Bwana ametoa,bwana ametwaa,
Kazi ya bwana hakika haina makosa,
Kila alitendalo bwana, lina makusudi makuu kwa mja wake,
Jina lake yeye, hakika litahimidiwa
Dada yetu, wifi yetu, shemeji yetu ametutoka,
Hili ni pigo kwa Familia ya JF na watanzania wote,
Tangulia mpendwa wetu, nasi twafata njia moja,
Sisi sote ni mavumbi, na mavumbini tutarudi.
Pole sana kaka FD, wana JF twakuombea,
Katika Majonzi twalia pamoja,hakika pokea zetu pole,