Mwana JF aaga dunia!

Status
Not open for further replies.
I know it is hard hard time for all of us at JF, but i hope we can also use this time to realise that we live by the Grace of God!
May the soul of our beloved sister rest in peace - Amen
 
Mungu wa faraja awape ujasiri katika hiki kipindi kigumu mume wa marehemu na wanafamilia wote. Roho ya mwana-jf mwenzetu ipumzike kwa amani.
 
Hi Members.
Tumetoka kumuaga dada yetu kwa mara ya mwisho hadi pale tutakapo onana tena kwenye Uzima wa milele.
Tuwaombee wenzetu wanaosafiri kuelekea Tanga kwenda kumpumzisha dada yetu mpendwa.Tuiombee familia ya kaka yetu wakati huu mgumu waliokua nao.

Upendo wa Mugnu wetu wazidi upendo wa wanadamu.Jina la bwana libarikiwe.
 
Mungu ailaze roho ya Mpendwa mama/dada yetu pema peponi...
nawapa pole wale wooote walioguswa na msiba huu
 
Jamani mlioko nyumbani na mliokwenda msibani, mnaweza kutupa updates? Mme mfiwa anaendeleaje?
 
Jamani mlioko nyumbani na mliokwenda msibani, mnaweza kutupa updates?
Rev,
Nipo msibani na sasa ni saa 10 alfajiri.

Mazishi yatakuwa saa 10 jioni na nitawafahamisha kadiri nitakavyopata muda wa kufanya hivyo maana natumia simu na charge imenipungukia.

Kwa niaba ya mme wa marehemu napenda kuwashukuru wana JF wengi ambao tuliungana na familia ya wafiwa na pia shukrani za kipekee ni kwa wale tulioambatana kuja huku kuusindikiza mwili wa marehemu. Pia wale walio nje waliompigia simu anawashukuru sana kwani imekuwa faraja kwake.

Zaidi nitawafahamisha pindi nikipata wasaa.
 
ahsante kaka melo kwa juhudi zako, mola akuzidishie moyo wa kujali na kupenda wenzio

kutoa kwa mwenziwe mtu hajatupA wala hajapoteza
 
Pole sana wana Jf na ndugu kwa ujumla tupo pamoja nanyi kwa sala katika hiki kipindi kigumu...
 
Asante kwa taarifa, ndugu Mac tunaungana nanyi mlioko hukTunamwomba Mungu mambo yote yaende salama ili dada yetu mpenzi alale kwa amani. Kaka FD endelea kumshukuru Mungu kwa kila jambo, yeye ni mwaminifu atakupa faraja katika wakati huu mgumu.
 
Tulikuja kwa mavumbi tutarudi kwa mavumbi. Jina la bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Mungu amlaze pema peponi amina.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom