotumia ni mali yake.

Violeth Mathias sasa alazwa ICU - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Hii imekaa vizuri. Haina ushabiki wala jazba.

Suala hapa ni kutokufuata taratibu na uamuzi wa violet kuchukua sheria mkononi kama vile vile ambavyo polisi na raia wamekuwa wakifanya mara nyingi.

kuna matukio mengi Polisi wamekuwa wakamataji, prosecutors na mahakimu wao wenyewe kwa wakati mmoja.

Tumejionea mara nyingi sana raia nao kwa kukosa imani na ama polisi ama mahakama, ama vyote kwa pamoja, wamekuwa walalamikaji na mahakimu hapo hapo. Kumekuwa na wimbi la upotevu wa maisha ya watu katika hizo sintofahamu.

Lakini sasa ninachokiona, ni mabadiliko ya sura na kiwango cha kutokuaminiana ambako obvious kunaelekea kuzaa hali ya kutokutambuana na kutokuheshimiana kati ya raia na vyombo hivyo vya serikali.

Tukio la violet kuamua kupambana na polisi kwa kutumia silaha, linaashiria kupoteza matumaini? Frustrations? Kukosa imani na sheria zilizopo? kuona hakuna mahali ataweze kupendekeza na akasikilizwa juu ya kuwepo mfumo anaoona ni bora zaidi? ukosefu wa elimu sahihi? muendelezo wa mahusiano mabaya kati ya polisi na raia? Kushuka kwa hadhi ya jeshi la polisi katika jamii? ulevi fulani? ama ni kitu gani?

Mimi nilishtuka sana kuona hiyo scenario. Nikaanza kufikiria hali hii isipotafutiwa ufumbuzi wa kudumu mapema, inazidi kuleta ujaasiri kwa raia kinyume na vyombo vya serikali na mwisho wake, ni maumivu kwa watu wengi.

Sijui nini kifanyike kiongozi?

Kwa sasa nasikiliza mawazo ya wachangiaji wenzangu.
 
Magesa Mlongo mkuu wa mkoa Arusha anatajwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamama aliyepigwa risasi jijini Arusha bank ya CRDB. Inadaiwa hata kiburi na jeuri aliyoonyesha mama huyo ilitokana na "kutoka" kwake na RC. Katika tukio hilo mama huyo aliingia na gari yake ndani ya viunga vya benki na kupaki eneo lisiloruhusiwa, mlinzi alimtaka aondoe gari lkn alikaidi ndipo mlinzi huyo alijulisha askari polisi. Alipotoka benki askari polisi walimsogelea kumhoji ndipo alichomoa bastola yake kitendo kilichopelekea askari kumuwahi kwa risasi wakidhani ni jambazi.

Ukaidi wa mama unajidhihirisha katika kauli zake na kitendo cha kutoa bastola ilhali hapakuwa na sababu yoyote ama mazingira ya kujihami kwa hatari yoyote
 
Huyo mama kama ni kweli atakuwa anamzalilisha RC ni bora sheria ichukue mkodo wake ili kama kuna vismall house vinatabia hiyo waache
 
Muwaambie hao wanaowanunulia hizo bastora, wasiwajaze ujinga mnapokuwa kitandani mtakuja kufa bure
 
Ingawa uzi wa zamani ila nimeusoma tena .......sasa kilicho mtokea huyo mama kingelitokea kipindi hiki nawaza ingekuwaje maana wengi walikuwa upande wa askari lakini leo ingekuwa tuonane 26 april, poli ccm kazini , wametumwa kuwamaliza wapinzani na mengine ....
..TZ tunajua kutumika vizuri ....
 
Unatukumbushaje mbali...huyu alikua kimada wa bosi wa mkoa aliyetumbuliwa kama jipu lililoiva
 
Ingawa uzi wa zamani ila nimeusoma tena .......sasa kilicho mtokea huyo mama kingelitokea kipindi hiki nawaza ingekuwaje maana wengi walikuwa upande wa askari lakini leo ingekuwa tuonane 26 april, poli ccm kazini , wametumwa kuwamaliza wapinzani na mengine ....
..TZ tunajua kutumika vizuri ....
Good observation!! Sasa hivi kila kitu kinalazimishwa kuwa cha kisiasa au kuonewa kwa upinzani!!!
 
Ingawa uzi wa zamani ila nimeusoma tena .......sasa kilicho mtokea huyo mama kingelitokea kipindi hiki nawaza ingekuwaje maana wengi walikuwa upande wa askari lakini leo ingekuwa tuonane 26 april, poli ccm kazini , wametumwa kuwamaliza wapinzani na mengine ....
..TZ tunajua kutumika vizuri ....
wafanyabiashara wa madawa ya kulevya; wezi wa fedha za miradi ya serikali; wafanyabiashara zote haramu; wanahasira sana na Serikali ya awamu hii.

Demokrasia inatumika kama mwavuli wa kuturejesha Katika Lindi la uovu.
 
Mwanamke ------- huyo!!! Wewe unajua askari ana silaha halafu unatoka na silaha unataka ukapambane naye?? Tena huyo askari hakufanya vema, angemtandika ya mguu auvunje kabia ili avae mguu wa bandia.
Bado anaishi zile zama za, "unanijua mi nani?"
 
Back
Top Bottom