Msiba umetufika, wa mwenzetu mwanachama
kwa huzuni naandika,msikie wote hima
mioyo yahuzunika,furaha imetuhama
Upumzike kwa Amani,dada yetu Mpenzi
ee bwana ulitoa, binadamu uliumba
na saa umetwaa, ndugu ulompenda
majonzi yametukaa,simanzi imetukumba
Upumzike kwa Amani,dada yetu Mpenzi
Mwenzetu tulikupenda, Kwa michango bodini
Mola naye kakupenda ,akakuita peponi
japo pumzi imekwenda,daima u mioyoni
Upumzike kwa Amani,dada yetu Mpenzi
Sote sisi tunalia, Kumpoteza mwenzetu
Sote twajiinamia, kumuwaza mtu wetu
Mioyo yetu yaumia,imepata kali kutu
Upumzike kwa Amani,dada yetu Mpenzi
Ewe baba mpokee, Mwenzetu huko mbinguni
Ewe Mola mtolee, Adhabu za kaburini
Malaika msichelee, Kumwongoza mbinguni
Upumzike kwa Amani,dada yetu Mpenzi
MAY THE SOUL OF OUR BELOVED SISTER REST IN HEAVENLY BLISS.