TANZIA Bilionea Mustafa Sabodo afariki dunia

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,817
Nimepokea taarifa, mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo amefariki Dunia. Sabodo ametokea mkoani Lindi na alijenga shule maarufu kule pia alifadhili chama cha upinzani cha Chadema


======


images (30).jpeg

Mustafa Sabodo alizaliwa mwaka 1942 mkoani Lindi na alipata kusema ametoka kwenye familia yenye utajiri wa imani na fedha.

"Mimi nimetoka kwenye familia ya Uislamu wa Kihindi wa Gujarati Khoja, nilijitahidi kupambana dhidi ya umaskini nikiwa na matarajio ya kuwa tajiri na ninamshukuru Mungu nimekuwa hapa nilipo,"alisema.

Licha ya kupooza sehemu ya mwili wake mwaka 2000, Sabodo aliendelea kufanya kile anachotaka ikiwemo kusimamia miradi yake na ya jamii kuhakikisha inafanikiwa ikiwemo kuchimbia visima zaidi ya 280 nchini.

Licha ya kutoka kwenye familia ya utajiri baadaye alifilisika na akapambana dhidi ya kufilisika huko kwa kuweka matarajio ya kuwa tajiri na baadae akawa.

ELIMU
Kielimu, Sabodo alisoma Shule ya Sekondari ya Lindi na baadaye alihitimu ngazi ya cheti kwenye Chuo cha Cambridge.

Baadaye alihitimu Chuo cha Edinburg nchini Uingereza mwaka 1965 ambapo alisoma sheria ya biashara na usimamizi wa mifuko ya fedha.

Baadaye aliishi nje ya Tanzania kwa kufanya kazi ya ushauri wa kimataifa na kurejea nchini mwaka 1996 na kuwekeza.

MOYO WA KUJITOLEA
Mwaka 2003 Sabodo alitoa udhamini wa uchezeshaji wa bahati nasibu ya mfuko wa Mwalimu J.K Nyerere wenye thamani ya Sh 100 milioni.

Wazo la kuanzishwa kwa mfuko huo wa Mwalimu Nyerere lilikuwa la Sabodo, pia alichangia Sh 1.3 bilioni katika kuufanikisha.

Pia Sabodo amechangia miradi mbalimbali ikiwemo kutoa kiasi cha Sh 5 bilioni kwa ajili ya kuchangia chuo cha ualimu cha elimu ya juu cha Mtwara, alichangia Sh 965 milioni kwa ajili ya upanuzi wa majengo ya hospitali ya Shree Hindu Mandal, mradi wa Khoja Shia-aheri Sh 1.6 bilioni.

Sabodo licha ya kuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), alitoa Sh 100 milioni kwa ajili ya kukipongeza chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ajili ya ushindi wa kiti cha Ubungo alichoshinda Joshua Nasari wa jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha wakati huo.

Pia alitoa baskeli 100 na kuahidi kuchimba visima vitano katika jimbo hilo.

======

KSI Jamaat of Dar es Salaam, Tanzania

Death Announcement

‎إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعون
”Surely we belong to Allah and to Him shall we return”.


It is with sadness that we share the news of demise of MUSTAFA RAJABALI JAFFER (SABODO) has passed away in Dar Es Salaam.

More Details To Follow...

Kafan - Dafan Committee
 
KSI Jamaat of Dar es Salaam, Tanzania

Death Announcement

‎إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعون
”Surely we belong to Allah and to Him shall we return”.


It is with sadness that we share the news of demise of MUSTAFA RAJABALI JAFFER (SABODO) has passed away in Dar Es Salaam.

More Details To Follow...

Kafan - Dafan Committee
Buriani, nakumbuka alikataa kuniuzìa eneo lake la Mwenge jirani na ITV. Kwa kuwa yeye ni tajiri, nilimuomba aniuzie kwa milioni kumi.
Mungu ampunguzie adhabu ya kaburi
 
Poleni CCM kwa kuondokewa na kada wenu.
Ila CCM na vyama vya upinzani hasa CHADEMA mmekula sana pesa ya Sabodo.
Poleni wote kabisa.
RIP
Duniani hakuna kada wa CCM, kuna wasaka tonge kupitia CCM kwa vile iko madarakani, inagawa vyeo, inarutubisha rushwa and the like! Makada/makamanda wa kweli wako Chadema! hakuna vyeo vya kugawa, chadema has nothing in terms of vyeo, mahela, rushwa..... lkn tuna Imani mioyoni mwetu na Chadema. Chadema ni IMANI Erythrocyte
 
Back
Top Bottom