Mwanamke akikuzidi kipato lazima ndoa ivunjike

Mwanamke akikuzidi kipato lazima ndoa ivunjike

Yupo jamaa yangu aliondolewa kwenye sakata la vyeti feki, kabla ya hapo alikuwa kwenye shirika la umma mjini na cheo kinono tu, yeye na mke wake ukiwaona ungeweza kufikiri wametongozana jana tu, mapenzi motomoto, walifanikiwa kupata mtoto mmoja.
Baada ya sekeseke, mke akaanza kuzisimamia biashara zote, hii ni kutokana na jamaa yangu kuvurugwa kisaikolojia na kukosa utulivu wa nafsi. Nilimuuliza kama ataweza kuweka aibu pembeni tufanye kazi ya udalali ambayo mimi ni mzoefu, akauliza vipi ikitokea mteja au muuzaji ni mtu tunaefahamiana, hapana siwezi. Nikamwambia, ikitokea hivyo hiyo kazi utaihamisha kwangu, na wewe utalamba kamisheni kama tufanyavyo kwenye michongo mingine, akakataa. Nikamwambia, chukua muda kuikubali hali yako kuwa sasa wewe si yule afsa mnene tena na huwezi kuwa yule afsa mnene, ila unaweza kuwa mnene kupitia fursa nyingine, ukijikubali.
Alichoamua jamaa ni kwenda kukaa kwenye moja ya maduka yao na kuuza, huku akisimamiwa na mkewe. Ndani ya mwaka mmoja mke akaona mume hana ramani tena, hela anayoingiza jamaa ni ile ya dukani pekee, hana tena safari za kikazi, warsha wala semina. Mke akaanza visa wakitaka waachane, maana jamaa ilifika kipindi mke siku zile za kushika ujauzito anavaa jinsi taiti na hagusiki.
Nikamuuliza bado unampenda mkeo, akajibu ndio.
Nikamwambia muage mkeo unasafiri kwenda mkoani kwa mwezi mmoja, uje ukae kijiweni kwangu, kweli, hapa niseme kitu, ukiamua kumsaidia mtu, msaidie tu, hata kama unajua kile atakachopata kinaweza kisivuke matarajio yake, lakini wewe msaidie.
Nikaanza kuzunguka na jamaa yangu kwenye michongo yangu yote ya udalali, ikawa wakati mwingine, nikitoka ofisini, namuacha jamaa akipokea wateja na kuwapeleka kwenye maeneo ambayo nilishampitisha iwe ni chumba, nyumba, kiwanja, shamba, magari, fremu, office appartment, masoko ya mazao n.k baada ya wiki tatu nikamwambia hiki ulichopata mtumie mkeo mwambie akaongeze mtaji wa dukani.
Kwa mara ya kwanza usiku wa siku hiyo jamaa akapokea simu kutoka kwa mke wake wakaongea kwa furaha baada ya wiki tatu za ukimya. Jamaa akaamini kuwa udalali ni kazi akawa ananishauri baadhi ya mambo ili kuboresha, na kweli tukaona vitu vina imarika bila kutumia nguvu nyingi kama zamani.
Ikatokea akanishauri tufungue kampuni flani hivi mwaka jana, mtaji ulikuwa ni mdogo tu, lakini jamaa yangu alisimama kikamilifu mpaka hivi ninavyokwambia kampuni inaendelea kuimarika na kile kinachopatikana kama faida tunagawana, ndoa yake imenusurika, na furaha imerudi kama zamani.
Alitumbuliwa 2017, 2018 akawa dalali, 2019 ni mkurugenzi wa kampuni yetu...Ndimi dalali.
Mwanamke hufadhaika sana akiona life lime change ghafla! Sijui kwanini huwa hivyo!
 
Kuugua ,kuachishwa kazi hzo ni case study nyngne ambazo hazihusiani na content ya mada rudi juu usome upya

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeshasema "sharti anizidi kipato", au akiwa amerejea katika uzima toka kwenye kuumwa na pesa hana anaanza kusafa upya anakuwa sio mumeo maana umemzidi!?
 
Nimefuatilia kwa ukaribu wanawake waliolewa wakiwa na kipato kidogo au hawana kabisa lakini wakabahatika kusaidiwa na waume zao either kwa kusomeshwa au kufufuguliwa biashara Mikubwa , baadae wakatalakiana hawa ni wachache tu ninawowafahamu na kabla walikuwa wananipa motisha ili nikioa niwe Kama walivyo coz niliwaona wanapendana .

Wakwanza ni mwalimu wangu mkuu wa O level ,huyu nikiwa form one 2009 alipokea madam mbichi kabisa ...fresh from University kipindi kile mzee kikwete alikuwa anamwaga ajira Kama njugu sio Kama awamu ya tano...(maendeleo Haina chama ) baadae mwalimu mgeni /madam akapangiwa kufundisha history f1 kusema ukweli mwanzo nilikuwa simwelewi anachofundisha sio kwamba hajui kufundisha... la asha anajua vizuri lkn jinsi alivyoumbika madam ana umbo namba nane ikabid Mimi nimfaidi umbo tu Kuona anavyotingisha akiandika ubaoni duuuuu kipindi hicho full utoto .kumbe mwl mkuu kapenda madam na kutokana na kulikuwa na walimu wengin vijanq ikabidi mkuu afanye faster ndani mwez sita ndoa tayari mkuu kavuta mtto walipendana Sana kila sehemu wapo pairs ,tatizo kimetokea mwaka Jana baadae ya mwl wg mkuu kutolewa ukuu wa shule coz ana diploma na madam kuwa mkuu wa shule kwa miezi mitatu na kupandishwa kutoka mkuu wa shule hadi afisa elimu taluma/msaidizi ....kumbuka madam ni mkali kiumbo na kisura alichofanya madam sijui kaomba kuamishwa /au kanishwa tu tuko nae jiji la makonda mume wake walitalakiana baada ya kushushwa cheo na yeye kupanda.


Wa pili ni ndg yg wa karibu yeye alikuwa kwenye ajira bahati mbaya vyeti feki kamtoa mke kabaki juzi wametalakian mke anamuita mzigo ...mke alianza kuingiza madume ndani ikabid njamaa ampige chini japokuw mke anafrah baada ya kupew talaka .


Kuna bext wg alikubalian na mke wake ..mke aende ongeze elimu bahati nzuri mke baada ya kumaliza Masters akapandishwa sio kwamba alikuwa na master pke yk hapan waliangalia v2 vigi pamojaja na yy kaanzia certificate hadi Masters ..jui jamaa kaenda mahakamni kuhusu talaka na ofisi ni moja cjui watafanyaje kazi.

Wapo wengi wengi Sana kwa kusamarise hawa wanawake wasikuzidi kipato ikitokea uwe na uvumulivu was Ali ya just ...Baba yg aliwai kuniambi "Mwanangu usioe mwanamke anaekuzidi kipato "alikuwa na maanake ,kwa niliyo yaona na binavyozidi kuyaona sitaoa mwanamke anaenizidizidi kipato nitapigana Hadi nimpite tunayoyaona ni aibu

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo si kuzidiwa kipato tatizo mambo mengi na mda mchache na kamwe usijifunze kwa walioshindwa maishani
 
Inakuwaje kama kakupenda na anasisitiza umuoe?
Pesa inafanya maamuzi na mwenye pesa ndiye mwenye maamuzi. Sasa sifikiria utakuwa mwanaume gani usiye na maamuzi.

Zitakuwa nyege zikimuisha utamtambua.
 
Mwanaume uliyemzidi kipato hata umtendee wema vip!!! kipato chako kitamnyanyasa.
 
Mwanamke hufadhaika sana akiona life lime change ghafla! Sijui kwanini huwa hivyo!
Wakati fulani huwa maisha yako mazuri wewe mwanaume yalikuwa ni mojawapo ya kigezo alichokupendea. So, kinapotoweka hicho kigezo huwa shida kidogo.
 
Wakati fulani huwa maisha yako mazuri wewe mwanaume yalikuwa ni mojawapo ya kigezo alichokupendea. So, kinapotoweka hicho kigezo huwa shida kidogo.
Huenda ni kweli ndio maana mie naona bora mke anipende nikiwa kapuku tu hapo ndio kipimo cha dhati cha upendo wake ili hata nikiwa na hela zaidi ama nikifulia heshima iendelee kuwepo tu!
 
Huenda ni kweli ndio maana mie naona bora mke anipende nikiwa kapuku tu hapo ndio kipimo cha dhati cha upendo wake ili hata nikiwa na hela zaidi ama nikifulia heshima iendelee kuwepo tu!
Ukweli mchungu ni kwamba, wapo warembo wazuri wanakupenda kwa dhati ila kwa sababu ya ujinga wetu tuliowengi tunaangalia status za familia zao, kumbe ukweli ni kwamba mwisho wa siku huoi familia unaoa mke mmoja na siku hizi kila mtu anapambana na hali yake, wale wakwe wa kuwasaidia watoto kimaisha kupewa zawadi ya nyumba na gari wameshakufa.

Trust me ukipendana na demu mkali mtoto wa fundi koroboi go for it, ajira ya mwanamke ina manufaa binafsi kwa mwanamke na siyo family, hakuna good wife material kama hawa wamama wa nyumbani, i can see kuna watu wanaenjoy ndoa zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli mchungu ni kwamba, wapo warembo wazuri wanakupenda kwa dhati ila kwa sababu ya ujinga wetu tuliowengi tunaangalia status za familia zao, kumbe ukweli ni kwamba mwisho wa siku huoi familia unaoa mke mmoja na siku hizi kila mtu anapambana na hali yake, wale wakwe wa kuwasaidia watoto kimaisha kupewa zawadi ya nyumba na gari wameshakufa.

Trust me ukipendana na demu mkali mtoto wa fundi koroboi go for it, ajira ya mwanamke ina manufaa binafsi kwa mwanamke na siyo family, hakuna good wife material kama hawa wamama wa nyumbani, i can see kuna watu wanaenjoy ndoa zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah they have less problems than the working class of women.
 
Yeah they have less problems than the working class of women.
Tusioe kwa kufuata class za wanawake, tuongozwe na utashi wa kimapenzi.

Kuna watu humu ukiwauliza wana mwaka hawajapikiwa na wake zao wala kufuriwa wala kunyooshewa nguo, na tendo la ndoa la mgao kama Tanesco mpaka anapojisikia mwanamke, ndoa za aina hii ni za kazi gani? Ndio sababu tatizo la stroke linaongezeka mioyo ya wanaume wengi ina majeraha ya ndani kwa ndani watu hawasemi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom