Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo kwani inadaiwa kuwa kabla ya ujio wa mbio za mwenge wa uhuru, marehemu alikabidhiwa fedha na ofisi ya TAKUKURU kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kibao cha “KLABU YA TAKUKURU RAFIKI SHULENI” lakini pamoja na kutumiwa fedha hizo hakuweza kutengeneza kibao hicho hadi Mwenge wa Uhuru ulipofika shuleni hapo kwa ajili ya ufunguzi wa Klabu hiyo.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wananchi walioibiwa mali mbalimbali kufika kituo cha Polisi Rujewa, Mbeya Mjini na Chunya kwa ajili ya utambuzi wa mali zao. Aidha, linatoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wakamatwe na kuchukulia hatua za kisheria.