Mwanamke akikuzidi kipato lazima ndoa ivunjike

Mwanamke akikuzidi kipato lazima ndoa ivunjike

Pale Magomeni jiarani yangu mmoja mke wake alienda kusoma USA, alivyorudi kapata kazi kwenye kampuni moja ya simu, wakamuweka katika kitengo cha International calls, akawa analipwa dola 9,000/month pamoja na marupurupu mengine. Jamaa alikuwa mtu wa madili kaenda kupiga kambi migodini yeye na best yake wakaondoka na mzigo wa maana, mwenzake kamgeuka na kumtapeli fedha Zaidi ya milioni 500, stress jamaa akawa mlevi hana mbele walau nyuma. Mke kwa upendo wa hali juu kila siku saa za usiku anamtafuta mume kwa gari, anapiga simu kwa marafiki wa mume mpaka ajue yupo wapi anaenda kumzoa na kumrudisha nyumbani, wanaume wakware wanamtongoza demu daily lakini demu anawapiga chini, mke sasa ana kipato kizuri na vitega uchumi kadhaa vya maana sana, lakini mapenzi yake kwa mume wake ni maradufu kiasi anapigiwa mfano Magomeni kote. Mapenzi ya kweli yapo wakuu, hata kama mume ni muflis.

Kuna kitu wanaume huwa mnasahau!

Mwanaume siyo mashine useme inaendeshwa hana maamuzi yake!

Baadhi ya wanaume wakiona mke anapesa unakuta anaanza kujihami ndani.. anaanza kumfanyia mambo ili awe inferior!
Anaanza karaha za hapa na pale kinachofuata mke nae anaamua lake!
Kwa kuwa anapesa mume atatumia kile kigezo ila pengine hata asingekuwa nazo kwa tabu za mumewe angeondoka tu/angecheat!

Wanaume pia huwa wanabadilika wakipaa juu financial ila wanawake wengi wana uvumilivu zaidi ya waume zao.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijamii wanawake wanapaswa kuwa watii,
Ili utii uwepo lazima iwepo any sort of Higherness ambayo 'The obeyed' anakuwa nayo,inaweza kuwa Pesa,Power,Hekima and so on.
Utii ni kama Kivuli chini ya Mti kwenye Jangwa,
Huwezi kukaa chini ya Mti,kama hauna kivuli,

The same applied kwa Mtii,Kama haoni cha kumfanya akutii,hata ufanyaje atatafta mtu wa kumtii tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee. Ndio walivyo hawa watu. Huwa hawachelewi.
Kama huyo bona. Angetulia kamamama samia yasingemkuta hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Yule manzi anaonekana much know tu hata kwa picha! Aisee ushamba mzigo yani. Ila sio mchezo kupata mshahara wake aliokuwa anausubiri kwa mwezi ndani ya masaa 24 kwa week nzima lazma awehuke na ubunge akishaumaliza ndio atatia akili!
 
Kijamii wanawake wanapaswa kuwa watii,
Ili utii uwepo lazima iwepo any sort of Higherness ambayo 'The obeyed' anakuwa nayo,inaweza kuwa Pesa,Power,Hekima and so on.
Utii ni kama Kivuli chini ya Mti kwenye Jangwa,
Huwezi kukaa chini ya Mti,kama hauna kivuli,

The same applied kwa Mtii,Kama haoni cha kumfanya akutii,hata ufanyaje atatafta mtu wa kumtii tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Inasikitisha sana kuona utatumia nguvu sana ili kupewa huo utii.

The basic thing a female has to consider should be the fact that you are her man, pia age na hekima. Ukiweka pesa kama kigezo uta struggle maana wapo wenye pesa zaidi yako.

Ila sikuhizi ni kinyume mwanamke akiwa na mkwanja tu anataka mume ndio amtii! Very funny sijui tunatengeneza jamii ya namna gani!
 
Ulimbukeni tu si kweli.Wengine tumeishi kwenye ndoa more than 20years na tunavipato vikubwa kuliko waumezetu na elimu pia.Issue ni tabia ya mtu hata kuna wanaume wa hivyo pia.Kingine wanaume wengi akishaona mke anakipato kikubwa anaanza kutafuta sababu badala ya kumsaidia mwenzi wake kwa hiyo kasoro kidogo tu anaanza visa.Wamama nao mmmm! wakipata hela wanaanza viburi na majivuno sasa hapo sasa badala ya kuongeza mapenzi kwa mumewe yeye anaona pesa ni kila kitu.
Nilishasikia kwamba mwanamke kadri anavyojitosheleza kwa kipato ndivyo mume anavyokuwa sio kitu cha maana kwake! Sija dig deep down ila kiuhalisia naona kama kuna ka ukweli flani!
 
Ni sawa tu na mwanaume akiwa kapuku anajifanya kukupenda ila akishazishika basi hamna namba utaacha kusoma. Tofauti ni kwamba wanawake huwa wanabaki humo ndani tu wakigugumia sababu ya watoto hawavunji ndoa zao.

Na wanaume wana inferiority complex, ukishqmzidi kitu tu basi visirani na kujistukia kwingi, kuishi nae kunahitaji moyo wa chuma. Hata ukimkosea kibinadamu tu anaona ni kwasababu tu umemzidi kipato.
Wanaume ishini na wake zenu kwa akili nao watawatii na hakutokuwa na shida.
Hahah akili ya kuvumilia kejeli sio 😁😁😁!
 
Halafu saingine ni inferiority complex tu kwa baadhi ya wanaume!




Sent using Jamii Forums mobile app
I concur ila kuna baadhi ya wanawake wana kejeli sana. Yani zile mume wangu za kutoka moyoni huwezi zisikia kabisa akishashika hela. Hasa wanawake wa kipare ni dadazangu ila waliotoka maisha duni huwa na ubabe sana wakishika jax! For that sake sitooa mpare, ni wavumilivu na wazuri sana wakiwa hawana doo!
 
Kwa hiyo makamu wa rais mama Samia hana ndoa?
Kaolewa na ana adabu sana na mumewe kiasi kwamba haogopi kujivunia jinsi anavyomuheshimu mume wake mbele ya umma! Anawasihi wengine waige mfano. Yeye umakamu wa raisi unaishia anaposhuka kwenye VX Geti la kuingilia kwake. Akiingia mjengoni ni mke wa mtu na mama wa familia.
 
Sasa kama mume he is misbehaving aendelee kuvumilia mtu anaefanya ufuska kwa makusudi?

Mwanamke atajiuliza aendelee kuishi kwa stress za mume ambae hana Msaada nae wowote zaidi ya huo mhogo?!

Kuna wanaume hana habari na familia hata mke au mtoto yuko hospitali amelazwa mwanaume haendi kuwaona,

Sasa huyo nae ni mume wa kuvumilia kweli?




Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ni mume kisheria ila kimapenzi sidhani, napenda kufahamu kama unam treat fairly pia isije ikawa unamletea madharau au unamfanyia unafiki unamsaliti kimya kimya halafu unategemea akupende. Being lenient is very essential kwa mwanamke ambaye anataka kujenga familia bora na imara yenye upendo kwa mume, watoto na hata ndugu!
 
Yupo jamaa yangu aliondolewa kwenye sakata la vyeti feki, kabla ya hapo alikuwa kwenye shirika la umma mjini na cheo kinono tu, yeye na mke wake ukiwaona ungeweza kufikiri wametongozana jana tu, mapenzi motomoto, walifanikiwa kupata mtoto mmoja.
Baada ya sekeseke, mke akaanza kuzisimamia biashara zote, hii ni kutokana na jamaa yangu kuvurugwa kisaikolojia na kukosa utulivu wa nafsi. Nilimuuliza kama ataweza kuweka aibu pembeni tufanye kazi ya udalali ambayo mimi ni mzoefu, akauliza vipi ikitokea mteja au muuzaji ni mtu tunaefahamiana, hapana siwezi. Nikamwambia, ikitokea hivyo hiyo kazi utaihamisha kwangu, na wewe utalamba kamisheni kama tufanyavyo kwenye michongo mingine, akakataa. Nikamwambia, chukua muda kuikubali hali yako kuwa sasa wewe si yule afsa mnene tena na huwezi kuwa yule afsa mnene, ila unaweza kuwa mnene kupitia fursa nyingine, ukijikubali.
Alichoamua jamaa ni kwenda kukaa kwenye moja ya maduka yao na kuuza, huku akisimamiwa na mkewe. Ndani ya mwaka mmoja mke akaona mume hana ramani tena, hela anayoingiza jamaa ni ile ya dukani pekee, hana tena safari za kikazi, warsha wala semina. Mke akaanza visa wakitaka waachane, maana jamaa ilifika kipindi mke siku zile za kushika ujauzito anavaa jinsi taiti na hagusiki.
Nikamuuliza bado unampenda mkeo, akajibu ndio.
Nikamwambia muage mkeo unasafiri kwenda mkoani kwa mwezi mmoja, uje ukae kijiweni kwangu, kweli, hapa niseme kitu, ukiamua kumsaidia mtu, msaidie tu, hata kama unajua kile atakachopata kinaweza kisivuke matarajio yake, lakini wewe msaidie.
Nikaanza kuzunguka na jamaa yangu kwenye michongo yangu yote ya udalali, ikawa wakati mwingine, nikitoka ofisini, namuacha jamaa akipokea wateja na kuwapeleka kwenye maeneo ambayo nilishampitisha iwe ni chumba, nyumba, kiwanja, shamba, magari, fremu, office appartment, masoko ya mazao n.k baada ya wiki tatu nikamwambia hiki ulichopata mtumie mkeo mwambie akaongeze mtaji wa dukani.
Kwa mara ya kwanza usiku wa siku hiyo jamaa akapokea simu kutoka kwa mke wake wakaongea kwa furaha baada ya wiki tatu za ukimya. Jamaa akaamini kuwa udalali ni kazi akawa ananishauri baadhi ya mambo ili kuboresha, na kweli tukaona vitu vina imarika bila kutumia nguvu nyingi kama zamani.
Ikatokea akanishauri tufungue kampuni flani hivi mwaka jana, mtaji ulikuwa ni mdogo tu, lakini jamaa yangu alisimama kikamilifu mpaka hivi ninavyokwambia kampuni inaendelea kuimarika na kile kinachopatikana kama faida tunagawana, ndoa yake imenusurika, na furaha imerudi kama zamani.
Alitumbuliwa 2017, 2018 akawa dalali, 2019 ni mkurugenzi wa kampuni yetu...Ndimi dalali.
Wewe jamaa ni rafiki wa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wew umenena kweli naomba wote humu wasome hii quote yako, alafu waniambie shida iko wapi.

Na je nikweli haifai kuwa na mke anaekuzid kipato?????

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukibahatika kudumu nae jua huyo sio limbukeni wa pesa na aidha amekulia kwao ambako kuna mali so pesa amezizoea!

Washenzi ni wale kajamba nani, oa mke wa hivyo halafu umpe nafasi ya kukuzidi ili uelewe vizuri tofauti ya dizel, petroli na Sundrop japo yote ni mafuta!
 
Mkuu wewe hilo tu mimi wa kwangu sasa yupo masters na akimaliza anampango wa PhD wakati mimi ni standard seven ila nafanya biashara zangu. Ahahhaahah
Ukiwa na mishe zako za kueleweka mke hata awe na PhD haikusumbui maana akitaka million unayo! Akitaka laki ipo chap tu. Ada unalipa, bills unalipa sasa hapo una presha gani bana.

Kimbembe ni wale ambao kipato cha kusua sua! Kila tatizo mpaka lisubirie tarehe 30! Lazma utasomeshwa namba ukiwa na mwanamke mshamba.
 
Aiseee mi ni mwanamke ila sipend kumzd mume wangu kipato na siombei itokee Mungu atusaidie

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama hutaki kumzidi kipato tulia ulee watoto tu.
Ila kwa comment yako mie kama mwanaume hata kama nilikuwa na mpango wa kuja kulipa mahari na cancel. Kwa level hii ya ufikiri hapana!
 
MTAZAMO MZURI, LAKINI KUNA WANAWAKE WANAZAA WATOTO KAMA UTITILI NA WANAISHI NA WANAUME WASIO NA KIPATO KIZURI. KUNA MWANAMKE AMEMPELEKA MUME WAKE KUSOMA, ANA MIMBA YA PILI SAA HIZI, YEYE NI POLISI JAMAA AMEISHIA FORM 4 TU LAKINI WANAISHI, ONCE BEFORE ALIMFUNGULIA BIASHARA YA STATIONARY NA SASA KAMPELEKA CHUO AKASOME!

WANAWAKE KAMA UNA UWEZO HAUNA MUME NA UMEMUONA JAMAA ANASOMEKA ILA TATIZO PESA MPIGANIE TU! MAFANIKIO YANAKUJA BAADA YA KUTOA KAFARA, USIKATISHWE TAMAA NA EXPERIENCE ZA WENGINE!
Watu watakuja kukupondea amini. Ila hayo kufanyiwa mwanamke wangepiga makofi na vigelegele! Wanasema ukitaka kufanikiwa fanya tofauti na matarajio ya wengi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom