Mwanamke akikuzidi kipato lazima ndoa ivunjike

Mwanamke akikuzidi kipato lazima ndoa ivunjike

Kuna mwalimu huku anatuhumiza tuoe wanawake wenye CPA..!

Nikimsikiliza, ndio kusema nijiandae kisaikolojia..?

Mpaka leo naogopa kuweka my lifestyle rehani kisa kuoa.

Mbona tupo wengi wenye CPA (T) tumeolewa na ndoa zetu ziko vizuri zina maelewano mazuri!
Ndoa zetu zinaheshimiwa na watu wote na malazi yake yako safi!
[emoji3][emoji3][emoji3]

After all kuwa na CPA mbona siyo ishu sana !




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binti aliyepata malezi mema tangu utotoni na Neema ya kumcha Mungu hata awe Profesa na kuwa Rais wa JMT hawezi mzarau mume wake hata kidogo labda huyo Mume aharibu yeye mwenye kwa makosa ambayo si ya kuvumilika kabisa!




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi kusingekuwa na haja ya Wanaume kupewa ukuu ktk uongozi kuwa tuwe vichwa vya familia.

Binti aliyepata malezi mema tangu utotoni na Neema ya kumcha Mungu hata awe Profesa na kuwa Rais wa JMT hawezi mzarau mume wake hata kidogo labda huyo Mume aharibu yeye mwenye kwa makosa ambayo si ya kuvumilika kabisa!




Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona tupo wengi wenye CPA (T) tumeolewa na ndoa zetu ziko vizuri zina maelewano mazuri!
Ndoa zetu zinaheshimiwa na watu wote na malazi yake yako safi!
[emoji3][emoji3][emoji3]

After all kuwa na CPA mbona siyo ishu sana !




Sent using Jamii Forums mobile app

Hahaha..!!

Definitely.. CPA is not an issue..

Ishu ni kwamba wanawake wenye CPA wana majukumu mengi sana ya kiofisi...

Unaeza jikuta ww ndio muogesha watoto, mbadilisha watoto nguo, mpishi, mtandika na mtandua kitanda...

Bado indiscipline(in most cases) kutokana na kipato anachopata mizungukoni mwake(rejea mafahari wawili hawakai zizi moja)...

I know I am being judgmental, All in all, personally tendo linaloitwa mahusiano achilia mbali ndoa is so scary, high risk... Sijui mpaka sasa lini hasa nitajihusisha na hayo matukio...

Hongera Mkuu for having a great family..!
 
Hahaha..!!

Definitely.. CPA is not an issue..

Ishu ni kwamba wanawake wenye CPA wana majukumu mengi sana ya kiofisi...

Unaeza jikuta ww ndio muogesha watoto, mbadilisha watoto nguo, mpishi, mtandika na mtandua kitanda...

Bado indiscipline(in most cases) kutokana na kipato anachopata mizungukoni mwake(rejea mafahari wawili hawakai zizi moja)...

I know I am being judgmental, All in all, personally tendo linaloitwa mahusiano achilia mbali ndoa is so scary, high risk... Sijui mpaka sasa lini hasa nitajihusisha na hayo matukio...

Hongera Mkuu for having a great family..!

Ni kwa Neema tu na rehema za Mungu!
Na siyo kwamba mambo yako tambalale kiivyo?!
Tofauti ndogo ndogo za hapa na pale wakati mwingine zinajitokeza!

Watu wanaokutana wakiwa tayari na meno 32 wakisema huwa hawagombani ni uongo!

Kupishana kupo ili mradi kuwe kule kwa makosa ambayo hayana madhara kwa mweza au wote!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilianza naye nikiwa nimemzidi kipato,elimu ila kwakuwa tuliheshimiana na kupendana hatukukumbuka hata kuwa nimemzidi. Kwakuwa tukipata tuliipangia pamoja kufanya mambo yetu. Nampenda namuheshimu "he is my King"

Alisikika mdada fulani hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke ndiye anayetakiwa kununua mashamba, viwanja , kulipa wafanyakazi wa familia n.k
Kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu!
Mwanamke anatakiwa kuwa mtu mwenye Hadhi na heshima kama vazi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kwa Neema tu na rehema za Mungu!
Na siyo kwamba mambo yako tambalale kiivyo?!
Tofauti ndogo ndogo za hapa na pale wakati mwingine zinajitokeza!

Watu wanaokutana wakiwa tayari na meno 32 wakisema huwa hawagombani ni uongo!

Kupishana kupo ili mradi kuwe kule kwa makosa ambayo hayana madhara kwa mweza au wote!


Sent using Jamii Forums mobile app

Haha..

Kwa hiyo Mkuu nikitafuta Mdada aliye kongoroka meno kama saba hivi ili nipate uwiano wa 32:25 nitakua pazuri...!!

Kama "ndoa na kugombana baina ya wanandoa" ni mtu na Kaka yake.. Kwa tusio penda kugombana unatushauri tendelee kuwa watizamaji tu....

Neema na rehema zake ziendelee kukuangazia Mkuu.
 
Haha..

Kwa hiyo Mkuu nikitafuta kadada kalikokongoroka hata meno saba nipate uwiano wa 32:25 nitakua pazuri...!!

Kama "ndoa na kugombana baina ya wanandoa" ni mtu na Kaka yake.. Kwa tusio penda kugombana unatushauri tendelee kuwa watizamaji....

Labda tuanze kwa kuelewana kwenye maana ya ugomvi ni nini kwanza kisha ndiyo tuendelee na majadiliano!
1. Ugomvi au kugombana maana yake ni nini?
2. Nini kupimo cha ugomvi?
3. Je ni ugomvi gani ambao ni wa hatari zaidi na madhara yake?

Ukielewa maana ya ugomvi utagundua kumbe hadi hapo ulipo ulishagombana mara nyingi sana!
Utakuwa ukishagombana na wazazi wako, walimu wako, marafiki, n.k

Sasa je kama kama hupendi ugomvi ungejua mapema ungeomba usizaliwe?
Je ungekataa kusoma Shule kwa kuwa hutaki ugomvi?





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haha..

Kwa hiyo Mkuu nikitafuta Mdada aliye kongoroka meno kama saba hivi ili nipate uwiano wa 32:25 nitakua pazuri...!!

Kama "ndoa na kugombana baina ya wanandoa" ni mtu na Kaka yake.. Kwa tusio penda kugombana unatushauri tendelee kuwa watizamaji tu....

Neema na rehema zake ziendelee kukuangazia Mkuu.

Maana rahisi ya watu kugombana yaweza kuwa ni ile hali ya kubishana , mmoja au au wote kuona mwenzie amemkosea,
Hali hiyo yaweza kuleta kurushiana maneno, au mgomo baridi (kununa), wengine ambao hawana hawana vifua au kukosa subra huweza kutukanana na hata kupigana ngumi na pengine kuachana kabisa!

Kama mtu unaweza kugombana na mzazi wako, ndugu yako wa tumbo moja n.k
Je sembuse mtu ulokutana nae akiwa na meno 32?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shuhuda zote mbili ninazo, tena ni nyingi coz kazi ya kusuluhisha ndoa nimeifanya sana tena sana. Mbaya zaidi naweza kukaa na mwanamke dakika tano tuu akafunguka yote ya moyoni!! Wanawake wanabeba mengi mazito na wapo wapo tu, ila siku akiotea pa kukuchapa anakuchapa haswa bila huruma. Yaan hii ni from the horse's mouth!

Nilichogundua kwa nini ndoa zinavunjika mwanamke akipata kipato wengi ni VISASI kutokana na jinsi tunavyoishi nao!

Kipato chako hajui, anakufumania kila leo, pombe na wewe familia huna muda nayo, akiwa na shida unamsimanga kwanza then unampa suluhisho, manyanyaso mengi mengi yanayochangiwa na mfumo dume.

Hapo hata kama ni wewe ukija kupata kipato lazima ulipe kisasi na kusepa zako!! Maana hayakuwa mapenzi!!

Pili: Wapo wenye wake wenye vipato vikubwa na ndoa ni za amani sana. Kwa sababu aliweka misingi imara ya mapenzi yao. Unachokipata onyesha consideration hata kama usimuonheshe kipato chote kwa mkeo, kaa nae muweke mipango mwambie hiki ndo ninacho, mpende kwa kumuonyesha, toka kazini kaa nae jua haja zake na familia, nenda kwenye pombe utamuona ana amani kabisa, mtimizie mahitaji kama mume bila manyanyaso au masimango, penda familia kwanza, onyesha juhudi za kujali kufanikiwa kwake!! Akivunja ndoa huyo alikuwa chizi na si mke!!

Wanawake wengi niliowahi kuongea nao kwa nini wanakimbia waume zao majibu yao yalikuwa ni hayo hapo! Ukisikia mwanamke anakwambia nakaa tu sababu ya watoto au sababu sina kazi ogopa sana mtu huyo. Na ndoa zetu nyingi zimefikia hapo na wanaume hatujali tunakuja kupigia kelele matokeo ya mwanamke kujikoboa!!

kwa muktadha huu sredi ifungwe tu umeshamalzia kila kitu hapa
 
Yupo jamaa yangu aliondolewa kwenye sakata la vyeti feki, kabla ya hapo alikuwa kwenye shirika la umma mjini na cheo kinono tu, yeye na mke wake ukiwaona ungeweza kufikiri wametongozana jana tu, mapenzi motomoto, walifanikiwa kupata mtoto mmoja.
Baada ya sekeseke, mke akaanza kuzisimamia biashara zote, hii ni kutokana na jamaa yangu kuvurugwa kisaikolojia na kukosa utulivu wa nafsi. Nilimuuliza kama ataweza kuweka aibu pembeni tufanye kazi ya udalali ambayo mimi ni mzoefu, akauliza vipi ikitokea mteja au muuzaji ni mtu tunaefahamiana, hapana siwezi. Nikamwambia, ikitokea hivyo hiyo kazi utaihamisha kwangu, na wewe utalamba kamisheni kama tufanyavyo kwenye michongo mingine, akakataa. Nikamwambia, chukua muda kuikubali hali yako kuwa sasa wewe si yule afsa mnene tena na huwezi kuwa yule afsa mnene, ila unaweza kuwa mnene kupitia fursa nyingine, ukijikubali.
Alichoamua jamaa ni kwenda kukaa kwenye moja ya maduka yao na kuuza, huku akisimamiwa na mkewe. Ndani ya mwaka mmoja mke akaona mume hana ramani tena, hela anayoingiza jamaa ni ile ya dukani pekee, hana tena safari za kikazi, warsha wala semina. Mke akaanza visa wakitaka waachane, maana jamaa ilifika kipindi mke siku zile za kushika ujauzito anavaa jinsi taiti na hagusiki.
Nikamuuliza bado unampenda mkeo, akajibu ndio.
Nikamwambia muage mkeo unasafiri kwenda mkoani kwa mwezi mmoja, uje ukae kijiweni kwangu, kweli, hapa niseme kitu, ukiamua kumsaidia mtu, msaidie tu, hata kama unajua kile atakachopata kinaweza kisivuke matarajio yake, lakini wewe msaidie.
Nikaanza kuzunguka na jamaa yangu kwenye michongo yangu yote ya udalali, ikawa wakati mwingine, nikitoka ofisini, namuacha jamaa akipokea wateja na kuwapeleka kwenye maeneo ambayo nilishampitisha iwe ni chumba, nyumba, kiwanja, shamba, magari, fremu, office appartment, masoko ya mazao n.k baada ya wiki tatu nikamwambia hiki ulichopata mtumie mkeo mwambie akaongeze mtaji wa dukani.
Kwa mara ya kwanza usiku wa siku hiyo jamaa akapokea simu kutoka kwa mke wake wakaongea kwa furaha baada ya wiki tatu za ukimya. Jamaa akaamini kuwa udalali ni kazi akawa ananishauri baadhi ya mambo ili kuboresha, na kweli tukaona vitu vina imarika bila kutumia nguvu nyingi kama zamani.
Ikatokea akanishauri tufungue kampuni flani hivi mwaka jana, mtaji ulikuwa ni mdogo tu, lakini jamaa yangu alisimama kikamilifu mpaka hivi ninavyokwambia kampuni inaendelea kuimarika na kile kinachopatikana kama faida tunagawana, ndoa yake imenusurika, na furaha imerudi kama zamani.
Alitumbuliwa 2017, 2018 akawa dalali, 2019 ni mkurugenzi wa kampuni yetu...Ndimi dalali.
 
Labda tuanze kwa kuelewana kwenye maana ya ugomvi ni nini kwanza kisha ndiyo tuendelee na majadiliano!
1. Ugomvi au kugombana maana yake ni nini?
2. Nini kupimo cha ugomvi?
3. Je ni ugomvi gani ambao ni wa hatari zaidi na madhara yake?

Ukielewa maana ya ugomvi utagundua kumbe hadi hapo ulipo ulishagombana mara nyingi sana!
Utakuwa ukishagombana na wazazi wako, walimu wako, marafiki, n.k

Sasa je kama kama hupendi ugomvi ungejua mapema ungeomba usizaliwe?
Je ungekataa kusoma Shule kwa kuwa hutaki ugomvi?





Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa tafsiri ya kugombana kama ulivyotanabaisha, siwezi kataa kwamba sijawahi gombana.. Tena sio huu ugomvi wa kutupiana maneno tu, nakumbuka miaka 5 iliyopita nikiwa kidato cha 6 niligombana na classmate wangu mpaka nikamg'ata meno(alinizidi nguvu aisee..). My teacher punished me severely na uongozi wa shule ukanitishia kunifukuza shule(nikawa mdogo 😁).. Namshukuru Mungu sana we settled the case na zaidi namshukuru Mungu mpaka leo nina mahusiano chanya na niliyemng'ata..!

Sio siri hilo tukio liliniumiza sana.. Nikatokea kuchukia sana ugomvi, na mazingira(ndoa mojawapo) yote yanayoweza nisababishia ugomvi...

Tokea hapo nikajiwekea azimio binafsi la kuishi maisha yaliyobaki bila ya kugombana na mtu kwa kujiwekea miiko kadhaa.

Nilijua toka mwanzo kujicontrol sio ishu sana kwangu ila tatizo lipo katk kucontrol watu mbalimbali wanaotoka nisikokujua and yet natakiwa nihusiane nao kwenye ishu zozote zile bila kuathiri azimio langu la kutogombana na mtu kwa namna yeyote ile.

"Handling people sio kazi rahis aisee.." kwa kuzingatia hili, kwa uchache nikajiwekea baadhi ya miiko kama, kusoma tabia ya mtu (learning person behavior profile), kupunguza kujaamiaana na watu, chukuliana na watu, heshimu watu, kutoendekeza madeni, kujishusha, omba msamaha.....

So far from hii miiko nimekwepa mishale miingi sana.. Itoshe kusema ila ndoa ndio changamoto au mkuki uliobakia kushinda yote...

Mpaka leo mimi ni mkimbizi mbobezi wa ugomvi..!
 
Sasa akitangulia kufa jamaa ndo kasheshe itakapokuwa,
Maana watoto kama walikuwa wanasoma Shule za maaana kama vile Fedha , n.k watashindwa kuendelea na masomo kwa kuwa mwanamke kwa kipato chake hataweza kuendelea kuwalipia ada watoto kwa kipato chake,
Hivyo watoto kurudi Shule za kawaida za Kiswahili hali ambayo huwakatisha tamaa kabisa watoto na saingine kuanza kuachana na masomo kabisa!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ruge nasikia wanae walikuwa wanasoma Fedha school,
Je kila mama wa mtoto au watoto husika atakuwa na uwezo wa kulipa ada ya Shule ya mtoto?

Kuwarudisha watoto Shule za kawaida haitakuwa kuwa demotivate watoto?!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pale Magomeni jiarani yangu mmoja mke wake alienda kusoma USA, alivyorudi kapata kazi kwenye kampuni moja ya simu, wakamuweka katika kitengo cha International calls, akawa analipwa dola 9,000/month pamoja na marupurupu mengine. Jamaa alikuwa mtu wa madili kaenda kupiga kambi migodini yeye na best yake wakaondoka na mzigo wa maana, mwenzake kamgeuka na kumtapeli fedha Zaidi ya milioni 500, stress jamaa akawa mlevi hana mbele walau nyuma. Mke kwa upendo wa hali juu kila siku saa za usiku anamtafuta mume kwa gari, anapiga simu kwa marafiki wa mume mpaka ajue yupo wapi anaenda kumzoa na kumrudisha nyumbani, wanaume wakware wanamtongoza demu daily lakini demu anawapiga chini, mke sasa ana kipato kizuri na vitega uchumi kadhaa vya maana sana, lakini mapenzi yake kwa mume wake ni maradufu kiasi anapigiwa mfano Magomeni kote. Mapenzi ya kweli yapo wakuu, hata kama mume ni muflis.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom