Tunapoongelea usawa katika ndoa tukumbuke tofauti za kiuumbaji kati ya Mwanamke na Mwanaume

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,274
Mwili wa mwanaume una misuli mingi kupita wa mwanaume. Misuli hii inampa nguvu za ziada katika kuilinda familia. Mkiona nyoka ndani ya nyumba hutashangaa kusikia muiteni baba, ni mara chache kwenye familia yenye wazazi wawili kusikia kuna nyoka huku muiteni mama. Baba akishamuua nyoka Ego yake inakuwa juu kuona ametimiza wajibu wake.

Baadhi ya wanaume hutumia hizi nguvu za asili walizopewa na Mungu Unamkuta baba hafanyi shughuli yeyote ya kuingiza kipato kwenye familia. Mama na watoto ndiyo wanaoenda shambani asubuhi na kurudi jioni kama shule zimefungwa. Baada ya kazi za shamba mama anategemewa apike chakula na usiku kuvumilia matusi ya mtu anaetaka kutumia akiba ya familia kwenye pombe.

Nimesoma divorce petition ya Bill na Melinda Gate. Melinda anasema kutoka siku za mwanzo za ndoa yao hakukubali aonekane kama mama wa nyumbani na mlezi wa watoto wao watatu. Alihakikisha yeye ni equal partner katika kila jambo la Bill. Hapa inawezekana Melinda alisahau kumpa nafasi mume wake ya kuonyesha nguvu yake kama mwanaume kwenye familia na kuipa nafasi eagle ya mwanaume kuonekana ndani ya familia

Pesa si kila kitu katika maisha. Furaha na amani ni muhimu vinapoambatana na pesa ndiyo ndoa mtaishi kama pepo ya duniani.

Kuna baba mmoja Mzungu wale wa familia za kitajiri (aristocracy). Amemuoa mama wa Kikikuyu. Ilikua ni baada ya ndoa yake ya kwanza kuvunjika na mke wake kumsafisha kisawasawa katika talaka. Aliwenda Kenya kupumzika kwa marafiki wa familia wanaoishi Kenya. Alikutana na mrembo huyu wa Kiafrika na wakafunga ndoa.

Alihojiwa na gazeti moja anasema sasa hivi anaishi kama Mfalme ndani ya nyumba yake. Mke wake anajua kahawa yake inakua tayari saa ngapi, shati atakalo vaa kwenye mkutano leo na chakula chake kitakua tayari muda gani. Yule mzungu alisema kwa mke huyu wa sasa hana mambo mbengi. Likizo anataka aende nyumbani kwake Kenya na gharama aliyoingia kubwa ni kumnunulia ardhi na kumjengea nyumba ya ndoto yake huyu mama ambayo kwa uhalisia ni ya kwao wote.

Nilipata jirani mke na mume na watoto wao wawili wakiume. Mke ni mtaalamu wa IT na amepata mkataba kwenye kampuni ya kimataifa. Mke ndiye aliye mleta mkate mkubwa nyumbani lakini ameolewa na mchumba wake wabutotoni kutoka nyumbani na ndani ya nyumba akitoka kazini yule dada ndiye mpishi wa familia. Mume wake ni dereva katika restaurant inayosambza vyakula majumbani.
 
Hivi wanawake kama huyo mkikuyu wapo kweli kwenye hii dunia?Kuna siku nilikuwa nawaza,hivi mbona wazee wengi wa zamani walikuwa na vitambi,nikaja kugundua kuwa wanawake wao pamoja na kuwa wengi wao walikuwa ni wamama wa nyumbani lakini walijua kucheza na akili za waume zao,sasa angalia dunia ya siku hizi kila mwanaume aliooa ana six packs,hii ni kuonyesha kuwa huko ndani kunawaka moto...
 
Tatzo ni kupuuza misingi ya ndoa iliyoweka na mwanzilishi wake na kutaka kuleta ujuaji mwingi
Kuna video ilizunguka katka mitandao ya kijamii. Mwaume Mnigeria wanaishi Marekani anasema mke wake anataka apikiwe, afuliwe na bills wagawane nusu kwa nusu kwakua wako Marekani. Anasema Waafrika wanaiga uzungu kupitiliza. Wakati huo huo snow ikifunika gari anaitwa baba akaitoe.
 
Hapo mm nakupa nauli ama eka ya kianzia maisha unipishe.
 
Napenda niwakumbushe katika Maandiko matakatifu nkirejea Biblia "Hata hivyo, kila mtu kati yenu anapaswa kumpenda mke wake kama anavyojipenda mwenyewe; kwa upande mwingine, mke anapaswa kumheshimu sana mume wake." Waefeso 5 : 33. Hivyo mke anapaswa kuwa na heshima na kuheshimu mamlaka ya mume wake.
 
naona tumeelewana sisi tuwapende wao watuheshimu
 
Wapo maslay queen wenye akili ya ndoa
Anajua mpenzi wake anapenda nini na anatakiwa kufanyiwa nini!kiufupi anajua majukumu yake nje ya huo uslay queen

Sio kila slay queen hajielewi kama mnavyodhani
Ila ni wachache
 
Wapo maslay queen wenye akili ya ndoa
Anajua mpenzi wake anapenda nini na anatakiwa kufanyiwa nini!kiufupi anajua majukumu yake nje ya huo uslay queen

Sio kila slay queen hajielewi kama mnavyodhani
Mshiko kama wa Bill Gate u slay queen tupa kule
 
HABARI KWA UFUPI: wanaume wa Kenya walalamikia serikali kupigwa na wake zao.

Taarifa zaidi zitakujia hivi punde.
 
Back
Top Bottom