TANZIA Shekhe Basaleh Afariki Dunia. Aliitetea vyema imani akiwa mwanzuoni

Mtanzania2020

JF-Expert Member
May 23, 2020
368
763
FB_IMG_1690738765034.jpg

Mwanazuoni na sheikh maarufu Maalim Basaleh amefariki dunia leo Jumapili katika Hospitali ya Aga Khan alipokuwa akipatiwa matibabu akisumbuliwa na matatizo ya figo na saratani.

Mtoto wa marehemu Abdullatif Ali Basaleh amesema baba yake amefariki saa 12 jioni baada ya kulazwa kwa takribani wiki mbili na nusu akipatiwa matibabu hayo. Amesema mazishi ya baba yake yatafanyika kesho saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu.

"Leo baba amefariki dunia si muda mrefu kesho tutakwenda kumpumzisha baada ya swala ya Adhuhuri," amesema Abdullatif.

Rafiki wa karibu wa Basaleh, Sheikh Issa Ponda ameliambia Mwananchi kuwa mwanazuoni huyo alikuwa amebobea katika masuala ya dini na kijamii. Amesema Sheikh Basaleh amewahi kuwa mwalimu wa shule za sekondari Unguja.

"Aliwahi kuwa mhadhiri mkubwa wa Kiislamu, baada ya kufariki Sheikh Abood Maalim yeye ndiye alibaki akiongoza mihadhara linganishi yaani hoja tofauti za itikadi mbalimbali. Atakumbukwa zaidi namna alivyopigania watoto wa kike kuvaa hijabu shuleni na Rais wa wakati huo (Ali Hassan Mwinyi), akaridhia.

" Haikuwa kazi ya kufanikiwa katika hili kwasababu alipata misukosuko kwa sababu yalifanyika maandamano aliyoyaongoza. Alikamatwa na polisi na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, lakini mwisho wa siku vazi liliruhusiwa," amesema Sheikh Ponda.

Kwa mujibu Sheikh Ponda, Basaleh amezaliwa mwaka 1947 mjini Unguja amesomea Zanzibar na kufanya kazi ya ualimu akifundisha masomo ya Kiingereza na Kiarabu.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwanazuoni na sheikh maarufu Maalim Basaleh amefariki dunia leo Jumapili katika Hospitali ya Aga Khan alipokuwa akipatiwa matibabu akisumbuliwa na matatizo ya figo na saratani.

Mtoto wa marehemu Abdullatif Ali Basaleh amesema baba yake amefariki saa 12 jioni baada ya kulazwa kwa takribani wiki mbili na nusu akipatiwa matibabu hayo.Amesema mazishi ya baba yake yatafanyika kesho saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu.

"Leo baba amefariki dunia si muda mrefu kesho tutakwenda kumpumzisha baada ya swala ya Adhuhuri," amesema Abdullatif.

Rafiki wa karibu wa Basaleh, Sheikh Issa Ponda ameliambia Mwananchi kuwa mwanazuoni huyo alikuwa amebobea katika masuala ya dini na kijamii.Amesema Sheikh Basaleh amewahi kuwa mwalimu wa shule za sekondari Unguja.

"Aliwahi kuwa mhadhiri mkubwa wa Kiislamu, baada ya kufariki Sheikh Abood Maalim yeye ndiye alibaki akiongoza mihadhara linganishi yaani hoja tofauti za itikadi mbalimbali. Atakumbukwa zaidi namna alivyopigania watoto wa kike kuvaa hijabu shuleni na Rais wa wakati huo (Ali Hassan Mwinyi), akaridhia.

" Haikuwa kazi ya kufanikiwa katika hili kwasababu alipata misukosuko kwa sababu yalifanyika maandamano aliyoyaongoza.Alikamatwa na polisi na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, lakini mwisho wa siku vazi liliruhusiwa," amesema Sheikh Ponda.

Kwa mujibu Sheikh Ponda, Basaleh amezaliwa mwaka 1947 mjini Unguja amesomea Zanzibar na kufanya kazi ya ualimu akifundisha masomo ya Kiingereza na Kiarabu.

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshatifa
 
Tanzania imepata pigo la kuondokewa na mwanazuoni na kiongozi wa Dini maarufu Shekhe Basaleh; mazishi ya kiongozi huyu wa dini wa yatafanyika kesho.

Poleni watanzania , poleni wanafamilia na pole nyingi kwa Shekhe Ponda kwa kumpoteza mshauri na kiongozi wa kiimani.

Tutaenzi matendo yake ikiwemo sifa kuu yakupigania haki.
 
View attachment 2703218

Mwanazuoni na sheikh maarufu Maalim Basaleh amefariki dunia leo Jumapili katika Hospitali ya Aga Khan alipokuwa akipatiwa matibabu akisumbuliwa na matatizo ya figo na saratani.

Mtoto wa marehemu Abdullatif Ali Basaleh amesema baba yake amefariki saa 12 jioni baada ya kulazwa kwa takribani wiki mbili na nusu akipatiwa matibabu hayo.Amesema mazishi ya baba yake yatafanyika kesho saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu.

"Leo baba amefariki dunia si muda mrefu kesho tutakwenda kumpumzisha baada ya swala ya Adhuhuri," amesema Abdullatif.

Rafiki wa karibu wa Basaleh, Sheikh Issa Ponda ameliambia Mwananchi kuwa mwanazuoni huyo alikuwa amebobea katika masuala ya dini na kijamii.Amesema Sheikh Basaleh amewahi kuwa mwalimu wa shule za sekondari Unguja.

"Aliwahi kuwa mhadhiri mkubwa wa Kiislamu, baada ya kufariki Sheikh Abood Maalim yeye ndiye alibaki akiongoza mihadhara linganishi yaani hoja tofauti za itikadi mbalimbali. Atakumbukwa zaidi namna alivyopigania watoto wa kike kuvaa hijabu shuleni na Rais wa wakati huo (Ali Hassan Mwinyi), akaridhia.

" Haikuwa kazi ya kufanikiwa katika hili kwasababu alipata misukosuko kwa sababu yalifanyika maandamano aliyoyaongoza.Alikamatwa na polisi na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, lakini mwisho wa siku vazi liliruhusiwa," amesema Sheikh Ponda.

Kwa mujibu Sheikh Ponda, Basaleh amezaliwa mwaka 1947 mjini Unguja amesomea Zanzibar na kufanya kazi ya ualimu akifundisha masomo ya Kiingereza na Kiarabu.

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshatifa
Pole Kwa family.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom